Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

Elections 2015 Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!

vinapatikana madukani sambamba na najisikia kuua tena, salamu toka kuzimu, malaika wa shetani, tutarudi na roho zetu, lazima ufe joram
PESA.jpg
 
Hakuna mwaka com waliwahi kuwa dilema kama mwaka huu!
 
kuacha kumchagua mtu mwenye nguvu ya umma na pesa na marafiki wakubwa ni jambo la hatari sana kwa nchi yeyote, isitoshe, ameshaonyesha nia, labda wangemzuia kabla, lakini sasa is too late.

Wamechelewa sana... Watu wengi wanawazia mwaka huu tu, 2020 si mbali Lowassa akikosa, 2020 ndo atakuwa kashaanzisha chama chake mwenyewe.

Lowassa ana mbinu za sasa na baadaye, anajua siasa kuliko unavyodhani ,na NEC iseje ikajidanganya kumwacha. Kwani kiongozi ajaye atakuwa na wakati mgumu sana, anyway muda utaamua. Yetu macho...

Hivi akiukosa urais mwaka huu EL atafika 2020?? Anyway, mnaomuunga mkono endeleeni kujipa moyo
 
kuacha kumchagua mtu mwenye nguvu ya umma na
pesa na marafiki wakubwa ni jambo la hatari sana kwa
nchi yeyote, isitoshe, ameshaonyesha nia, labda
wangemzuia kabla, lakini sasa is too late.
Wamechelewa sana... Watu wengi wanawazia mwaka
huu tu, 2020 si mbali Lowassa akikosa, 2020 ndo
atakuwa kashaanzisha chama chake mwenyewe.
Lowassa ana mbinu za sasa na baadaye, anajua siasa
kuliko unavyodhani ,na NEC iseje ikajidanganya
kumwacha. Kwani kiongozi ajaye atakuwa na wakati
mgumu sana, anyway muda utaamua. Yetu macho...
 
Atarudi kwake akalale,japo kisha nunuliwa atawawaomba wauze tembo.
 
Wanabodi,

Hii ni tetesi ya habari mbaya kwa wapenzi wa kipenzi cha watu, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kuwa pamoja na Mhe. Lowassa kuwa ndie mtu anayekubalika sana kuliko mtu mwingine yoyote ndani ya CCM, wale wasiolitakia mema taifa hili, wamepania kupanga njama za kumhujumu kwa kuhakikisha kuwa jina lake halitaingia hata ndani ya kikao cha CC kujadiliwa!, wamepanga kumchinjia baharini kwenye kamati ya maadili, itakayoyajadili majina wagombea kabla ya kuyaingiza kwenye Kamati Kuu, kujadiliwa!.

Mtoa habari wangu amesema kamati ya maadili ya CCM, itamchinja Lowassa kwa kumpa alama za chini kabisa kuliko wagombea wengine wote ili kuirahisishia kazi Kamati Kuu ambayo inatakiwa lazima itoke na majina matano kuyaingiza Halmashauri Kuu, ambapo mgombea rasmi wa CCM ameishachaguliwa, hivyo hili zoezi la kutangaza nia na kuomba uteuzi ni kwa lengo la kukamilisha tuu taratibu.

Sifa za Wagombea Watano watakao pitishwa na CC kuingia tano bora ya NEC ni hawa...
1. Mgombea mmoja mwanamke
2. Mgombea mmoja Muislamu
3. Mgombea mmoja kutoka Zanzibar
4. Mmoja wa Mawaziri Wakuu ambaye ameandaliwa kama kingio la huyo aliyeshachaguliwa!
5. Mgombea aliyeshachaguliwa kuipeperusha bendera ya CCM.

NEC itawapigia kura, ambapo mgombea tajwa, ataongoza kwa kura nyingi atasindikizwa na mgombea mmoja mmoja Mwanamke kutoka Zanzibar na Yule Waziri Mkuu Kingio, ambapo kwenye Mkutano Mkuu, wale wagombea wasindikizaji wawili watajitoa hivyo mgombea huyo kupaswa bila kupingwa kisha Wajumbe wa Mkutano Mkuu watapiga kura zuga tuu na matokeo, atakuwa amechaguliwa kwa asilimia 99%, na hiyo asilimia 1% itakayo mkataa ni kuzungia tuu kuwa CCM demokrasia!.

Lengo la hujuma hiyo ni kufuatia Lowassa kukubalika kupindukia, jina lake likifika tuu CC, hakuna wa kumkata, hivyo wahafidhina wa CCM, wanaounga mkono kambi ya mmoja wa wagombea, wameapa kuhakikisha jina la Lowassa, halivuki kisingiti cha kamati ya maadili, kwa kumchinjia rasmi baharini kwa kumpa maksi za chini, ili mgombea wao apete kwa mteremko!.

