Life is a journey.....nimemiss days of my childhood.

Mr the dragon

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2017
Posts
1,937
Reaction score
3,718
Guess what!!!!!!!!!!!!!!?

Nimemiss zile siku naamka asubuhi natoka nje naanza kukamua maziwa then mida ya saa mbili napata ugali mkubwa na maziwa yaliyopekechwa "masuke" kwa kisukuma.Kisha naelekea huko milimani kuchunga ng'ombe mpaka jioni ndio unarudisha mifugo nyumbani.

Huko malishoni Ni mwendo wa kuwinda sungura ukiwa na mbwa Kama ni kipindi Cha mvua.Au ndege aina ya "ndingwa" ukitumia rungu na manati.Usiombe ujisahau ng'ombe wakavamia shamba la mtu, baadae ukakutwa na mwenye shamba bakora utakazo chezea usiombe.

Namaanisha yale maisha ya kwenda shule siku mbili kwa wiki nyingine ni shambani na kuchunga.Shule iko umbali wa zaidi kilometre kumi lakini tunaenda kwa mguu.Kabla hujaenda shule unatafuta kiporo cha ugali na mgagani unakigonga then ndio unaenda shule.

Mliozaliwa Kariakoo and the likes I know you can't come across to imagine this kind of life.But we countrysiders we lived those kind of life on nothern Simiyu.

Kipindi hicho kila akifa mtu sisi tunaamini amerogwa, haiwezekani kufa bila kurogwa.Kiswahili tumekijua shuleni, sisi darasani ulikuwa mwendo wa "nyanoko, "lushindo loko".Sekondari huwa wanavalishwa madude ya "Swahili speakers",Lakini sisi tulivalishwa pembe la ng'ombe kwa "Sukuma speakers" sijui kosa letu ni nini wakati kilugha ndio tulikimudu vyema.

Maisha ya disko ikitokea kuna sehemu mtu kaoa au kaolewa.Nyimbo zinazopigwa hutamsikia Michael Jackson, P square au Juma nature.Ni mwendo wa ng'wana Kanundo,Saida Karoli,Budagala na Maringita.

It was very funny days I missed as a legend, though nisingependa mwanangu ayapitie.The rest is history
 
Mi nimekulia dar,,,nimemmiiss kule uswahilini kwetu mdundiko( ngoma ya wazaramo)ikipita tunakimbilia mpaka tunapotea

Kuna ngongoti na Mzee jangala,,acha tu

Nakumbuka michezo ya goroli na makidamakida😀 hapo hatufagii ndani wala hatuoshi vyombo mpaka mida ya mama kurudi ndo tunakimbizana kufanya

Namiss baba akilewa wote tunanunuliwa soda,😂
Namiss kombolela,,acha kabisa

Nimekumbuka mbalii
 
Mimi naungana na wewe kwenye kujifunza kiswahili shule. O leve darasa letu tulikuwa 48 na kati ya hao 46 walikuwa wasukuma, mwalibu wa biology alikuwa anatufundisha kwa kisukuma baazi ya terminology. Burudani sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…