ASANTE,
Marekebisho kidogo, Macadamia zinalimwa sehemu nyingi sana Tanzania, sehemu nyingine ni Arusha, Moshi na Tanga, lakini baba lao ni Sahare Mission Tanga. Pale lipo shamba lililoanzishwa na RC, Benedictine Fathers mwaka 1945 kabla ya Uhuru.
Kiwanda cha kubangulia zao hili cha kwanza kilikuwa Ndanda Mission kule Lindi kikipotea mzigo toka Sahare Mission Tanga. Kiwanda kingine kipo Rungwe kwenye shamba la Parachichi la Rungwe avocado pale juu ya Rungwe secondary ukishapita Moravian head Quarter.
Tatizo la macadamia ni ukuaji wake, growthrate ni ndogo sana, ila ukitumia grafted muda ni mfupi, changamoto ni kupata miche hiyo ya muda mfupi, bei ni kubwa kwa scale kubwa, bei ya jamaa wale wa Mbozi wenye kitalu ni Tsh 4000/ kwa mche. Kama unanunua mzigo mkubwa wanakuletea mpaka shambani kama uko pande za nyanda za juu kusini.