Naomba nisitaje chanzo cha habari hizi, kwa kutumia kanuni ya "the confidentiality of the source"
ila kwa vile hizi ni tetesi tuu, zitakapothibitika ndipo nitaweka source!.

Kama kawaida yetu jf, habari kama hizi ambazo hazijathibitishwa, zimeletwa humu hivi hivi zilivyopokelewa, ili wewe kama mwana jf, be the first to know!, na information is power!, hivyo kutoa fursa kwa wenye uwezo wa kuizuia hii mipango dhalimu inayopangwa, kutaka kuwakosesha Watanzaia mgombea kipenzi chao, chaguo la wengi, na mwenye uwezo usio tia shaka kuyamaliza matatizo yote ya taifa letu Tanzania.

Hii ni thread ya info tip, tuu, hivyo naomba nisiulizwe swali lolote kuhusu hii news tip for your info tuu.

NB. Chama cha Mapinduzi ni taasisi huru yenye uwezo wa kufanya shughuli zake kwa uhuru vile ambavyo wataona wenyewe inafaa, ikiwemo vigezo na jinsi ya kuwachagua wagombea wake, ila kwa sisi ambao ni wakereketwa wa mustakabali mwema wa nchi hii, kamwe hatutakubali, kuona watu wenye uwezo wa uongozi, wa kulibadili taifa hili kuwa nchi ya neema, na wanaokubalika na wengi, wakienguliwa kwa mizengwe tuu, kitu ambacho CCM imekuwa ikikifanya mara nyingi huko nyuma na ikabaki salama, hivyo kama ni kweli hiki ndicho walichopanga kukifanya this time!, hakitabaki sala!. Yaani CCM imekuwa ikiwaengua wagombea wazuri kwa mizengwe na ikabaki salama!, lakini this time, nimewasikia baadhi ya wana CCM kindakindaki, kuwa wamejiapiza, this time CCM ikimuengua chaguo lao kwa mizengwe, patachimbika!.

Pasco

acha upuuzi wako tumia akili yako
 
jamani tuacheni masiala tunapoelekea uchaguzi mkuu mwaka huu lowassa
amekuwa akizungumziwaa sana kuliko wagombea wote wa ccm....

Vijana wa boda boda karibia wote wanamuunga mkono lowassa.

Maeneo ya bar na sehemu za vinywaji lowassa amekuwa akizungumziwa kuwa anaonekana akiungwa mkono.....


Yaani sijui nini kimetokea kila mtu lowassa .......kila kona ya nchi lowassa amekuwa akizungumzia wapo wanaompinga ila asilimia kubwa wengi wanaonekana lowassa. ......


Swali jee ikitokea lowassa amekosa hiyo nafasi unadhani wapiga kura wake kura zao watapigia wapi......


Nadhani ccm bila kutumia busara huenda kura za lowassa zikaenda upinzani na ccm ndo tukawa tunaisahau........

Maana ukawa ..... Wameitege vibaya mnoo ccm wanajua ni wapi wataimalizaa
 
Amekuwa gumzo kwa kuwa anataka awe gumzo ili imsaidie kwenye mbio zake za sakafuni. Akikatwa jina kama inavyotarajiwa, maisha yataendelea kama kawaida.

Atapata wasaa mzuri kuangalia afya yake bila shaka.
 
Mungu kashasema lowasa ndio rais wa Tanzania ajaye,hawawezi kushindana na nguvu za Mungu

Hivi wewe una dini au unautani na hilo jina, haya ni uhuru wako kusema pia ukumbuke hilo jina lenyewe 'nipo ambae nipo'. Ndio shida ya kuiba kutaja jina la Bwana Mungu hovyo hovyo. Wenzako hata kusema Mungu waliona kosa hadi wanatumia 'bwana' lakini wewe mwezetu rahisi tu. Hata dini za asili wanamajina na hawaiti hivyo lakini wewe fasta tu. Haya nendelea uhuru ...
 
Mungu kashasema lowasa ndio rais wa Tanzania ajaye,hawawezi kushindana na nguvu za Mungu

Kama JK alikuwa chaguo la Mungu, basi na Lowassa atakuwa chaguaola Mungu.

Swali - ni Mungu yupi?

Ni Mungu wa haki, amani na upendo au ni mungu wa rushwa, ufisadi, wizi, uporaji na ujambazi?

Ni kama ni Mungu wa haki, amani na upendo, Lowassa hana chake!
 
lowasa n kila kitu anatisha sana mm mwenyewe wakimkata kura yangu ukawa
 
Back
Top Bottom