Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Tafadhali nisaidieni kuwajua wajumbe wa kamati ya Maadili ya CCM ... Naona wanatumia nguvu kubwa sana kumtosa Lowassa bila mafanikio!!! Sijui yeye akiaanza kuwatosa wapinzani wake itakuwaje ...
 

Mkuu umeongea kwa uchungu sana usijali iko siku watanzania wataujua ukweli nimewai kukaa private akaniambia hii nchi itakua ya asali na maziwa soon
 

Asante Mkuu JokaKuu kwa kutukumbusha kilichotokea back in 2005.Hawa Pro- Membe wanadhani sisi ni wajinga sana na tunaweza kutishwa na simple arguments za eti "Ridhiwan kaapa" who is Ridhwan by tha way? Kama kuna Mwenyekiti wa chama niliwahi kuamini ana msimamo dhabiti ukiondoa Mwl Nyerere,nilidhani alikuwa Mkapa,guess what? I was totally wrong,alisalimu amri kwa wanamtandao dakika za mwisho na akakubali yaishe.Sasa sijui hawa wanaokuja na hadithi za Ridhiwan kaapa kuhama Nchi EL akiwa mgombea wa Rais wanamtisha nani? Kwani Ridhiwan ndio ana hati miliki ya Nchi hii and he can decide who is the next President? EL wanae mpaka hatua za mwisho,waendelee kuhangaika nae huku sisi tunawasubiri na Mgombea wetu wa UKAWA.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu ulivyoipamba post yako utadhani unaemwandikia ndiye mgombea wa UKAWA!?kweli nimeamini sasa EL akipita hakuna UKAWA!
 
Last edited by a moderator:
[h=3][/h]
Ili kuondokana na Kisingiti hii na muamvuli huu wa Uvyama. Kuna haja wapenda haki kufungua Kesi ya Kikatiba kwa Hati ya dharura-huu ndio muda na wakati wa Mgombea Binafsi kurudi kwenye historia ya Nchi yetu.

Waheshimiwa wote wenye kutishwa na Vyama vyao pambaneni kutafuta na kuipata haki hii ya Kikatiba.



 
Kumbe ni walewale! Lowasa naye kajiunga na ukawa?
 
Lowassa ni mwizi hafai kuwa kiongozi. Lowassa ni fisadi hafai kuwa kiongozi, huko kupendwa na wengi siyo bali ananunua kupedwa

Uthibitisho khs kauli yako tafadhar usiamin kila unachoambiwa, akili ya kuambiwa changanya na ya kwako ndg,kununua watu hayo maneno yanasemwa na mahafidhina wasiolitakia mema taifa letu
 
Watanzania wa leo wemeelika wameerevuka, lakini wakimpa lowassa Ikulu ntaamini Taifa hili ni kichwa cha mwendawazimu
 
Nyamizi,

..lakini usiwategemee sana hawa wa-Tz.

..hawaeleweki wanataka nini haswa.


..UKAWA wana kazi kubwa kwelikweli bila kujali CCM watamsimamisha nani.

cc Gagnija
Kwenye uchaguzi wa mitaa uliopita wameonyesha wanachokitaka. Kile kilichoelezwa na serikali kwamba ni dosari na hivyo kuahirisha uchaguzi hazikuwa dosari. Ni baada ya kubaini kipigo walichokuwa wanakwenda kukipokea hivyo wakapanga namna ya kuepuka aibu. Oktoba ni kiama kwa watawala wa sasa.
 
ngoja sheria ya makamba iipite....
 
Mimi navyoona ni Lowassa anayetumia nguvu kubwa sana dhidi ya wenzake. Humu JF watu wote ni against Membe, against January against Pinda yaani zinatungwa hadithi hadi Wachungaji kuzua hoja dhidi ya mtu yeyote anayesimama dhidi ya Lowassa maana wameisha lewa na nguvu ya kiza.

Nitakuwa mpumbavu nilioje, nikiamini kwamba Lowassa anaonewa ikiwa magazeti yote nchini ni Lowassa, wanamuziki Lowassa, wachekeshaji Lowassa, makanisani na misikitini Lowassa..yaani huyu Lowassa anapendwa kama Katiba ya Wananchi (tume ya Warioba). Halafu hao hao wanakuja sema Lowassa anatengwa. Ama kweli Miafrika Ndivyo Tulivyo!
 
Atakayetaka kuona ccm inawekwa jumba la makumbusho
milele amuengue EL.2015 ni wazi EL hakwepeki iwe kupitia upinzani
au ccm yenyewe,sababu ni kwamba kwa jinsi alivyopita kwenye mikikimikiki
ataiweza tanzania tuitakayo.
Kwa mawaziri wakuu tuliowahi kuwa nao ukimuondoa sokoine hakuna anayemfikia EL kiutendaji japo alitumika muda mfupi sana.
Hivyo ataiweza TZ.
 

Daah,nimekuelewa mkuu huyu Lowasa asipopitishwa patachimbika ccm,ngoja tuone itakuwaje ila jina lake likipitishwa hana haja ya kufanya kampeni
 

..na sisi tunawaombea iwe hivyo.

..itokee kama Nigeria ambapo chama tawala wamepata kipigo mpaka mgombea wao akasalimu amri kabla hata tume ya uchaguzi haijamaliza kuhesabu kura zote.
 
Mkandara,

..hii michezo Lowassa alianza kuifanya tangu mwaka 95.

..alipumzika hapa katikati ili kumpa nafasi JK kwa "makubaliano" maalum.

..sasa this time inaonekana Lowassa doesn't wanna take any chances.

..hivi kipenga hakijapulizwa mambo yako hivi. wakiruhusiwa ku-campaign itakuwaje?

cc Pasco, Gagnija, Nyamizi
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…