Licha ya kuhusudu mabadiliko, siyo kila kitu kinapaswa kubadilishwa

Licha ya kuhusudu mabadiliko, siyo kila kitu kinapaswa kubadilishwa

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Mabadiliko yamefungamanishwa na kila kitu mfano miamba hubadilika, siasa hubadilika itikadi hubadilika, teknolojia hubadilika ....

Binadamu ndiye kiumbe wa pekee ambaye ameumbiwa "UTASHI" ambao unaomtofautisha na viumbe wengine wote kwani unamuwezesha siyo tu kuwa muhanga wa mabadiliko bali pia kuwa msababishaji wa mabadiliko.

Kuna watu ambao ni wahanga wa mabadiliko na kuna watu ambao ni wasababishaji wa mabadiliko lakini kuwa msababishaji ni sifa ambayo Mwanadamu ameumbiwa kwa asili yake na hiyo ya kuwa muhanga ni sifa ambayo Mwanadamu hujichagulia mwenyewe.

Leo karibu kila mtu anaimba wimbo wa mabadiliko na tumefikia hatua ya kuafiki kuwa kukua "growth" ndiyo mabadiliko "changes".Lakini tujiulize pamoja je ni kweli kuwa mabadiliko ni sawa na kukua? Kwa mfano Mtoto wa kiume au wa kike akikua na kufikia hatua ya uzee je anabadilika jinsia? Ni dhahiri tunaweza kuona ukuaji ila mabadiliko ni kitu kingine kabisa.

Kuna vitu ambavyo havipaswi kabisa kubadilishwa siyo tu katika maisha ya mtu binafsi bali hata katika ngazi ya Taifa. Mabadiliko yasiyokuwa na mipaka yake ni fedheha na yanaweza kuleta dhahama kubwa kwa jamii.

Kuna Nchi nyingi leo Duniani zimengia kwenye machafuko makubwa kutokana na kukimbilia kuhusudu mabadiliko bila kuangalia misingi isiyopaswa kuguswa.

Wanadamu wanaweza kuingia katika hasara kubwa sana kutokana na kukimbilia mabadiliko na kusahau misingi ambayo haupaswi kubadilishwa hata kidogo. Misingi hiyo ni nini basi?

Kuna misingi mikubwa miwili ambayo naweza kuiita sheria. Misingi hiyo ni;
(i) Sheria za asili(natural laws).
(ii)Sheria za kiroho(spiritual laws)

Sheria hizi mbili zikikiukwa iwe ni kwa kujua au kutojua matokeo mabaya lazima yaiandame jamii.

Jamii ya wanadamu inapokuwa watu kwenye mijadala na vikao muhimu vinavyolenga kusukuma mabadiliko wanaosimamia misingi hiyo miwili hujikuta ikifanikiwa sana kuliko watu wanaomsema misingi hiyo wanapokosekana.

Katiba za Nchi nyingi Duniani zimejaribu kuiweka misingi yake mwanzoni kabisa kwa lengo la kuhakikisha mabadiliko yoyote yanayohitaji na yatakayohitajika yanasadifu hitaji la msingi na hayauvuki mpaka wake.

Kupingana na sheria hizi mbili ni ujinga wa Mwanadamu unaweza kuleta hasara kubwa katika maisha ya mtu mmojammoja na pia kwa Taifa. Sharti kila jambo lipimwe kwa kuangalia sheria hizi mbili kama tunahitaji kufanikiwa.

Katika maisha ya kawaida hatupaswi kukubali na kupokea kila kitu kwa kuamini tu ni mabadiliko na ni maendeleo kwa sababu kuna mabadiliko unayoweza kutuondoa kwenye misingi ya uwepo wetu na kuuweka hatarini zaidi.

Embu tafakari juu ya fundisho hili la " TRUE NORTH" linalopatikana katika somo la Jiografia ambapo Ncha ya Kaskazini huchukuliwa kama upande rejeleo na usiobadilika unaosaidia kutambua upande nyingine. Kushindwa kuelewa ncha ya Kaskazini ni sawa na kushindwa kuelewa pande nyingine zote. "TRUE NORTH" inahesabika kama msingi wa kuelewa pande nyingine.

Fundisho hilo la " TRUE NORTH" linanifanya niafiki kuwa siyo kila kitu kinapaswa kubadilika. Misingi haibadiliki kwa sababu ndiyo mipaka ya mabadiliko. Kuiondoa misingi ni sawa na kuiondoa mipaka ya mabadiliko na kusababisha ukichaa Duniani.
 
Usipokubali mabadiliko, mabadiliko yatakubadilisha..
 
Back
Top Bottom