LHRC yamuonya Oscar Oscar kwa Vitendo vya Udhalilishaji dhidi Wanawake

LHRC yamuonya Oscar Oscar kwa Vitendo vya Udhalilishaji dhidi Wanawake

Sioni Tatizo katika post zake anazoandika. sana sana kutakuwa na tatizo kama alishawahi kutolea ufafanuzi huwa anamaanisha nini, hakuna tusi, dhihaka wala chochote cha udhalilishaji.

Hata mbunge msukuma alishawahi kusema vitoto vya miaka 10 vinavaa sidiria Sijui ni wapi alichukuliwa hatua za kisheria.

Kama kuna post ambayo oscar aliandika anadhalilisha wanawake iwekwe hapa. Kama hakuna basi aachwe au aulizwe anamaanisha nini.

Mama yangu Anna Henga kwa hapa kafeli sana
Wangeanza kumchukulia hatua Kikwete kwanza aliyesema "ili ule lazima nawe uliwe"
Kisha akasema "Kikwete hii hachomoi nikauliza kwani nimechomeka nini?"
Ni ngumu sana kuunda kesi ya maana kwa memes au kauli kama hizo.
 
LHRC njooni kwanza mtujibu, kwani mwanamke sio chombo cha starehe kwa mwanaume?
Kama jibu sio, kwanini wanajiuza?
Huko kwa makungwi mwanamke anaandaliwa kumstarehesha mwanaume kwa chakula, mavazi, sauti, na mibinuko ya kitandani. Hii yote lengo lake nini kama si kumstarehesha mwanaume?
Haya, kafungueni kesi kama mna hoja za kuishawishi mahakama kwamba bwana Oscar ana kesi ya kujibu.

Huyo bwana amevunja maadili ya Kitanzania (ethics). Ethics is all about what is wrong and right based on the conduct of the people in relation to the society. Wala si kuvunja sheria.
Kwani kutomwamkia baba mkwe Mtanzania mwenzako ni kosa kisheria? Ila sio maadili ya Mtanzania.
 
Wangeanza kumchukulia hatua Kikwete kwanza aliyesema "ili ule lazima nawe uliwe"
Kisha akasema "Kikwete hii hachomoi nikauliza kwani nimechomeka nini?"
Ni ngumu sana kuunda kesi ya maana kwa memes au kauli kama hizo.
Tatizo wabongo huwa tunalalamika watu wanapofanya maovu. Cha kushangaza hatua zikichukuliwa tunalalamika tena na kuwatetea.
 
Tatizo wabongo huwa tunalalamika watu wanapofanya maovu. Cha kushangaza hatua zikichukuliwa tunalalamika tena na kuwatetea.
Ulisikia wapi nimelalamika habari za Oscar? Mi naona anajifurahisha tu. Haya, siku zote hizi walikua wapi?
Leo ndio wamejua anakosea? Au walishampa onyo amekaidi?
 
Back
Top Bottom