Moja kwa moja niende katika mada.
Leo asubuhi kama kawaida yangu kuna mahali huwa naenda kunywa chai, ni mgahawa wa jamaa yangu mmoja wa karibu, nimekunywa chai, nilipomaliza nikaona kuna funguo juu ya meza, ambazo ninafahamu ni za jamaa yangu(Nimeshazitumia mara kadhaa kukatia kucha kwa maana zina nail cutter), nikatumia katika kukata kucha.
Nilipomaliza kukata kucha nilipigiwa simu, nikasogea pembeni kuzungumza na simu, nikazungumza na simu kwa muda mrefu, hivyo sikuona umuhimu wa kurudi pale tena maana nimemaliza kunywa chai, kumbe wakati huo nimesahau funguo zile nimeziweka mfukoni, nilipofika nyumbani nimeendelea na shughuli zangu bila kuelewa chochote wala kukumbuka, nimekuja kupigiwa simu na binti kuwa kumbe zile funguo zinahitajika, ndio nikakumbuka kujisachi najikuta na funguo kuwa ninazo mfukoni, na kumbe si za jamaa yangu, kumpigia simu anasema si zake kweli, ni za binti anayefanya kazi hapo mgahawani, ni kwamba zimefanana, tukio hili limeniachia fedheha na aibu kubwa maana moja kwa moja nimeonekana kama nilikuwa nina hila mbaya, na hakuna yoyote ninayeweza kumueleza akaniamini, imebaki kuniuma mwenyewe rohoni, maana ningehusishwa na wizi.
Katika maisha kuna mambo ambayo yanatukuta kwa bahati mbaya bila sisi kutarajia, hayo mambo huwa yanapelekea aibu na fedheha ambayo haistahili kwa kweli, na hata haielezeki kwa mtu kirahisi.
Kama na wewe una kisa chochote tupe hapa tupate funzo kidogo.
Kitambo flani nilikuwa na mpenzi mmoja matata sana na uzuri tulikaa mtaa mmoja ila yeye aliajiriwa shirika binafsi na ni karibu na ofisini kwangu.
Binti akawa na tabia akitoka kazini kwake anakuja kunipitia tunakwenda home na gari ya ofisi (serikalini) kwangu. Ambapo ilikuwa ni kawaida coz watu wengi walifanya hivyo hata kwa watoto wao washule pia witumia fursa hiyo kwa kupanda gari za hapo ofisini kurahisisha usafiri.
Mara chache sana Bosi alikuwa anapanda gari za Utawala coz yeye alikuwa na VX lake!! Na gari za utawala zilikuwa cruiser mkonge sita na zilikuwa zinabeba watumishi kwa idara. Idara yangu tulikuwa watatu so gari ilikuwa na nafasi kibao tu.
Kumbe katika hizo mara chache Boss akamuona binti wangu na akamuelewa ila pa kumpatia hana!! So, akawa anabanana nasi kwenye gari ya wasaka tonge na hataki kukaa siti ya mbele ambayo tulikuwa tunamuachia kwa heshima yake (sisi tukajua Boss anapenda sana gari ya idara yetu πππ kumbe ana yake)!
Kitendo cha kukaa siti za nyuma na wavuja jasho akafanikiwa kupata contact za binti wangu mrembo na akawa anaimbisha mi bila kujua! Bahati mbaya sana, binti akampa cha mbavu Boss kubwa!!
Bosi akajawa na hasira, akaona njia ya pili baada ya ile ya kwanza kufeli ili kumpata Binti ni kunidhalilisha mbele ya binti ili kunishushia status!
Siku hiyo sina hili wala lile, muda wa kutoka umefika nikasogea garini na mrembo wangu. Kuna staff mwenzangu akachelewa kuja garini dereva akawa anapiga honi asikie aje.
Dereva alipoona jamaa haji akaamua kushuka amfuate ofisini! Lilikuwa kosa kubwa sana!! Aliibuka Boss from nowhere akaanza kunitukana kwanini napiga honi nasumbua na pia si kazi yangu kufanya hivyo!!
Alinitukana sana japo nilijitahidi kumwelewesha kuwa dereva ndiyo kapiga honi hakunielewa! Na kesi zikawa zinahama, zinatoka kwenye honi zinakwenda ofisini zinarudi zinakwenda mtaani zinarudi zinakwenda kwenye umalaya zinarudi huuuuh!!
Dereva akimwambia ni mimi nilipiga honi mkuu, anahamisha kesi inakuja madai ya umalaya mradi matusi na dharau zimtoke!! Niliyakoga siku hiyo sitasahu kabisa!! Dereva akitaka kutoa gari anamwambia ondoa gari langu na wewe nikuonyeshe!!
Nilikaa kimya, nachezea nokia ya tochi zile toleo la kwanza kabisa!! Ilikuwa ndiyo simu hot kabisa kabisa wakati huo!!
Aliporidhika akaondoka zake, garini hakuna mtu aliongea mpaka tunashuka!! Staff zote walitoka nje kuona kunani huko parking!!
Baadae ndiyo Binti ananiambia inawezekana kaamua kufanya hivyo sababu anamtaka kimapenzi, na sms zake akanionyesha!! Pia baada ya kutukana sana akamtumia Binti msg "si ndiyo kibwana chako unachoringia, haya ana nini sasa"
Hii kesi hii kwangu haijaisha kabisa!! Kuna siku akajitusua nikafuma kabrasha analipa vibarua hela ndogo kuliko iliyopitishwa na bodi na kuna allowance alikuwa analipa kidogo kuliko iliyopitishwa kwenye bajeti na bodi kisha inayobaki anapiga!
Nikanyofoa karatasi piga kopi nikamchoma macho makavuu huku anaona!! Kidogo avuliwe ukuu wake kama si kuhonga sana na baada ya hapo nikatafuta ajira kwingine nikasepa!!
Ila bado nikikumbuka naona kama kanidhalilisha jana hivi!! Bado namuwinda, nilimuotea mwanae kwenye harakati flani hivi nikamtosa then nikamwambia kamsalimie baba yako!