Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
- Thread starter
-
- #741
Portion 10.
.... Tuliondoka kule alfajiri kabisa, kabla hata hakujapambazuka vizuri. Tulivyofika mjini, nilienda moja kwa moja ghetto kwangu. Nilijimwagia maji kisha nikachapa usingizi.
Nililala mpaka kwenye mida ya saa tisa au kumi kasoro. Nilikuta missed calls na msg za Mama Husna ila sikuhangaika kumjibu. Kati ya msg nilizokuta, kulikuwa pia na msg za demu mmoja hivi tulikuwa tunafanya kazi ofisi moja. Nilishawahi kutupia mistari kipindi fulani ila akachomoa, nikampotezea. Kwenye msg nilikuta ameandika "Mambo"
Nikamjibu, tukaanza chat chat pale. Nilivyoona chatting zimenoga, nikamwambia aje walau kupaona ninapoishi, akachomoa. Akasema amechoka na hajisikii kutoka. Kwavile nilishachoka kukaa ndani na usingizi pia ulikuwa umeisha, nikaamua kusogea mtaani kwake. Yeye alikuwa anakaa maeneo ya Mwananchi.
Hapakuwa mbali, hivyo chap tu nilikuwa pale. Sikuwahi kufika pale kwake kabla ya siku hiyo. So, ilikuwa mara ya kwanza. Nilishangaa kukuta yuko njema, ndani kunapendeza tofauti na kipato chake. Kulikuwaga na tetesi kwamba anatoka na boss wetu pale ofisini, japo yeye mwenyewe alikuwa anakataa. Na hata hiyo siku nikajaribu kumuuliza tena kuhusu ilo jambo, akakanusha. Wakati niko pale, alikuwa anajiachia tu. Kiufupi alikuwa huru. Binafsi kama kuna somo ambalo nafaulu sana, basi ni kujiongeza.
Nikaanza kupiga hesabu, namuweka vipi kwenye target zangu bila kumpa muda wa kujiandaa. Maana wakishaonaga unatengeneza mazingira ya kumla, wanaanzaga pozi hata kama na yeye anataka. Sasa Mimi muda wa kuvutana vutana kama wahindi huwa sina kabisa.
Nikamuuliza kilipo choo. Akanielekeza kuwa kipo kwa nje, nikaomba anioneshe. Akatangulia kusimama, nikafatia kwa nyuma yake. Sikusubiria aufikie mlango, nikawahi kumshika, nikapitisha mkono wa kulia kwa mbele yake kama namkumbatia tokea kwa nyuma, alaf mkono mwingine nikamshika kiuno.
Alijaribu kunizuia kidogo, ilo mwisho wa siku akanipa uhuru. Baada ya hapo jioni yetu ikawa nzuri kabisa, akanisahaulisha stress za jana yake. Niliendelea kukaa pale mpaka kwenye mida ya saa tatu usiku, maana kila nikiaga ananiambia niendelee kubakia. Ilivyofika mida hiyo akawa anataka nilale. Siwezagi kulala kwenye ghetto la mwanamke, hivyo nikamgomea kulala.
Tukiwa bado tunabishana bishana hapo, mtu akanyonga kitasa cha mlango kama anataka kufungua mlango kutokea kwa nje. Uzuri mlango ulikuwa umefungwa kwa ndani na taa zilikuwa zimezimwa, maana tokea giza linaingia hatukuwa tumeziwasha.
Nikamuuliza ni nani anayenyonga kitasa muda ule au kama anatarajia mgeni?. Akasema hatarajii mtu yeyote. Ikabidi niende kuchungulia dirishani, nakutana na Boss wetu amesimama mlangoni huku ameshika kiparcel mkononi. Ikabidi nimrudie demu kumuuliza, boss anafanya nini pale wakati amesema hawana uhusiano? Demu anakatoa utetezi wa kizembe "Mimi sitoki nae, ila anan'taka"
Mimi: "Anakutaka? Kapajuaje hapa? Na mbona amenyonga kitasa kama vile ni mwenyeji?"
Demu akabaki kimya.
Mimi: "Kama hutoki nae, acha nikafungue mlango"
Demu akawahi kunizuia. Nikawa nishajua kinachoendelea.
Boss aliendelea kugonga mlango ila kule ndani tukaendelea kukausha. Nina uhakika alihisi ndani kuna watu, maana kama alisikiliza kabla hajagonga mlango lazima atakuwa alisikia sauti zetu, lakini pia pale njee niliacha viatu vyangu.
