Lifahamu daraja refu zaidi duniani kuvuka bahari, Hong Kong-Zhuhai-Macau lililounganisha kilomita 55

Lifahamu daraja refu zaidi duniani kuvuka bahari, Hong Kong-Zhuhai-Macau lililounganisha kilomita 55

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,716
Reaction score
9,051
Madaraja marefu zaidi duniani yamebeba reli sehemu kubwa ikiwa nchi kavu na China ikiongoza. Uhalisia wa urefu wa daraja hili la Hong Kong kwa kipimo tulichonacho ni sawa na kuunganisha madaraja 80 ya Kigamboni ambalo lina urefu wa mita 680 ili upate kilomita 55.

Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macau lililofunguliwa mwaka 2018 ndio daraja refu zaidi lililokatisha maji linalobeba magari. Limeondoa safari ya masaa manne mpaka dakika 30 pekee. Wakati wa ujenzi wake, lilimeza dola bilioni 20 sawa na trilioni 46 kwa viwango vya thamani ya fedha ya sasa na limeundwa kudumu kwa miaka 120.

Umaarufu wake umeshereheshwa kwa kujumuisha kipande cha daraja kilichopita chini ya bahari, kipande kilichoshikiliwa na kamba na visiwa vinne vya kutengeneza majini. Kilomita 6.7 zinapita chini ya bahari baina ya visiwa viwili vya kutengeneza.

Ujenzi wake ulicheleweshwa na hatua za kiusalama ambapo si chini ya watu 18 walifariki wakati wa ujenzi wake huku mamia wakipata majeraha. Pia ujenzi wake unatajwa kuwa na athari hasi kimazingira hasa kwa bahari na viumbe vya majini.

Ili kupita kwenye daraja hili lazima kulipia.

Macau.jpg
 
Wanalipishwa hela kuvuka hilo daraja mkuu?
Sio magari yote yanaruhusiwa kupita hapo zaidi ya yale yenye vibali maalum (vinaambatana na fees), hii ni kwa sababu ya vikwazo ambavyo serikali ya Macao na HongKong wameweka kwa magari binafsi kutumia barabara (kuepusha misongamano)...

Kwa wale wasio na vibali, unakwea shuttles maalumu (mabasi) ya kucross kutoka sehemu moja kwenda nyingine...

Hili daraja linaunganisha territories 3 za Uchina ambayo ni mji wa Zhuai uliopo Guangdong, kisiwa cha HongKong na ile kisiwa/penisula ya Macao...

Infact hili dude lilijengwa kwa ajili ya wala bata tu kwenye hiyo miji mitatu, maana hiyo miji ni mizuri laana
 
Mi mpaka leo bado najiulizaga haya madaraja yanajengwa vp huko chini ya maji...yaani najiuliza sana
 
The world's longest bridge is the Danyang–Kunshan Grand Bridge in China, part of the Beijing-Shanghai High-Speed Railway. The bridge, which opened in June 2011, spans 102.4 miles (165 kilometers). Another part of that train line, the 70.8-mile (114-km) long Langfang–Qingxian viaduct, is the second longest bridge in the world.
Danyang–Kunshan Grand Bridge - Wikipedia
Daraja la Hong Kong-Zhuai mpaka Macau ni la 31 kwa urefu wa Madaraja Duniani labda sifa ni ya kubeba magari
 
Tatizo sio rasilimali serikali inaweza kuingia mkataba na mwekezaji binafsi likajengwa baadae kunakuwa na tozo kama daraja la Kigamboni.
.... mwekezaji binafsi ajenge daraja kuunganisha Dar na Zanzibar? Kwa dola bilioni 20? Zaidi ya utajiri wa Alhaji Aliko Dangote Africa's #1? Ili daladala za Kwa Limboa - Makunduchi zipite? Huo mzigo wa USD 20 bn/= (TZS 46 tr/=) unaelewa maana yake lakini?

Kwa ufupi huo mzigo ni sawa na SGR 7 (sema standard gauge railways saba); moja inatutoa kamasi hadi shughuli za vipaimara na kumcheza mwali zinapigwa kodi lakini wapi!
 
Sio magari yote yanaruhusiwa kupita hapo zaidi ya yale yenye vibali maalum (vinaambatana na fees), hii ni kwa sababu ya vikwazo ambavyo serikali ya Macao na HongKong wameweka kwa magari binafsi kutumia barabara (kuepusha misongamano)...

Kwa wale wasio na vibali, unakwea shuttles maalumu (mabasi) ya kucross kutoka sehemu moja kwenda nyingine...

Hili daraja linaunganisha territories 3 za Uchina ambayo ni mji wa Zhuai uliopo Guangdong, kisiwa cha HongKong na ile kisiwa/penisula ya Macao...

Infact hili dude lilijengwa kwa ajili ya wala bata tu kwenye hiyo miji mitatu, maana hiyo miji ni mizuri laana
Ama wenzetu wana pesa..yaani kutupa hela yote hiyo kwa ajili ya kupitisha watu wachache tu? Hasa iwata recover lini pesa iloyotumika?
 
.... mwekezaji binafsi ajenge daraja kuunganisha Dar na Zanzibar? Kwa dola bilioni 20? Zaidi ya utajiri wa Alhaji Aliko Dangote Africa's #1? Ili daladala za Kwa Limboa - Makunduchi zipite? Huo mzigo wa USD 20 bn/= (TZS 46 tr/=) unaelewa maana yake lakini?

Kwa ufupi huo mzigo ni sawa na SGR 7 (sema standard gauge railways saba); moja inatutoa kamasi hadi shughuli za vipaimara na kumcheza mwali zinapigwa kodi lakini wapi!
Kuna watu wana pesa zao zinahitaji matumizi ila wanaangalia wawekeze wapi lakini hiyo hesabu ya usd 20 bilioni sijui umeitoa wapi
 
Back
Top Bottom