Daaah umenikumbusha mbali sana mkuu, Nilitongozaga demu mtandaoni baada ya kumuona akiwa anapost picha mara kwa mara akila bata na alionekana mzuri balaa kama unavowaona akina Beyonce vile, yaani ukiona picha yake utafikiri hajazaliwa ni kama malaika kashushwa vile nikamfuata Inbox baada ya kuzoeana sana nikamtongoza akakubali kwa vile nilikuwa mkoani kikazi na yeye alikuwa Dar, ikabidi tukakubaliana nimtumie nauli aje niliko akakubali nikamtumia, siku ya kuja Alifika mda kama saa8 unusu nikiwa bado niko kazini na kwa vile rafiki zangu nilishawaonesha picha za yule mdada na kwa kweli na wao wakaona nimeopoa lulu, ikabidi nimtume dereva na gari la ofisi akampokee ampeleke hoteli akale then nikamuelekeze pa kumuacha.... nikiwa nimetulia mda wote nachart nae nikaona text kutoka kwa dereva " mzee demu gani huyu umeleta, njoo umpeleke mwenyewe hotelini mimi siwezi kuongozana nae" nikajua jamaa anatania maana ni mtu wa utani .. alivorudi akawa anacheka sana anawahadithia rafiki zangu nikiwemo nikajua anatania hasa nikirudi kuangalia zile picha hata rafiki zangu hawakuamini mda wa kazi ulipoisha marafiki zangu wakanifuata kwenda kumuona shemeji yao.Sitaki kuamini nilichokiona kule, picha ni zake kweli lakini sio uhalisia wake kabisa jamaa wakaniacha bhna hawakutaka hata kukaa na mimi halafu sijui ex wangu alijuaje niko pale si akaja aliongea maneno yaliyofanya ile siku ikawa mgumu sana kwangu.
kesho yake nikampa nauli arudi yule demu hata sikupiga aisee, nilipoingia ilikuwa ni kila mtu akawa ananidiscuss mimi kwa kilichotokea usiku wa jana yake.
hawa madada msiwaamini kwa picha za mitandaoni, wakiwa nyuma ya camera za iphone ni tofauti na uhalisia wao.
mtandaoni binafsi sitongozi tena