Lifanyike tambiko kuondoa mikosi inayoliandama taifa letu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Mababu zetu walikuwa wanajali sana masuala ya muhimu hasa linapokuja suala la kuondoa majanga katika jamii.

Ilikuwa ikikosekana mvua na dalili za ukame kuwepo mababu zetu walifanya makafara na mizimu iliweza kulinda taifa letu.

Sasa hivi kuna balaa la ajali limeandama taifa letu. Hapa panahitajika kafara la kuondoa mikosi ya ajali. Tufanye hima watalaamu watafutwe na kafara la kuondoa mikosi lifanyike.

Nawasilisha.
 
Matambiko ni Ujinga kama ulivyoujinga wa kudhani nchi inamikosi.

Ulaya,China,us,Singapore, Namibia,Malaysia hawakunya tambiko ili watoboe kimaisha.

Tatizo letu ni Ujinga tu
 
Una uhakika na ulicho kisema ? Unaijua china,Malaysia na Singapore vizuri wewe?
 
Suluhu siyo tambiko. Suluhu ni kuboresha miundo mbinu yetu mfano: ata barabara za mikoani zafaa kufungwa mataa. Tanua barabara zenye umuhimu, njoo na sera bora za kutumia barabara.
 
Naunga mkono hoja kwa 100%. Wenye akili fupi watabeza sana hoja hii. Ukweli ni kwamba, kwa sasa Nchi yetu inapita katika wingu jeusi la BALAA.
Kama miezi miwili/mitatu iliyopita kulikuwa na Wimbi la watu kuuana kiholela holela, tena akiulizwa muuaji anakwambia "mimi nilinyimwa pombe kilabuni nk." ambazo ni sababu za kijinga kabisa.
Kwa sasa kuna Wimbi la AJALI. Kwa sasa haziwezi kupita siku 3 hujasikia ajali. Ukipita barabarani humo huwezi kukosa japo magari kadhaa yaliyopinduka au kugongana.

Watu ufinyu wa ufahamu wanadhani kutambika ni ushamba, kumbe wao ndo washamba.
Ukitaka kuamini nenda CHINA, INDIA, JAPAN,KOREA NK. Huko ndiko kwenye visima vya matambiko.

Na naomba kudhauri, kama tumemsema vibaya JPM eti tu kwa sababu hayupo, hakika tumelaaniwa au tutalaaniwa kwani mimi naamini kwamba JPM hakuwa mtu wa kawaida sana, alikuwa kama NABII aliyeshuka kutoka juu kwa wakati wake na mahala pake.
Nakumbuka ile mwaka jana baadhi ya watu walimdhihaki sana JPM. Mara tukakuta mvua hazinyeshi wakati msimu wake umefika.
Nadhani wenye akili waligundua hilo, walipoacha kumdhihaki iwe kwa kulazimishwa au kwa hiari, mvua zilianza kunyesha ingawa ni kwa kuchelewa kidogo.
Kwa hiyo, kufanya toba kwa pale tulipokosea si dhambi hata kidogo.
 
Mababu zetu walikuwa wanajali sana masuala ya muhimu hasa linapokuja suala la kuondoa majanga katika jamii.

Ilikuwa ikikosekana mvua na dalili za ukame kuwepo mababu zetu walifanya makafara na mizimu iliweza kulinda taifa letu.

Sasa hivi kuna balaa la ajali limeandama taifa letu. Hapa panahitajika kafara la kuondoa mikosi ya ajali. Tufanye hima watalaamu watafutwe na kafara la kuondoa mikosi lifanyike.

Nawasilisha.
Mikosi na matatizo yanayokabili taifa hili ni matokeo ya matambiko mbalimbali ambayo nchi imefanya na kumwaga damu nyingi kwenye makafara.
Mwenge pia ni tambiko baya sana.

Nchi haiwezi kuendelea kwa kutegemea matambiko
 
Mababu zetu walikuwa wanajali sana masuala ya muhimu hasa linapokuja suala la kuondoa majanga katika jamii.

Ilikuwa ikikosekana mvua na dalili za ukame kuwepo mababu zetu walifanya makafara na mizimu iliweza kulinda taifa letu.

Sasa hivi kuna balaa la ajali limeandama taifa letu. Hapa panahitajika kafara la kuondoa mikosi ya ajali. Tufanye hima watalaamu watafutwe na kafara la kuondoa mikosi lifanyike.

Nawasilisha.
Mshana Jr awe consultant
 
Tatizo kuna genge mpaka leo wanashangilia kifo cha Dkt Magufuli. Kumbuka kiroho Dkt Magufuli alikuwa ni kiongozi.
 
Matambiko ni Ujinga kama ulivyoujinga wa kudhani nchi inamikosi.

Ulaya,China,us,Singapore, Namibia,Malaysia hawakunya tambiko ili watoboe kimaisha.

Tatizo letu ni Ujinga tu
Waafrika bhana!!

China mpaka leo ni among of the greatest county in the world kwasababu hawakukubali tamaduni zao kuharibiwa na watu wa magharibi.

China wanafanya vitu vyao from their own na hawa imitate tamaduni za popote pale.

Tatizo letu la Afrika linaanzia kwa viongozi mpaka raia.

Kiongozi Afrika ni Mungu mtu Lakini kiongozi kwengine ni mtoa huduma tu.

Ubinafsi,ujuaji na roho mbaya ndio tatizo letu..
 
Akili za kiafrika hizi..
Badala ya kutafuta suluhisho la kisayansi..
Je barabara zetu zina standard?
 
Mababu zetu walikuwa wanajali sana masuala ya muhimu hasa linapokuja suala la kuondoa majanga katika jamii.

Ilikuwa ikikosekana mvua na dalili za ukame kuwepo mababu zetu walifanya makafara na mizimu iliweza kulinda taifa letu.

Sasa hivi kuna balaa la ajali limeandama taifa letu. Hapa panahitajika kafara la kuondoa mikosi ya ajali. Tufanye hima watalaamu watafutwe na kafara la kuondoa mikosi lifanyike.

Nawasilisha.
Matambiko hayataondoa tatizo yatazidisha!! Hata hapa tulipofika ni kwa sababu ya matambiko!
 
Mikosi ipi hiyo hebu iweke hapa kwanza

Ova
 
Back
Top Bottom