Uzi uendelee wadau,wale walio weza kulima waje na mrejesho tujifunze pamoja ili tuelimishane kwa undani na namna ya kukabiliana na changamoto zote zinazojitokeza.
Kuna kipengele cha muhimu sana hakijagusiwa na wadau, kwa asilimia kubwa,
1.Uangalizi kwenye hatua zote 4 za ukuaji
A.Ukuaji wa mwanzo kabisa -Establishment
B.Maendeleo ya ukuaji (Growth development)
C.Maua - Kutunga Matunda-Kuwa tayari kuvunwa (Flowering - Fruit set- maturity)
D.Mavuno(Harvesting)
2.Mahitaji na uwekaji wa Mbolea katika hatua zote 4
3.Muda sa hihi wa kuweka mbolea(idadi ya siku baada ya kupanda(Days After Transplanting)) na aina ya virutubisho vya mbolea vinavyohitajika na mmea huu kwa wanaopanda mashambani (N-Nitrogen,P-Phosphorus,K-Potassium,Ca-Calcium,Mg-Magnesium,S-Sulphur)
4.Magonjwa na dawa zake(viambata badaya ya majina ya dukani).
Kwa mwenye uelewa tunaomba ku share unachokijua.
Binafsi ni mkulima,na bandika hichi kidogo nlichofanikiwa kukijua katika harakati,
Ngogwe hizi tunazolima sisi kwa asilimia kubwa ni za group la "DB3" hasa hasa Gilo,
Zinahitaji udongo wenye rutuba nzuri ,mbolea za samadi na mboji (ng'ombe,mbuzi na kuku) ambazo zinakua na NPK(hapa hizi ndio Base dressing) ni sahihii sana pia mbolea za viwandani kwa namna moja ama ingine zinaweza hitajika sana hasa kwa wale wanaolima kwenye udongo wenye upungufu wa rutuba na watakao kosa samadi na mboji.
Ntaelezea mbolea hizi,
Ngombe na Mbuzi zinakaa muda mrefu shambani na kufanya udongo kua na rutuba kwa muda mrefu ukilinganisha na aina nyingine ya mbolea(hizi ziko katika mtindo (form) ya inogarnic Nitrogen na organic Nitrogen ambayo ipo kwenye mkojo na urea ambayo ipo kwenye mavi,hii huitaji kubadilika kua Nitrogen(N) alafu bacteria na enzymes watazibadili kwenye udongo ili iwe Nitrate NO3(mfumo ambao mmea utaichukua kwa haraka),kwa hiyo ni slow acting/release,ndo mana unashauriwa uweke week 2 ama zaidi kabla ya kuhamisha miche yako,
Mbolea ya kuku hii ina Nitrate tayari nyingi kwa hiyo ni nzuri kwa kipimo sa hihi kwa mahitaji ya haraka(fast release/acting) na haikai shambani muda ikishachukuliwa na mmea basi zoezi limeishia hapo,zingatia kwamba ukizidisha mbolea hii itaunguza mmea.
Note: Zao hili linaweza kuota bila kuweka chochote,hapa ina maanisha udongo ilipo ota umejitosheleza,
Hapa tunaongelea kwa wale wanaotaka kulima kibiashara wakilenga mazao mengi na ya uhakika.