Aliendelea kugonga huku anaita, lakini ndani kimya. Demu ananiambia hakuna kufungua mlango, ataondoka tu. Nikawa namuuliza "Vipi asipoondoka?". Demu kakomalia lazima ataondoka tu, maana kesho anatakiwa kuwahi kazini, wanasafari ya siku mbili. Ikabidi nimuulize amejuaje kama Boss kesho anasafiri? Inamaana mnawasiliana?.
Demu kimya. Boss aliendelea kukaa pale mpaka mida ya saa nane kasoro usiku, sasa sijui kwa mkewe aliaga anaenda wapi, maana ameoa.
Mida hiyo ya saa nane, tukamsikia anapiga mlango teke akaachia tusi alafu akafyonya. Nilipoenda kuchungulia dirishani, nikamuona anaishia zake huku kashika viatu vyangu mkononi. Vile viatu nikajua ofisini lazima vikaibue msala.
Ilibidi niondoke pale muda ule ule. Maana kwanza sikuwa najua kama Boss atarudi au la, lakini pia sikuwa na viatu ikabidi niondoke na ndala za yule demu, niwahi kujiandaa ghetto.
Nilivyofika home, nikalala kidogo. Muda wa kuamka ulivyofika, nikajifikiria sana kwenda kazini. Maana yule Boss jinsi alivyo mtata, panaweza tokea lolote kule. Nikaamua ngoja ni doji.
Niliomba udhuru tu kwamba nimeamka najisikia vibaya. Mara kwa mara nikawa namuuliza yule demu kama kuna jambo lolote kuhusu Mimi linaloendelea kule ofisini. Hapakuwa na lolote.
Kesho yake nikaendelea na ratiba zangu kama kawaida. Na hata siku boss alivyorudi nilikutana nae na tukaongea fresh tu. Kumbe Boss pamoja na kujua siku ile pale ndani palikuwa na mwanaume, ila hakujua ni nani. Na vile viatu akaviweka kwenye gari la ofisi, akawa anatembea navyo daily.
Kuna jamaa yangu mmoja ndio alivyoviona mule, akavitambua kuwa ni vyangu. Na kila akipiga hesabu, wiki hiyo yote hakumbuki kuniona nikiwa nimevivaa wakati nilikuwa navipenda sana. Ikabidi aje aniulize inakuwaje boss yuko na viatu vyangu?. Ikabidi nimueleze story nzima ilivyokuwa. Akanicheka sana, mwisho wa siku akanishauri tuviibe mule. Ila nikagoma, kwavile Boss hajashtukia chochote, niliona acha nivitoe kafara viatu ili maisha yaende kwa amani. Ila yule demu nae nikampotezea mazima.
***** ***** ***** ****** ***** ******
Mahusiano na Mama Husna yaliendelea, japo ile hamu au raha ya kuwa na yeye ni kama ilianza kupungua, hasa tokea yale matukio ya ile sherehe. Maana niliona kama vile sasa tumeanza kuburuzana. Lakini kwa upande wake yeye wala, ndio kwanza anazidi kujiachia. Kuna muda anaweza akaniona kwa mbali, utasikia anaita "Baba Husnaaaa" yani utafikiri huyo Husna ni mwanangu kweli. Nikimwambia sitaki aniite vile, ndio kwanza anazidisha. Nikawa namuacha tu.
Wik end moja mida ya jioni nikasema acha niende Sigara kuangalia kama kuna mashindano au mechi yoyote, maana nilipitisha kipindi kadhaa sijaenda. Nilikuta wanafanya mazoezi tu, hapakuwa na mechi hivyo nikaamua kurudi zangu ghetto.
Nikiwa nimekaribia kabisa na mitaa ya home, nikapishana na pisi moja sio matata sana, lakini ilitosha kunifanya nipunguze mwendo. Sikusubiria anipite alafu ndio nigeuke nyuma, nikaamua kumsimamisha kabla hajanipita. Akawa ananijibu huku anaendelea kutembea, ikabidi na Mimi nianze kutembea uelekeo wake. Kwavile alionekana ana haraka sana, nikaomba namba kisha nikamuacha aendelee na safari yake.
Nikaanza kumtumia msg kabla hata sijafika ghetto. Tukawa tunachat chat.
