Licha ya mafanikio aliyoyapata Avcii nini kilimpelekea kujiua (suicide)?

Licha ya mafanikio aliyoyapata Avcii nini kilimpelekea kujiua (suicide)?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Majina yake halisi ni Tim Bergling amezaliwa septemba 8 mwaka 1989 Stockholm Sweden anafahamika zaidi kwa jina la Avcii alikuwa mkali wa EDM (Electronic Dance Music). Amefariki tarehe 20 Aprili mwaka 2018 Muscat nchini Oman chanzo cha kifo kujiua(suicide).

Alitengeneza Hits nyingi akishirikiana na baadhi ya wasanii kama Levels, Hey brother, addicted, The days, The nights, waiting for love, without you na nyinginezo nyingi.

Mimi BabaMorgan pamoja na ugumu wa maisha plus kusalitiwa kwenye mapenzi bado nina imani kuwa ipo siku ntakuwa na maisha ya furaha kwa hiyo bado naendelea kuomba kwa Mungu anipe miaka mingi ya kuishi ili nije kukutana na yale nayo yatumaini.

Kurudi kwenye mada kwa nini Avcii alijiua licha ya kuwa na mafanikio katika career yake ya muziki?

labda wazee wa intelijensia walifanya yao kwa sababu wanazozijua wao?

Note kujiua ni kifo kama ilivyo vifo vingine kwa maana kama umeandikiwa kufa kwa kujitoa uhai wako mwenyewe basi maandiko yatatimia waweza kuwa na kila kitu ila siku ukaangalia taarifa ya habari ukaona masikini wanateseka ukajifeel guilty ukaamua kujiua.

walizaliwa tarehe moja na Agnes Masogange na walikufa wote tarehe moja
From northern part of Tanzania.

images.jpeg
 
26 27 28 29
namba za kimkakati ukiwa STAR uliyeibuka ghafra na kupata mafaniko makubwa
ukivuka vizingiti vya miaka hiyo wewe umekomaa
Nini sababu nyuma ya pazia? Kimsingi maisha yana mengi ata movie star wetu The greatest Kanumba alituacha akiwa na age 28
 
Kofi cha Avicii kiliniuma kupitiliza, nilimkubali sana. Kuanzia Levels, SOS, Blessed, Wake Me Up, Waiting For Love, Hey Brother n.k.

Mental health is real. Hiyo video ni tribute ya life ya Tim Bergling aka Avicii 💔
 
Avicii mimi ni shabiki wake mkubwa. Kifo chake cha kujiua naamini kilitokana na kuwa na magonjwa mazito sana ambayo hakustahimili kuishi nayo. Tangu utotoni ana magonjwa makali na hivo alikuwa anaishi maisha tofauti kidogo. Alafu alijiua kwa vipande vya chupa ingawa familia yake ilitaka usiri sana kwenye kifo na mazishi walihudhuria waalikwa tu. Yeye mwenyewe alikuwa msiri

Pamoja na kutoa hits kali na kupendwa duniani kote ila niamini nikikwambia Avicii hakuwa akiishi kwa furaha. Alafu alikuwa ashaacha kufanya concerts, daktari wake nakumbuka muda fulani alimzuia baada ya kuzidiwa akiwa on stage.

I think pia aliwahi tumia drugs kupunguza makali yake. Sikuwahi sikia Avicii ana girlfriend wala kuonekana na mwanamke. Alikuwa mpweke sana.

Msanii yeyote asiye na mademu huwa namtilia wasiwasi. Labda aimbie madhabahuni
 
Kuna nyimbo yake moja naikubali, kali sana inaitwa wake me up ina 2 billion views youtube kama sikosei.

Jamaa alikuwa ni mtu anayependa kujiuliza maswali juu ya chanzo cha maisha na lengo la kuishi (kuwa duniani).
Alikuwa truth seeker. mtafuta ukweli juu ya maisha na uhalisia wake.
Jamaa alikuwa anapenda music na alikuwa mtu aliyependa kuwa perfect mpaka ikapelekea kuwa anafanya kazi kwa nguvu zote mpaka kupelekea kuwa na stress kupitiliza.

Baada ya kuacha kufanya tours alitaka kuwa na balance kwenye maisha yake kuwa na furaha na kufanya kitu anacho kipenda zaidi yaani Music.
Lakini jamaa bado alikuwa akisumbuliwa na mawazo ya "Kwanini" yaani kutafuta maana ya maisha, furaha nk
So baada ya muda jamaa maji yakamfika shingoni kwamba alishindwa kuishi namna hiyo, so akataka kutafuta amani (peace).
Solution ya kupata amani ya milele ni kufa, so akajitoa roho. Suicide kwa kipande cha chupa.

Pia jamaa alikuwa mtu wa matumizi mabovu ya painkillers na pombe kupitiliza mpaka kufikia hatua ya kucancel two world tours ambazo zingeingiza 2 million usd karibu 5 billion za kitanzania.
Jamaa hakuwa mtu wa biashara so akaiignore hiyo part bali alikuwa mtu aliyependa mashabiki zake kiasi cha kuogopa kuwadissapoint, alikuwa overachiever na perfectionist. na hii ni sababu moja wapo iliyopelekea kifo chake.