Tuendelee
Mbolea za viwandani,
Mmea wa nyanya chungu(ngogwe) huhitaji mbolea ya Nitrojeni na Phosphorus kwa kukua vizuri na imara na Pottasium kwa matunda (Nitrogen inaleta makuzi,majani,shina na kusaidia photosynthesis-upumuaji,lakini isiwekwe kwa wingi sana, nitrojeni ikiwa nyingi na ikiwekwa mara kwa mara huleta majani mengi na kufanya mmea kua na msitu,hii hupunguza mazao sana,pia mmea huhitaji phosporus kwa wingi katika hatua hizi za awali baada ya kuhamisha miche ili kuleta mizizi bora na mingi pia imara ambayo huwezesha mmea kuchukua chakula katika udongo ikiwemo hiyo nitrogen,pia husaidia kinga ya mmea kwa magonjwa,
Kwa hizi za viwandani inashauriwa kuweka mbolea pembeni ya mmea(side dressing) baada ya week 2(hapa mmea unakua umeshajishika chini vizuri na kuanza kutoa majani mengine mapya) weka mbolea shambani zenye uwiano sawa wa NPK isiyo ya kiwango cha juu mfano (10:10:10, 12:12:12) hata zenye kupungua kidogo na kuongezeka kidogo hazina tatizo mfano 11:14:10(kama zipo)
Utarudia mbolea wakati maua yana anza,utaweka mbolea zenye nitrojeni ya chini zaidi na Potassium ya juu kidogo mfano 5:10:20 etc,Calcium(CaO na Magnesium(MgO),zikiwa na O maanza yake ni oxides(kwamba zinayeyuka kwenye maji -soluble) zitahitajika,Calcium Nitrates(Ca(NO3)2) kama CAN ina Nitrogen 26-27%,Nitrabor,CALCINIT etc zenye N 13-15.5% na 25-27% CaO hizi nusu ya nitrogen ni ni slow release na nusu ni fast acting (kuna mbolea nzuri zenye michanganyiko inayofaa direct kama Minjingu Pamba(white diamond hii ina N,P,K,S,Mg,CaO),kuna Mbolea za kampuni OCP,Kuna mbolea za Yara(Nitrabor) hii ina 15.4 N(nusu N na nusu NO3-inayochukuliwa haraka na mmea) pia ina Boron kidogo,na aina zingine zenye majina tofauti tofauti. Tafadhali zingatia mbolea ina virutubisho(nutrients) gani na sio jina tuu ili mradi,
Utaendelea na mbolea za maji (Foliar) zenye Potassium kubwa(K 35-60%) kila baada ya siku 10-14 kama Multi K,Master Fruiter etc,alafu utarudia tena mbole za punje,NPK(Nitrogen ya wastani,phosporus ya chini kabisa na potassium ya juu zaid ya zote)kila baada ya siku 21-30
Utazingatia muonekano wa mmea kwa macho ili uweke mbolea sa hihi na kiwango sa hii hii,utakua pia unapiga mbolea za maji za kwenye majani(foliar),wakati huu phosporus haihitajiki kwa wingi kwa kua mizizi ishajishika vizuri katika hatua ya awali.
Kuna booster nyingi na nzuri,zenye virutubisho vingi vikuu(NPK),vya kati(Ca,Mg,S) na vya chini(Fe,Mn,Cu,Zn,B,Mo),pendelea zile zenye virutubisho vya kawaida na vya ziada pamoja,kuna zingine zina pendelewa sana lakini zinaivisha matunda haraka(mfano Vigmax) iwekwe mwanzoni wakati wa maua na sio wakati wa mavuno,kuna mbolea kama Max Green na zingine zipo vizuri(tukichambua zina virutubisho gani tutampoteza kabisa mkulima).
Mbolea za chenga chenga hizo nlizotaja (NPK,CaO,MgO,S) ni muhimu sana,alafu unaweza endelea na mbolea za juu za majani(hizi zote zinafanya kazi haraka sana kwa maana ya matokeo yake),zingatia maelezo ya kila mbolea kwenye vibandiko vyake.
Napokea maswali kwa hapa nlipo elezea,maswali yaliyoshiba na yenye uelewa ndani yake,sio maswali yasio na kichwa wala mguu i.e mtu anataka lima eneo flani,mkoa flani labda anauliza soko,soko kafanye research mwenyewe mazingira unayoweza yafikia.
NB:TUSIKARIRI,TUELEWE (ni nini na kwa nini)
Kwa wale wavivu wa kuuliza unaweza toa kiasi gani kwa ekari wakati hajui tofauti ya ekari na hekta wasituchoshe (~2.5 ekari ndo 1 hekta),4047m² ni ekari ama kibongo bongo 70mx70m - 4900m²,hii ntaijibu kwa mfumo unao eleweka.
Kwa upandaji wa 60cm mche hadi mche na 100cm kwa mstari hadi mstari maana yake kwa ekari moja ya 4900m² utakua na miche ~8,150-8,200
kwa mbegu hizi za kawaida za mashamba ya nje (OPV) na aina ya "DB3" unaweza toa kwa wastani wa mavuno yote kwa msimu usio pungua ukubwa wa eneo kwa square meter x 0.01,mfano eneo lako ni robo ekari,tuseme 1000m² - 1250m² utazidisha kwa 0.01 upate debe 10-12.5 wastani wa mavuno yako yoote kwa msimu wako,
Mwanzo wa mavuno utaweza kutoa debe 60 kila mchumo(itapanda mpaka debe 75 na kushuka mpaka 30 kutokana na mazingira,uangalizi,usimamizi na ulishaji wa virutubisho,wadudu na magonjwa).
Natanguliza heshima za dhati kwa mwenye uzi huu
Kubota ,hizi elimu zinasaidia sana kama upako vile,tusichoke kuwa ng'amua watakao kua tayari na wenye uelewa.
Nawasilisha