Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

daaaah sijui ni uelewa wangu mdogo ama vipi ila kiukweli sijaona jambo kubwa alilolifanya lowasa hadi makundi yaandamane kwenda kwake.....
 
daaaah sijui ni uelewa wangu mdogo ama vipi ila kiukweli sijaona jambo kubwa alilolifanya lowasa hadi makundi yaandamane kwenda kwake.....

..kwani JK alikuwa amefanya jambo gani kubwa?

..mbona wananchi walimchagua, tena kwa kishindo?

..hizi ni siasa kibongo-bongo, rekodi/uwezo siyo kigezo cha kuchaguliwa nchi hii.

cc Mkandara, Kiranga, Pasco
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka sana na bahati mbaya sijui hawa watu wa Lowassa wanafikiri sisi wajinga kiasi gani maana kila siku kazi kubwa ni kuwashambulia wagombea wenzake na maandalizi yao ni dhidi yake tu sio kwamba wanafaa kuwa viongozi. Sasa Lowassa alitaka kugombea peke yake hii nafasi au?

Kibaya zaidi basi kampeni zenyewe wanazifanya Kitaifa kana kwamba taifa zima ni CCM badala ya kujiandaa na uchaguzi wa chama. Huwezi kuwa chaguo la wananchi hata huna baraka za chama chako na kibaya zaidi wote wanaokwenda kumuomba achukue fomu sio hata wanachama wa CCM - huoni maajabu haya...

Hivi kweli akienguliwa atabakia vipi CCM nani atamshika mkono maana wagombea wengine woote kisha wapaka nani atamvumilia.Labda kweli anafikiri UKAWA watampokea au pengine sheria hiyo ya Mgombea binafsi ipo kwa sababu yake na Katiba Pendekezwa ndio hivyo inapigwa panga, yaani namhurumia kuliko anavyojitambua.
 
Sasa hako kakamati ka maadili ndiyo sauti ya wengi, basi wafanye hivyo!! Ni wazi, wakimwaga mboga na sisi tunamwaga ugali. Na kama mbwaa na iwe mbwaa! Kura zote zitakwenda UKAWA!
 
Tutarajie vifo kwa baadhi ya watu.
 
Nikiangalia hali ilivyo na ndoto za lowassa za kukalia kiti cha urais toka enzi ya mwalimu. Ikitokea Ccm wakakata jina lake basi ni wazi hata maisha ya mzee huyu hayatokuwa na mdamrefu duniani

Mimi sio mungu ila kiuhalisia naona msungo mkubwa wa mawazo wa lowassa akikosa nafasi ya kuwa mgombea na msongo wa mawazo ni maradhi mabaya mno na huwa husababisha vifo vya ghafla.

Kamati kuu ya Ccm msaidieni EL aendelee kuishi bado ni kipenzi cha wengi pamoja na mapungufu yake kama binadamu.
 
Niliwahi andika kitu kama hiki na nikashambuliwa sana.Ngoja nione leo itakuwaje kwa upande wako.
 
Hivi kuna binadamu anaamini ccm ya leo inaweza kumkata lowassa:what::what::what:hivi hamjui Lowassa ndio ameishikilia ccm isianguke!
 
Niliwahi andika kitu kama hiki na nikashambuliwa sana.Ngoja nione leo itakuwaje kwa upande wako.


Kwahiyo akabidhiwe nchi sababu ya kuogopa atakufa?? Jiulize anapambana kote kuingia ikulu ili awasaidie watanzania? Au mnataka kuigeuza Ikulu kuwa pango la wanyang'anyi?
 
Pasco kweli nawe ni mweupe kanuni za ccm hakuna mahali kamati ya maadili inaweza kugusa kukata jina la mtu wao wanapeleka maoni yao ya kimaadili kamati kuu ndo inapendekeza majina umedanganywa
 
pasco umehaidiwa unikuru mkuu wa itakayokuwa ikulu ya lowasa au?nasikia tayari mshaanza kugawana vyeo.kila la kheri mkuu
 
pasco umehaidiwa unikuru mkuu wa itakayokuwa ikulu ya lowasa au?nasikia tayari mshaanza kugawana vyeo.kila la kheri mkuu

Sasa kinachowasha ni nini? Kukatwa kwa jina la Lowasa? Kwani mmesahau kuwa mtoto wa rais alishasema kuwa rais wa nchi hii hataweza kutokea kanda ya Kaskazini? Kwani tangu alipoitoa kauli hiyo akiwa uvccm iliwahi kukanushwa na mtu yeyote ndani ya uvccm au wa ndani ya ccm? So kutopitishwa kwa jina LA Lowasa ni utekelezaji wa kauli hiyo iliyoonyesha ubaguzi wa kikabila na kikanda, japo ccm watajaijutia.
 

Mkuu nimejitahidi kadri niwezavyo kurudia mara nyingi changio lako lakini bado sijapata mantiki yoyote ya kuniquote..msaada tafadhali yamkini waweza kuwa na maana iliyojificha.
 

Leo ndio kipenga cha CCM kinapulizwa!, hivyo hizi tetesi au zitathibitika au kuwa dismissed!.

Pasco
 
kuacha kumchagua mtu mwenye nguvu ya umma na pesa na marafiki wakubwa ni jambo la hatari sana kwa nchi yeyote, isitoshe, ameshaonyesha nia, labda wangemzuia kabla, lakini sasa is too late.

Wamechelewa sana... Watu wengi wanawazia mwaka huu tu, 2020 si mbali Lowassa akikosa, 2020 ndo atakuwa kashaanzisha chama chake mwenyewe.

Lowassa ana mbinu za sasa na baadaye, anajua siasa kuliko unavyodhani ,na NEC iseje ikajidanganya kumwacha. Kwani kiongozi ajaye atakuwa na wakati mgumu sana, anyway muda utaamua. Yetu macho...
 
Lazima kufuata taratibu na sheria kwani kama hana sifa ataachwa tu na kama akiachwa na kuleta fujo sheria zipo na lazima kufuata utawala wa sheria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…