..mimi sidhani kama Kikwete anaweza kumtupa Lowassa.
..hawa wametoka mbali mno, tangu mwaka 95 na inawezakana kabla ya hapo.
..Lowassa ametoa mchango mkubwa sana kumfikisha Kikwete hapo alipo.
..hata ile kashfa ya Richmond, Lowassa took the hit kuwakinga wengine.
..kumbuka Dr.Mwakyembe alisema kuna mambo hawajayatoa ili kutoiabisha serikali. Lakini ripoti hiyo ilifikia mpaka kumuaibisha Waziri Mkuu, sasa huyo aliyefichiwa mambo yake alikuwa nani?
..Nakubali kwamba JK anazijua sana siasa za nchi hii, lakini sidhani kama ni mtu katili mwenye kuweza kumdhulumu mtu waliyetoka naye mbali na aliyemhangaikia kama Edward Lowassa.
cc
Pasco