Siku zote ukitaka kujua ukweli kuhusu maisha na chanzo chake lazima akili yako ivurugike na kama hauna mind iliyo stable enough kuhimili Ukweli basi lazima uone kifo ndio option na hutokiogopa.

Kingine ni kwamba Binadamu na maisha ni kama mbwa anayekimbiza gari hatojua ataifanyia nini kama akiikamata.

You see wakati upo masikini au tuseme unapokuwa na plans na ambitions za kufikia mafanikio fulani uliyojiwekea basi tayari unakuwa na purpose ya kukufanya uendelee kuishi ila baada ya kufikia mafanikio uliyojipangia unakuwa hauna tena purpose. There's nothing there, ushafikia mafanikio uliyoyataka na labda kupitiliza now what?, what is the point and where's the point?.

Unaona? mbwa ameikamata gari lakini hajui hata nini cha kuifanya. now hayo ndio maisha yalivyo.
Heath Legder aka The joker himself once said this: I'm a dog chasing cars, I wouldn't know what to do with one if I caught it.
 
Kuna record ya msanii mmoja alitoa kibao cha kuhuzunisha ambacho kilibamba sana afu baadaye mchizi akajiua, baade watu wengi wengi waliosikiliza ile ngoma walijiua.

Mpaka ikapelekea nyimbo kufungiwa kutokana na idadi ya watu kujiua baada ya kusikiliza ile ngoma imekua ikiongezeka
 
Inaitwaje hiyo ngoma?
 
Kuna nyimbo yake moja naikubali, kali sana inaitwa wake me up ina 2 billion views youtube kama sikosei.

Jamaa alikuwa ni mtu anayependa kujiuliza maswali juu ya chanzo cha maisha na lengo la kuishi (kuwa duniani).
Alikuwa truth seeker. mtafuta ukweli juu ya maisha na uhalisia wake.
Jamaa alikuwa anapenda music na alikuwa mtu aliyependa kuwa perfect mpaka ikapelekea kuwa anafanya kazi kwa nguvu zote mpaka kupelekea kuwa na stress kupitiliza.

Baada ya kuacha kufanya tours alitaka kuwa na balance kwenye maisha yake kuwa na furaha na kufanya kitu anacho kipenda zaidi yaani Music.
Lakini jamaa bado alikuwa akisumbuliwa na mawazo ya "Kwanini" yaani kutafuta maana ya maisha, furaha nk
So baada ya muda jamaa maji yakamfika shingoni kwamba alishindwa kuishi namna hiyo, so akataka kutafuta amani (peace).
Solution ya kupata amani ya milele ni kufa, so akajitoa roho. Suicide kwa kipande cha chupa.

Pia jamaa alikuwa mtu wa matumizi mabovu ya painkillers na pombe kupitiliza mpaka kufikia hatua ya kucancel two world tours ambazo zingeingiza 2 million usd karibu 5 billion za kitanzania.
Jamaa hakuwa mtu wa biashara so akaiignore hiyo part bali alikuwa mtu aliyependa mashabiki zake kiasi cha kuogopa kuwadissapoint, alikuwa overachiever na perfectionist. na hii ni sababu moja wapo iliyopelekea kifo chake.

Huyu jamaa ni completely me except mimi sinywi pombe na sitocommit suicide, ukitaka kujua ukweli kuhusu maisha na chanzo chake lazima akili yako ivurugike na kama huna mind iliyo stable enough kuhimili Ukweli basi lazima uone kifo ndio option na hutokiogopa.

Kingine ni kwamba Binadamu na maisha ni kama mbwa anayekimbiza gari hatojua ataifanyia nini kama akiikamata.

You see wakati upo masikini au tuseme unapokuwa na plans na ambitions za kufikia mafanikio fulani uliyojiwekea basi tayari unakuwa na purpose ya kukufanya uendelee kuishi ila baada ya kufikia mafanikio uliyojipangia unakuwa hauna tena purpose. There's nothing there, ushafikia mafanikio uliyoyataka na labda kupitiliza now what?, what is the point and where's the point?.

Unaona? mbwa ameikamata gari lakini hajui hata nini cha kuifanya. now hayo ndio maisha yalivyo.
Heath Legder aka The joker himself once said this: I'm a dog chasing cars, I wouldn't know what to do with one if I caught it.
Ukiyafikia mafanikio uliyoyataka, unapambana umaintain palepale.

Sema nyie wasoma vitabu sana na wazee wa kureason sana mna kazi kichizi.
Kuna mwanangu nae naona anaishi kwa shida baada ya kusoma soma vitabu na kuanza kuviishi alivyovisoma.

Sioni shida katika kusoma vitabu lakini je ni kipi cha kweli na kipi si cha kweli. Vitabu vinaelimisha lakini vile vile vinapotosha ni uchambuaji wako tu.
 
Ndio hata mimi naiona ya kawaida au sijui imepoteza mvuto kwasababu imekua translated, lakini ndio nyimbo inayoongoza mpaka sasa kusababisha watu wajiue
duuu bas tumeumbwa tofaut,kwangu ni ya kawaida mnoo tena mno na imenitia uvivu kuimaliza
 
Back
Top Bottom