Ni kweli kabisa inabidi kizazi chote cha gadafi kipigwe marufuku kujihusisha na siasa libya;
kwa sababu gaddafi alisomesha walibya wote na kuwatibu bule, gaddafi alitoa posho ya dolla Elfu 5, kwa kila mwanamke aliyekuwa mjamzito kwa ajili ya kujikimu, gaddafi ndiye aliekuwa anawalipa mshahala waitimu wote wa chuo kama waajiliwa wengine mpka pale serikali itakapo wapa ajila, ndiye huyu huyu gaddafi aliyekuwa anauza mikate 40 kwa dolla moja, ndiye huyu huyu gaddafi asiyetakiwa kizazi chake kutawala tena libya kwa maana libya ya sasa tangu marekani na magaidi wenzie wavamie imekuwa sehemu salama kama peponi, uchumi umekuwa watu wanaamani hakuna vita, watu wanakula raha tu,
Unaweza ukatoa ushahidi shadidifu wa haya unayomsingizia Gaddafi kwamba aliwafanyia Raia wake au Ni mwendelezo wa stori za kwenye kahawa? Alitoa Dollar Elfu 5 kwa kila Mwanamke aliyekuwa akijifungua? Basi tuseme Ni kweli.
Kipindi Cha Gaddafi,idadi ya Walibya wote (2010) ilikuwa Milioni 6.5. hapo wanawake Ni wengi kuliko wanaume. Tuseme wanawake walikuwa Jumla 3.5M
Kati ya hao,tuseme Wajawazito Ni 600,000.
600,000 × $ 5,000 = $3,000,000,000
Hapo tunazungumzia Dollar 3B sawa na Tsh 7 Trillion kila Mwaka.
Eti alitoa Mishahara kwa waliomaliza vyuo Mpaka walipopata ajira za kazi Walizozisomea? Ngoja tuone.
Takwimu zinaonesha kwamba,Kila mwaka Wahitimu wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Kati nchini Libya walikuwa Elfu 70.
Tuseme Wasitani wa Mshahara wa kila mtu Ni $ 600 kila mwezi.
$ 600 × 70,000 = $ 42,000,000
$ 42M × 12 = $ 504M
Hapo tunazungumzia $ 504M sawa na Tsh 1.3 Trillion kila Mwaka.
Wakati wa Utawala wa Gaddafi kabla ya 2011,Nchi ya Libya ilikuwa na Jumla ya Wanajeshi Laki moja. Wastani wa Mshahara wa kila mwanajeshi kwa Mwaka ilikuwa Ni $ 1,200 kwa mwezi.
$ 1,200 × 100,000 = $ 120,000,000
Kwa mwaka Ni $ 120,000,000 × 12 = $ 1,440,000,000
Hapo tunazungumzia $ 1.44B sawa na Tsh 3.4 Trillion.
Pia,Ukiondoa Wanajeshi,Jumla ya wafanyakazi wengine wa Umma nchini Libya ilikuwa Laki 6 wakiwezo Walimu,Manesi,Madaktari,Wafanyakazi viwanda vya Mafuta,Polisi,Walinzi wa Misikiti,n.k
Wastani wa Mshahara wa kila Mfanyakazi ilikuwa $ 800 kwa mwezi
$ 800 × 600,000 = $ 480,000,000
Kwa mwaka Ni $ 480,000,000 × 12 = $ 5,760,000,000
Hapo tunazungumzia $ 5.76B sawa na Tsh 13.6 Trillion.
Ukijumlisha vyote hapo na vile ambavyo sijapiga hesabu ambavyo mnahadithiana kwamba Gaddafi alivifanya Libya enzi za Uhai wake Pesa inakuwa nyingi kuliko Pato ghafi la Nchi ya Libya.
Hapo inaonesha kwamba,huo UPUUZI wa eti aliwajengea Nyumba bure,kuwalipa mishahara wasio na ajira,Kuwalipa waliojifungua,Kuchangia gharama kwa 50% ya mtu kuagiza Gari nje, na mengine Ni hadithi za kusadikika. Na Kama yalifanyika Basi Ni kwa watu wachache(Upendeleo) na Sio kwa kila mwananchi.