Libya: Tume ya Uchaguzi yakataa maombi ya Urais ya Saif al-Islam Gaddafi


Hawezi kurudi mfwasi wa mabeberu huyu let the caged bird sings
 
Unaweza kuwa right kwa hoja lakini haitakaa itokee katika kizazi hiki. Kiongozi wa Marekani kushitakiwa kwenye mahakama yoyote nje ya Marekani yenyewe.

G. Bushi ameuwa maelfu ya innocent people, obama nae ivyo ivyo, tony blair, cameron, sarkozy n.k,,,,, sharon, netanyahu n.k hawa wameuwa sana wapalestina n.k lakini hawachukuliwi hatua.
 
Unaweza ukatoa ushahidi shadidifu wa haya unayomsingizia Gaddafi kwamba aliwafanyia Raia wake au Ni mwendelezo wa stori za kwenye kahawa? Alitoa Dollar Elfu 5 kwa kila Mwanamke aliyekuwa akijifungua? Basi tuseme Ni kweli.

Kipindi Cha Gaddafi,idadi ya Walibya wote (2010) ilikuwa Milioni 6.5. hapo wanawake Ni wengi kuliko wanaume. Tuseme wanawake walikuwa Jumla 3.5M

Kati ya hao,tuseme Wajawazito Ni 600,000.

600,000 × $ 5,000 = $3,000,000,000

Hapo tunazungumzia Dollar 3B sawa na Tsh 7 Trillion kila Mwaka.


Eti alitoa Mishahara kwa waliomaliza vyuo Mpaka walipopata ajira za kazi Walizozisomea? Ngoja tuone.

Takwimu zinaonesha kwamba,Kila mwaka Wahitimu wa Vyuo vikuu na Vyuo vya Kati nchini Libya walikuwa Elfu 70.

Tuseme Wasitani wa Mshahara wa kila mtu Ni $ 600 kila mwezi.

$ 600 × 70,000 = $ 42,000,000
$ 42M × 12 = $ 504M

Hapo tunazungumzia $ 504M sawa na Tsh 1.3 Trillion kila Mwaka.

Wakati wa Utawala wa Gaddafi kabla ya 2011,Nchi ya Libya ilikuwa na Jumla ya Wanajeshi Laki moja. Wastani wa Mshahara wa kila mwanajeshi kwa Mwaka ilikuwa Ni $ 1,200 kwa mwezi.

$ 1,200 × 100,000 = $ 120,000,000

Kwa mwaka Ni $ 120,000,000 × 12 = $ 1,440,000,000

Hapo tunazungumzia $ 1.44B sawa na Tsh 3.4 Trillion.

Pia,Ukiondoa Wanajeshi,Jumla ya wafanyakazi wengine wa Umma nchini Libya ilikuwa Laki 6 wakiwezo Walimu,Manesi,Madaktari,Wafanyakazi viwanda vya Mafuta,Polisi,Walinzi wa Misikiti,n.k

Wastani wa Mshahara wa kila Mfanyakazi ilikuwa $ 800 kwa mwezi

$ 800 × 600,000 = $ 480,000,000

Kwa mwaka Ni $ 480,000,000 × 12 = $ 5,760,000,000

Hapo tunazungumzia $ 5.76B sawa na Tsh 13.6 Trillion.

Ukijumlisha vyote hapo na vile ambavyo sijapiga hesabu ambavyo mnahadithiana kwamba Gaddafi alivifanya Libya enzi za Uhai wake Pesa inakuwa nyingi kuliko Pato ghafi la Nchi ya Libya.

Hapo inaonesha kwamba,huo UPUUZI wa eti aliwajengea Nyumba bure,kuwalipa mishahara wasio na ajira,Kuwalipa waliojifungua,Kuchangia gharama kwa 50% ya mtu kuagiza Gari nje, na mengine Ni hadithi za kusadikika. Na Kama yalifanyika Basi Ni kwa watu wachache(Upendeleo) na Sio kwa kila mwananchi.
 


Hii ndiyo libya ya gaddafi dikteta
hii ndiyo libya ya demokrasia
 
Kwahiyo hayo Magorofa ambayo hata hayajafikia idadi Yale yaliyoko Kariakoo ndio mnamsifu Gaddafi kwamba Alitoa Mishahara kwa wasio na ajira?

Kama shida Ni Magorofa mbona hata Kariakoo yamejaa? Basi na Watanzania wapewe Mishahara kwa wasio na ajira.
Fanya tafiti kabla hujaanza ku post pumba, gaddafi Kafanya mengi kwa nchi yake ambayo mtu kama wewe ukiambiwa utaona hayawezekani....... Nilikua hater wa Gaddafi kama wewe na kuamini chochote kinachorushwa na Western Media mpaka pale nilipojua nini maana ya Propaganda
Gaddafi aliondolewa kwa hila za Ufaransa, na Washirika wake (USA + NATO) baada ya kuona potential ya project yake ya Gold Dinar ambayo ingetikisa kwa kiasi kikubwa uchumi wa ufaransa

Kumuondoa, ikabidi wa fool watu kuwa Gadaffi ni dictator
Kama walivyosema Saddam Husein ana silaha za Nuclear, wakati hakua nazo

Marekani na washirika wake, wameharibu nchi nyingi zisizofata sheria zao kwa jina la Demokrasia, Democracy is flawed, inafanya vizuri kwenye nchi yenye watu 10,000 tu baada ya hapo ni useless, kila nchi ina uhuru wa kuwa na mfumo unaofanya kazi kwao, Gaddafi aliweza kusuka mfumo uliofanya kazi Libya

Now, umeiona Librya mpya baada ya ujio wa Demokrasia?
 
Mtoto wa Khadafi hawezi kuoitishwa kuwania Urais kutokana na shinikizo la Mataifa ya magharabi hata kama angepenya angetafutiwa mbinu za kumtoa pumzi - wazungu no watu wema hata kidogo.
 
Mbona hivyo vigorofa hata hapa Bongo vimejaa? Ndio vinawadanganya eti Maendeleo ya Libya? Utakuwa hujawahi Kufika Dar. Ukifika Dar hivyo vigorofa vya Libya Ni uchafu tu.View attachment 2024775View attachment 2024776

Wewe umetokea bushi nini? Hujaona pakutolea mfano ila dar uozo m2pu!!!! Yani wewe Unachoangaria ni magorofa na co maendeleo co!!! Mbona nchi nyingi tu duniani hazina magorofa marefu sana lakini economy yake Tanzania ikasome.
 
Hizi porojo hazina tofauti na zile za Wafuasi wa Kayafa wanapotetea Legacy mfu ya mungu wao mfu.
 
Niliwahi kusoma manifesto ta Saif, moja ya Agenda zake ni kuwa na Libya moja isiyo na Benghaz na Tripoli kama ilivyokua enzi za baba yake.
 
Kwahiyo hayo Magorofa ambayo hata hayajafikia idadi Yale yaliyoko Kariakoo ndio mnamsifu Gaddafi kwamba Alitoa Mishahara kwa wasio na ajira?

Kama shida Ni Magorofa mbona hata Kariakoo yamejaa? Basi na Watanzania wapewe Mishahara kwa wasio na ajira.

Endelea kuukaza ubongo
 
Hizi porojo hazina tofauti na zile za Wafuasi wa Kayafa wanapotetea Legacy mfu ya mungu wao mfu.

Kayafa hana legacy ndani ya nchi hii;na kama unaona nachosema mimi porojo basi sema wewe ambacho sio porojo;hoja upingwa kwa hoja na sio mipasho kama bunge la ndungai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…