Life Experience: Jambo gani liliwahi kukutia aibu katika maisha?

Yaani mpumbavu kweli.
 
Daaah umenikumbusha mbali sana mkuu, Nilitongozaga demu mtandaoni baada ya kumuona akiwa anapost picha mara kwa mara akila bata na alionekana mzuri balaa kama unavyowaona akina Beyonce vile, yaani ukiona picha yake utafikiri hajazaliwa ni kama malaika kashushwa vile nikamfuata Inbox baada ya kuzoeana sana nikamtongoza akakubali kwa vile nilikuwa mkoani kikazi na yeye alikuwa Dar, ikabidi tukakubaliana nimtumie nauli aje niliko akakubali nikamtumia.

Siku ya kuja Alifika muda kama saa8 unusu nikiwa bado niko kazini na kwa vile rafiki zangu nilishawaonesha picha za yule mdada na kwa kweli na wao wakaona nimeopoa lulu, ikabidi nimtume dereva na gari la ofisi akampokee ampeleke hoteli akale then nikamuelekeze pa kumuacha.... nikiwa nimetulia muda wote nachart nae nikaona text kutoka kwa dereva " mzee demu gani huyu umeleta, njoo umpeleke mwenyewe hotelini mimi siwezi kuongozana nae" nikajua jamaa anatania maana ni mtu wa utani..

Alivorudi akawa anacheka sana anawahadithia rafiki zangu nikiwemo nikajua anatania hasa nikirudi kuangalia zile picha hata rafiki zangu hawakuamini muda wa kazi ulipoisha marafiki zangu wakanifuata kwenda kumuona shemeji yao. Sitaki kuamini nilichokiona kule, picha ni zake kweli lakini sio uhalisia wake kabisa jamaa wakaniacha bhna hawakutaka hata kukaa na mimi halafu sijui ex wangu alijuaje niko pale si akaja aliongea maneno yaliyofanya ile siku ikawa mgumu sana kwangu.

Kesho yake nikampa nauli arudi, yule demu hata sikupiga aisee, nilipoingia ilikuwa ni kila mtu akawa ananidiscuss mimi kwa kilichotokea usiku wa jana yake.

Hawa madada msiwaamini kwa picha za mitandaoni, wakiwa nyuma ya camera za iphone ni tofauti na uhalisia wao.

Mtandaoni binafsi sitongozi tena
 

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Daah sawa mkuu ila pole
 
Alikuaje kwani mkuu
 
Pole sana mkuu
 
Inasikitisha japo inachekesha[emoji1] [emoji1]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mm 2007 nilikuwa naenda Advance Songea, basi nikatoka kusini hadi dar, Dar nikapanda basi la superfeo kwenda songea, lile basi ilikuwa wakigawa soda ila mukifika maeneo ya Iringa na kwenda mbele, ila mm sikuwa nimewahi kupanda basi ambalo wanagawa soda, sasa ile tunafika mikumi naona njaa kwa mbaaaaali inaninyemelea ile nikipepesa macho nikaona kreti la soda kwa katikati, nikasema isiwe shida sasa kucheki vema siti za jirani zina mabinti wawili wamevalia yunifomu za songea girls basi nikashoboka na kumuuliza mmoja eti dada zile soda kwenye kreti nani anauza?

Yule dada akaniambia haziuzwi mbona watagawa bure tu baadae!!!!! Haki ya mungu niliona fedheha vibaya mno na safari ikawa chungu saanaa hadi tunafika songea mida ya saa mbili na nusu usiku,

Na tangu hapo sikutongoza mwanafunzi wa songea girls Hadi namaliza form six na kurudi zangu kusini,

Pumbavu kabisaaaaaa fedheha ile...
 
Hahaha hahaha jamani nimecheka vibaya sana.
 
Daaahhhhhhhh mkuuu hiii Kali saaaaaana
 
Dah kuna siku gari ya mshua ilikodiwa kwenda Njombe... Ilibeba wanakwaya wanaenda kwenye harusi ya mwenzao. Sasa kufika kule wakawa kanisani wanasherehekea...mimi nipk ndani ya gari nimelala daaaaaaaaaaah!!!! NILIJAAMBAAA KWANGUVU KAMA MARA 3 AFU KWA UHURU NIKIJUA NIPO PEKEANGU NDANI.... baada ya dakika mbili hivi nikashituka kuangalia hivi kuna mmama kakaa pembeni daaaaaaaah!!!!!!
 
Nawazaaa mimi[emoji87] [emoji87] [emoji87]
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] we jamaa asee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…