Mawasiliano kati yetu yaliendelea kwa takribani wiki moja hivi, na ndani ya hiyo wiki alikuwa tayari ashakuwa mwenyeji ghetto kwangu. Maana ilikuwa kila nikirudi kutoka job, lazima mida ya saa moja moja aje, alafu kwenye saa tatu au mbili anaondoka. Na kuingia kwake ghetto, ilikuwa lazima nichore ramani na kuset mazingira fresh, kisha ndio aje. Ila pamoja na jitihada zote hizo, ila kumbe kuna wadau waliushtukia mchezo, ila wakakausha.
Tulidumu kama wiki na siku mbili au tatu hivi, alafu akapotea ghafla pale mtaani. Hata kwenye simu sikuwa nampata kabisa. Niliendelea kumtafuta, lakini bado hakuwa hewani. Nikampotezea.
Hazikupita hata siku nyingi, yani kwa ufupi ndani ya ile ile wiki ambayo yule manzi alitoweka, nikapata ugeni pale ghetto. Nilikuwa nimekaa zangu nje nafua, akaja jamaa mmoja ambae namfahamu ni boda boda, akiwa kaongozana na wazee wawili na mmama mmoja. Alivyowafikisha kwangu akaniambia "Broh, wageni wako hawa" Kisha akawaaga wale wageni wangu, akaondoka.
Sikuwa nawafahamu, hivyo nikabaki nawashangaa tu. Mzee mmoja kati ya wale wawili akaniuliza "Samahani kijana, wewe ndio fulani?". Nikamjibu "Ndio"
Mzee: "Unamfahamu fulani (akataja jina la yule manzi)"
Moyo ukalia Pa!. Nikataka nimkatae, ila akili ikaniambia mpaka wamekuja moja kwa moja kwangu, lazima watakuwa wanajua.
Analyse: "Ndio namfahamu"
Mzee: "Tunahitaji kuzungumza nawe juu yake"
Ikabidi niwape ndoo wakalie ili tuongee. Ndio kuniambia sasa hayo mazungumzo yenyewe. Kumbe yule manzi, kuna muda akili yake huwa inaruka, yani anakuwa kama kichaa kabisa. Na kwa wakati huo (ule muda ambao alikuwa kimya) kumbe akili yake ilishapoteana. Sasa kilichofanya wale wazee wanifate, ni kwasababu yule manzi amekutwa ni mjamzito, na kwenye simu wamekuta mawasiliano yangu Mimi na appointment zetu zote, hivyo wanaamini mimba ni yangu.
Ikabidi kwanza nikubali kuwa nilikuwa na mahusiano nae, lakini pia ilinilazimu nijitetee kuwa hakuna siku ambayo sikuwahi kutumia kinga alafu pia mahusiano yetu hayajazidi wiki hivyo hiyo mimba sio yangu. Yule mmama alionekana kuamini maneno yangu, lakini wale wazee walionekana kukaza. Na inavyoonekana vijana wengi pale mtaani wanamjua yule manzi na hali yake, hivyo huwa akili zikimruka, vijana wanaichukulia kama fursa ya kulala nae. Kwahiyo wale wazee walidhani Mimi pia nililala nae kipindi akili zimemruka.
Ilibidi nijitetee sana kuwa wakati nipo nae alikuwa timamu kabisa na ndio maana appointment zetu zote zilifanyika kwa simu. Tulibishana sana pale ila mwisho wa siku ikabidi waondoke tu, lakini wale wazee wakasema watanionesha.
Nikajuta kuvamia mademu mitaa ya watu bila hata kuuliza wenyeji. Hata hamu ya kufua ilikata, walivyoondoka na Mimi nikaingiza nguo ndani. Kitu kingine kilichofanya nisitishe zoezi la kufua, ni kitendo cha majirani kuninyooshea vidole pindi wakiongea. Nikaanza kuhisi pengine walisikia mazungumzo yetu, kumbe hapana. Sio kwamba wameyasikia, bali walikuwa na taarifa zote kabla hata Mimi hazijanifikia.
Na kuonesha kuwa kitaa hakuna siri, zile taarifa zilipepea zikafika hadi kwa Mama Husna, nikashangaa ananipigia simu:
Mama Husna: "Nakuona kidume cha mbegu, shababi wa mjini. Nasikia unatia mimba hadi vichaa huko!"
Analyse: "Unaongelea nini wewe?"
