Lifahamu daraja refu zaidi duniani kuvuka bahari, Hong Kong-Zhuhai-Macau lililounganisha kilomita 55

Lifahamu daraja refu zaidi duniani kuvuka bahari, Hong Kong-Zhuhai-Macau lililounganisha kilomita 55

Ama wenzetu wana pesa..yaani kutupa hela yote hiyo kwa ajili ya kupitisha watu wachache tu? Hasa iwata recover lini pesa iloyotumika?

Habari ya miaka mingi Dina heri ya mwaka mpya...

Upekee wa hilo daraja tu tayari ni kivutio cha utalii...

Plus, zamani kutoka HongKong kwenda ama Macao au Zhuhai ilikuwa ni lazima upande ferries sisi bongo tunaita pantoni ambapo ni takribani dk 40 kukatiza maji...Wakati kwa sasa kutumia daraja ni dk 15

Sasa hiyo miji mitatu ni moja ya miji ya kitalii na bata la kufa mtu (especially Macao), hivyo itarahisisha wepesi wa kutoka point A to B
 
Tatizo sio rasilimali serikali inaweza kuingia mkataba na mwekezaji binafsi likajengwa baadae kunakuwa na tozo kama daraja la Kigamboni.

Sahihi mkuu lakini pia kabla mwekezaji hajaweka fedha anaangalia uwezekano na muda wa fedha yake kurudi(ROI) kisha kutengeneza faida... Span ya kurejesha fedha iliyotumika kujenga daraja la Kigamboni sidhani kama hata ina dalili ya kumalizika na tetesi zinasema mifuko ya hifadhi hali zao si nzuri kifedha hivyo uwezekano wa kujihusisha na miradi mikubwa ni mdogo, kwa sekta binafsi kuweka fedha kwa umbali wa Zanzibar ni long shot hasa ukizingatia uwezo wa wasafiri kulipa.
 
The world's longest bridge is the Danyang–Kunshan Grand Bridge in China, part of the Beijing-Shanghai High-Speed Railway. The bridge, which opened in June 2011, spans 102.4 miles (165 kilometers). Another part of that train line, the 70.8-mile (114-km) long Langfang–Qingxian viaduct, is the second longest bridge in the world.
Danyang–Kunshan Grand Bridge - Wikipedia
Daraja la Hong Kong-Zhuai mpaka Macau ni la 31 kwa urefu wa Madaraja Duniani labda sifa ni ya kubeba magari

Kweli mkuu lakini kuvuka bahari hili ndio refu..
 
Sahihi mkuu lakini pia kabla mwekezaji hajaweka fedha anaangalia uwezekano na muda wa fedha yake kurudi(ROI) kisha kutengeneza faida... Span ya kurejesha fedha iliyotumika kujenga daraja la Kigamboni sidhani kama hata ina dalili ya kumalizika na tetesi zinasema mifuko ya hifadhi hali zao si nzuri kifedha hivyo uwezekano wa kujihusisha na miradi mikubwa ni mdogo, kwa sekta binafsi kuweka fedha kwa umbali wa Zanzibar ni long shot hasa ukizingatia uwezo wa wasafiri kulipa.
Ni kweli unavyosema, hakuna mwekezaji anayetoa pesa ya hisani lakini akiona itamrudishia kwa muda mfupi atawekeza ila kama itachukua muda mrefu kurudisha faida ni ngumu kuwekeza
 
Habari ya miaka mingi Dina heri ya mwaka mpya...

Upekee wa hilo daraja tu tayari ni kivutio cha utalii...

Plus, zamani kutoka HongKong kwenda ama Macao au Zhuhai ilikuwa ni lazima upande ferries sisi bongo tunaita pantoni ambapo ni takribani dk 40 kukatiza maji...Wakati kwa sasa kutumia daraja ni dk 15

Sasa hiyo miji mitatu ni moja ya miji ya kitalii na bata la kufa mtu (especially Macao), hivyo itarahisisha wepesi wa kutoka point A to B
Habari ni njema tu na heri kwako pia.
Kama ni kivutio basi si heri liachwe kutumika na kila mtu at a fee kuliko kuachia wachache? Au wachache hao fee wanalipa fee kubwa inayopelekea karibu na kutosheleza?
 
Madaraja marefu zaidi duniani yamebeba reli sehemu kubwa ikiwa nchi kavu na China ikiongoza. Uhalisia wa urefu wa daraja hili la Hong Kong kwa kipimo tulichonacho ni sawa na kuunganisha madaraja 80 ya Kigamboni ambalo lina urefu wa mita 680 ili upate kilomita 55.

Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macau lililofunguliwa mwaka 2018 ndio daraja refu zaidi lililokatisha maji linalobeba magari. Limeondoa safari ya masaa manne mpaka dakika 30 pekee. Wakati wa ujenzi wake, lilimeza dola bilioni 20 sawa na trilioni 46 kwa viwango vya thamani ya fedha ya sasa na limeundwa kudumu kwa miaka 120.

Umaarufu wake umeshereheshwa kwa kujumuisha kipande cha daraja kilichopita chini ya bahari, kipande kilichoshikiliwa na kamba na visiwa vinne vya kutengeneza majini. Kilomita 6.7 zinapita chini ya bahari baina ya visiwa viwili vya kutengeneza.

Ujenzi wake ulicheleweshwa na hatua za kiusalama ambapo si chini ya watu 18 walifariki wakati wa ujenzi wake huku mamia wakipata majeraha. Pia ujenzi wake unatajwa kuwa na athari hasi kimazingira hasa kwa bahari na viumbe vya majini.

Ili kupita kwenye daraja hili lazima kulipia.

View attachment 1688041
Uwe makini, hii mambo ya kutaja kilomita inaweza kutuponza tukataka kujenga refu zaidi ya hizo 55
 
Habari ni njema tu na heri kwako pia.
Kama ni kivutio basi si heri liachwe kutumika na kila mtu at a fee kuliko kuachia wachache? Au wachache hao fee wanalipa fee kubwa inayopelekea karibu na kutosheleza?
Hao wachache ni kwa wale waendeshao magari binafsi na hii yote ni katika kudhibiti wingi wa magari kwenye hii miji haswa HongKong...(kuepusha foleni)

Watu wengine hulazimika kukatiza kwa kupanda shuttles (mabasi maalumu), kwa kulipia nauli/tozo...
 
Back
Top Bottom