Lifahamu zao la Macadamia (Karanga Pori) na jinsi ya kulilima

Lifahamu zao la Macadamia (Karanga Pori) na jinsi ya kulilima

Wadau,

Kuna fursa kubwa kwenye kilimo cha matunda especially kwa nchi yetu ambayo ina ardhi nzuri na ambayo inafaa kwa mazao mengi.

Zao la Macadamia ni miongoni mwa mazao ya muda mrefu ambalo linaweza kubadirisha kilimo cha Tanzania, kwa sasa kuna mtaalamu ambaye ana kitalu cha miche ya macadamia (mche mmoja unauzwa shs 2,000) macadamia inaweza kustawi vizuri kwenye sehemu za baridi lakini siyo baridi sana hivyo kilolo, ifakara, morogoro, arusha, lushoto inaweza kustawi kwa uzuri zaidi.
Mimi nimechukua miche michache kwa ajiri ya kujaribu kwenye maeneo ya kisarawe.

Ni PM kama unataka maelezo zaidi au google

Unaweza pia kupata taarifa zaidi hapa: http://www.agroforestry.net/scps/Macadamia_specialty_crop.pdf
haya madude ni matamsana, sikuyajua jina, ukitupia mdomoni, utahisi umechota unga wa nido na kutupia mdomoni. shida yake ni kubangua,,, utaenda azima nyundo ya wajenzi
 
WanaJF naomba mwenye uelewa wowote wa kilimo ch Macadamia anijuze. Najua kuwa ni zao ambalo bei yake ni nzuri kutosha. Mara ya mwisho nilizungumza na dada mmoja akaniambia kuwa kule Lushoto kuna watu wanalima hilo zao. hakuweza kunipa taarifa kwa kina cha kutosha.

Zao hili lipo Tanzania? Hali gani ya ardi inahitajika? Najua Kenya wanafanya export ya zaidi ya USD120m kwa mwaka.
maeneo ya wilaya ya tukuyu, hasa kiwira hapo yanapatikana sana na kuna kampuni inanunua kwa ajili ya export.
 
Hizo Arusha zipo tunaita njugu mawe,
Wala sijawahi kuona umuhimu wake.
Ila ni tamu sana.
 
Anaejua link ya namna ya kuziuza nje jamani atusaidie tusije kuishia kupga adisi za utotoni...

Agro Business Iringa
 
Anaejua link ya namna ya kuziuza nje jamani atusaidie tusije kuishia kupga adisi za utotoni...

Agro Business Iringa
Mkuu kama una Macadamia basi tuwasiliane.

Soko lipo ndugu yangu.
 
Arusha vinaitwa "Vinazi"

Ndani ni kama nazi kabisa ila shughuli ni kukipasua...kigumu haswa.
 
Hi wadau, nikipata miche iliyofanyiwa grafting nitawaambia ilipo ili mkafuate wenyewe.
 
Nimekumbuka mbali sana zaidi ya miaka 20 nyuma kutoka sasa tulikuwa tunaita miti ya vinazi
ukitaka kuvichuma adi upande kwenye mti wake majani yake yana washa washa na yana vimiba pia kukipasua kana ukakasi kiasi vilikuwa vinalimwa
na tasisi tu siyo watu binafisi pia huwezi panda alafu ukachanganya na mazao mengine miti yake huwa mikubwa kiasi pia hutoa matunda yake kwa msimu nadhani mwaka mara moja!!!
nijuwavyo linastawi vizuri sehemu kahawa inapo stawi pia kama lina dhamani ni kwa sasa maana siku za nyuma lingeoteshwa kama lingekuwa na dhamani kushinda kahawa!!!
 
Hatimaye nimempata mhusika wa hii kitu, hawa jamaa wana miche kule Mbozi, kila mche ni Tsh 4,000/, miche hii ni grafted na inatazamiwa kuzaa baada ya miaka minne tangu kuoteshwa. Wao wanachukua vikonyo kule Rungwe juu kwa yule jamaa wa parachichi.
Simu kanipa, ila ukitaka njoo pm, si vizuri kuweka public.
 
26230607_10208920259998251_7221657076897096321_n.jpg


Salam za mwaka mpya.
Kama ilivyo kwenye korosho kule Mtwara, basi kwa wale wahenga wenzangu wa Tukuyu mtakuwa mnajua zile karanga za mitini kwa watu wa mjini na sehemu zinginezo wanaweza kudhani nadanganya, lakini la hasha ni kweli kuna karanga humea mitini na ni miti mikubwa kabisa, kwa kinyakyusa zinaitwa (Macadamia). Hizi zina vinasaba vya korosho kwa mbali, ni very delicious and healthy vilevile.

Wakati bei ya korosho ikipanda mpaka kufikia elfu nne kwa kilo kule Nangwanda Sijaona kunako Mtwara, watani wetu wa jadi hapo Kenya wameamua kuchana na mashamba ya chai na kukazania kilimo cha karanga za mtini ambazo zimefikia kilo moja Tshs 21,000.00 nakuendelea.

Hapa nchini sijui kama kuna sehemu nyingine zaidi ya Tukuyu ambako macadamia zinalimwa na baadhi ya sehemu mkoa wa Mbeya, nimewahi kuziona Mbozi pia.

Hizi karanga kama ukiweza kuzi process unaweza kuziuza kilo moja kwa $40 yes ndio hivyo, utajiri unachezewa.

Our research institutes zinaweza kulifanyia kazi hili zao ili tuweza kujua kama tunaweza kuli scale na kulifanya la kibiashara zaidi, hapo zamani sie wakulima tulikuwa tunalitumia kucheza michezo yetu ya kitoto, nakumbuka tukiwa watoto tulikuwa tukizinunua na kuzichezea then tunakula baadae sana, wazee wetu wanahangaika sana na chai labda hili zao linaweza kuwa mwarobaini wa ugumu wa zao la chai.

2018 mwaka wa mabadiliko, karanga za mtini zaweza kuwa mbadala muafaka kabisa wa chanzo cha mapato yetu. Rais wa benki ya maendeleo ya Africa kaamua kulivalia njuga swala kilimo ni muhimu kwenda hii vision ya Afrika pamoja, alinukuliwa akisema asilimia 80% ya mabilionea hapo baadae watakaokuwa wakitokea Afrika watakuwa wanajishughulisha na kilimo, Yes inawezakana Inaanza na wewe na mimi.

Happy new year ndugu zanguni, muwe na mwaka wenye baraka tele.
 
Back
Top Bottom