Paulsylvester
JF-Expert Member
- Oct 15, 2021
- 1,464
- 3,379
Staki nirudie mambo mengi tu ambayo kila leo yanasemwa na kuandikwa hapa jukwaani kuhusu ughali wa maisha n.k nadhani mh Rais ameamua kuyaacha ili kuandikwe historia nyingine mpya Katika nchi yetu, ambapo watanzania watakuwa kila wakikumbuka kuhusu hayo, basi linatajwa na jina la mh Rais wetu kwamba kulikuwa ni kipindi cha uongozi wake.
Kwa heshima na taadhima, sisi watanzania wa hali ya chini, ambapo maisha yetu yanategemea saaana nishati ya umeme katika kujiletea maendeleo yetu.
Tulifadhaika saana baada tu ya hali ya hewa na mvua kutokunyesha Kwa wakati, ambapo kumesababisha mabwawa ya kuzalishia umeme kukauka na kuleta mgao mkali wa nishati hiyo!
Mitaji yetu imeyumba saaana kutokana na ukweli kuwa, bila nishati hiyo, maisha yanakuwa magumu sana kwetu!
Kwa tarifa iliyotolewa mwezi December mwanzoni kabisa na wizara ya Nishati kuwa, Bwawa la JKNHP litaanza kujazwa tarehe 15/12, ilitutia moyo saaana!
Cha kushangaza ni kuwa, hakuna tena tarifa za kujazwa Kwa bwawa hilo, maana yake ni kwamba, Waziri anayesimamia wizara hii, wananchi tumeanza kuingiwa na hasira naye, ni bora sasa Mh Rais, umtoe hapo Kwa sababu si tu kwamba hafai, bali hakufai wewe na wananchi na taifa kwa ujumla, na bila shaka hata yeye hajifai na ndiyo maana hana anachoweza!