Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kuna kitu kimoja ambacho nakichukia kupita kiasi katika maisha yangu ya U-Tanzania. Hiki ni kauli za Polisi au wanasiasa pale ambapo wanajaribu kuficha au kupotosha ukweli ambao ukiwekwa wazi wananchi wataona wanavyokiuka haki za msingi za Watanzania, wanavyokandamiza demokrasia au hata wanavyofanya uhalifu kama wanasiasa au polisi.
Nadhani mmesikia kauli za polisi za "waliuwawa katika mapambano makali ya silaha na polisi na hakuna askari aliyejeruhiwa", "aliuwawa na kitu cha ncha kali tunafanya uchunguzi", "alikufa kwa kujaribu kuruka toka kwenye gari akiwa na pingu" nk.
Na pia kauli za wanasiasa kama "kama hutaki tozo nenda Burundi"; "kama huna nauli piga mbizi"nk.
Sasa leo nimekutana na kauli ya Waziri wa Mambo ya Nchi za nje, Liberata Malamula, akijaribu kueleza kwa nini mkutano kati ya Raisi Samia na wapinzani haukutokea. Anasema "Raisi Samia alipanga kukutana na wapinzani lakini ratiba zikaingiliana". Hivi huu mkutano ulikuwa ufanyike kwa muda gani, miezi sita mfululizo?
Ni wazi kwamba hawa watu wanapotoa hizi kauli wanaona sisi Watanzania ni wajinga, hatuna akili na tanakubali lolote tutakaloambiwa.
Kwa kiingereza huwa ni falsafa ya "insulting Tanzanians' intelligence"
Napenda kwa mara nyingine niwaambie Polisi na Wanasiasa jambo moja, kwamba mtitutukane Watanzania, msidhani kwamba hatuna akili, na msione upole wetu na utunzaji wetu wa hali ya amani nchini kuwa ni watu ambao tupotupo tu kama mazezeta. Uvumilivu wa kutukanwa una mipaka yake, na mnatutukana sana kwa hizi kauli zenu.
Hizi ni kauli zinafanya niwachukie wanasiasa na polisi kwa kiwango cha juu kabisa, kwa kuwa ni kauli ambazo naziona kama matusi kwa Watanzania. Ninavyozitafsiri mimi ni kwamba mnatoa kauli kama hizo eidha kwa kuwa nyie hamna uwezo wa kufikiri, au kwa kuwa mnadhani sisi Watanzania hatuna uwezo wa kufikiri. Jitafakarini sana. Tanzania ya 2021 sio Tanganyika ya 1961. We are not naive - you are disgustingly naive.