Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!


Sasa wewe Pasco unalilia nini? Mwenyekiti wenu alishasema kuwa watu waliojitokeza hawana sifa akiwamo na EL, hivyo akawaomba wanachama kuwashawishi wagombea wengine, yeye lowasa kaamua kuwashawishi watu ili wamshawishi. So tegemea tetesi yako kuwa kweli coz wewe mwenyewe uko jikoni.
 
Mimi nadhani kama hawatampitisha na uku ikiaminika kuwa anaungwa mkono na watu wengi ndani na nje ya chama chake kwanini asigombee kupitia chama kingine.
 

Misconstrued feelings. No objective analysis.
Pole
 
kama tunaamini katika utafiti, wakimbwaga EL , nimefuatilia ni mara ya pili utafiti unaonyesha kuwa ni EL na Dr. Slaa, hayo tuachie ccm wataamua wenyewe, ila njia ya kwenda Ikulu mshale unagongea upande wa UKAWA kwa sasa, Mungu amechoshwa na ufisadi wa ccm , ameamua kuwapiga upofu wasijui la kufanya kuelekea October
 

Pasco you have conflict of interest in this EL tetesi story.
EL is your client, as PR firm, so the public should take such words as ‘Lowasa kipenzi cha Watanzania wengi' with maximum caution.
 

Watafiti wa aina hiyo ndio kuna mswada umepitishwa ili itungwe sharia wafungwe
 

Ndiyo maana Mkapa alikuita KANJANJA! Unaandika vitu ambavyo huna ujuvi navyo! Soma kwanza katiba ya CCM kabla ya kuleta vapour zako jukwaani.

FYI, Kamati ya maadili ya CCM haina uwezo na mamlaka ya kukuta jina la mgombea yeyote wa Urais wa JMT, hata kama mgombea huyo SIFA yake pekee ni UFISADI.

Kamati ya maadili ya CCM hujadili majina yote ya wagombea na kuyapatia grades A,B,C,D&F na kuyapeleka majina ya wagombea wote kwenye CC ya CCM.

Kikao chenye madaraka ya kukata majina ya wagombea ni CC ya CCM pekee yake.

User yako ni verified lakini bado unaandika vapour kiasi hiki!
 
Misconstrued feelings. No objective analysis.
Pole
Mkuu unapopinga kitu then we huonyeshi kitu kinachoweza tokea mbeleni basi we pia ni TATIZO.Sisi wengine tusio na vyama lakini tunao amini katika wana mageuzi wa kweli huwa tunampongeza mtu na kumkosoa mtu na kumuonesha namna ya kufanya.Sasa wewe unaonyesha kwamba ni hisia tu hakuna ukweli,Unasahau kwamba kila kinachozungumzwa au kutendwa huwa ni hisia tu kabla ya ukweli haujabainika.
 

Nakubaliana na wewe kaka hakuna msafi 100% kila huyu ana lake.
sasa mbaya zaidi, hao wengine ni watu wa hewala hewala lakini huyu Mh. hata kama ana mapungufu lakini ni mtu mchapa kazi, bora huyu kuliko mtu ambaye atakuwa hawezi hata kufungua mdomo kukemea pale panapoharibika.
hao ambao waliopo sasa hivi tumeshuhudia mangapi? Escrow hiyo bado inatikisa na hili ndio jinamizi la kufungia mwaka halijakata roho bado.

Kama tunataka msafi 100% basi tusubiri malaika toka mbinguni waje kutuongoza.
Nawasilisha
 
Halafu as journalist unapopata taarifa hutakiwi kuitoa kwa kuegemea upande mmoja na ushasema ni tetesi mbn km kwa upande mwingine ushaziamini tayari, kwa hiyo hata c wanajaJF unataka tuwe upande upi?
 
Pasco na wenzio naona kama ushabiki wenu kwa EL unataka kuvuka mipaka ya taratibu na kanuni za chama chenu. Hamuoni kuwa kelele zenu kwa siku za hivi karibuni zinaashiria kuwa mnajaribu kukitishia chama chenu kwamba kisithubutu kuliondoa jina la huyo mtu wenu katika kinyang'anyiro cha urais. Hakuna taasisi inayoweza kufaya kazi kwa kutegemea sauti za wapambe kama nyie. Hata hivyo EL siyo kipenzi cha Watanzania zaidi ya nyie mnaofanya yote haya kwa influence ya malipo
 
pasco wa jf siku hizi hueleweki,mara ulie na chadema,mara ccm!...,acha wafu wazikane
 
Kwani uko ccm nani msafi when it comes to Ufisadi?
Tena akikatwa jina ndo vzr coz naamini ana watu wengi tu humo ccm ambao ataondoka nao!!!
Lichama liendelee kuvunjika
 
Hivi kaka Pasco unaamini hadi leo kuwa Edward Lowassa atakuwa Rais wa Tanzania? Kwa lipi hasa? Mtakuwa na madodoki na magunzi mangapi kumsafisha? Kuongozwa naye ni pigo kwa nchi na vita dhidi ya ufisadi

Wewe unataka nani awe Rais, ebu tuondolee umasaburi wako hapa
 
Jaman hata EL angekuwa mkweli why asitoboe ukweli wote wa Richmond na hapo ndipo kashfa ya ufisadi itamuepuka lkn anapokaa kimyaa sasa anapokaa kimya anamaanisha nn, mtu anayetaka kugombea nafasi kubwa namna hiyo ya uongozi hlf ana tuhuma kubwa ya ufisadi na hataki kuutolea ufafanuzi wkt alisema angesema Nchi ingekuwa pabaya why asiseme na ni kikubwa gani ambacho anakiepuka km hao anaoogopa kuwataja leo cc tunawaona wasafi tena weupe hata kwa darubini hawana hata kirusi cha ufisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…