Mama Husna: "Unapenda sana nyakwa wewe mtoto, utakuja kulala na majini unyonywe damu, shauri yako"
Ikabidi nimkatie simu, maana nilishaanza kupandwa na hasira. Lakini pamoja na kukata simu, lilifatia lundo la msg za matusi na kejeli hadi nikajuta kwanini nilifahamiana nae.
Nikikumbuka matukio ya kwenye sherehe na nikaongezea na haya matusi, nikaona hapa siwezi kuendelea nae huyu. Mdogo mdogo akaanza kunitoka.
Mida ya saa mbili usiku nikiwa nipo ghetto, nashangaa gari ya polisi imefika. Bila hata kujua kosa langu ni lipi, jamaa wakanibeba. Baadae ndio nikaja kujua kuwa wale wazee ndio wameniitia polisi. Miongoni mwa askari niliowakuta ndani ya gari lao, mmoja wao nilikuwa namfahamu anaitwa Hoza. Nilisoma nae advance, ila nilimuacha darasa moja. Kipindi Mimi nipo kidato cha sita, yeye alikuwa cha tano.
Alikuwa ni mwanangu, japo sio kivile. Nilishawahi kufanya nae dili kadhaa. Nakumbuka kuna kipindi pale shuleni waliweka utaratibu kwamba mtu ukiumwa siku za wik end, unajitibia kwa gharama zako alafu jumatatu unapeleka lisiti ili urudishiwe gharama zako. Sasa kuna lisiti za dispensary fulani nilikuwaga nazo. Nikampa Hoza zile lisiti, wakawa wanajaza na kuzisign alafu wanaenda kudai hela shule as if wik end walikuwa wanaumwa. Mimi alikuwa ananipa commission yangu tu kwa kila lisiti waliyokuwa wanalipwa. Japo baadae walikuja kushtukiwa, ila wali-enjoy kwa kipindi kirefu.
Sasa huyu Hoza baada ya kumaliza shule, alijiunga na polisi. Leo hii ndio kaja kunikamata Mimi. Nilipomuona nilitoa tabasamu la ushindi kwa kumuona mwanangu, ila cha ajabu jamaa alinikataa. Hapo ndio nilisema siwezi kuwa na urafiki na askari hata awe ndugu yangu. Jamaa aliniletea ukauzu sana, akawa anataka hela ndio anisaidie. Nilipombembeleza sana, akajitoa kwenye ule msala. Akawaachia wenzake ndio wanikamue hela. Mwisho wa siku hela ikanitoka.
Baada ya kuwa nimewapa hela, Hoza akaanza kunichangamkia na kukumbushia baadhi ya matukio kipindi tuko shule. Tukabadilishana namba, ila moyoni mwangu nilijua kuwa sitoweza kumtafuta. Kiufupi nilimuona kama snitch tu.
***** ****** ******* ******
Mama Husna nae alizidi kunikalia kooni, kiasi kwamba mzuka nae ukapungua. Nikaanza kumpotezea. Nikapunguza ratiba za kuonana na yeye. Nikawa sionani nae tena katikati ya wiki, ikabakia wik end tu ndio tunaonana. Na hata hizo wik end ikawa sio zote.
Sasa kuna wik end moja ambayo nilikuwa kwake. Nilifika nikiwa kama mtu mwenye haraka, lengo nisikae sana. Ikabidi aniulize:
Mama Husna: "Hivi unajua sikuelewi siku hizi?"
Analyse: "Kivipi?"
Mama Husna: "Naona kama umeingiwa na kiburi, shida nini?"
Analyse: "Mawazo yako tu"
Mama Husna: "Ni mawazo yangu ndio, lakini yana sababu"
Analyse: "Achana na hizo habari bhana"
Mama Husna: "Acha kukwepa mada, kama umeshachoka haya mahusiano kuwa huru kila mtu ashike hamsini zake"
Analyse: "Wewe utakavyoona ni sawa"
Mama Husna: "Funguka mwanaume, acha kona kona"
Nikanyanyuka nilipokuwa nimekaa;
Analyse: "Mimi acha niende nikupunguzie kiwingu"
Mama Husna: "Nenda na husirudi tena hapa"
Analyse: "Hata hivyo Sina mpango wa kurudi tena"
Mama Husna: "Unasemaje wewe mtoto, ushamaliza haja zako unaenda kutafuta chaka jingine sio?".
Sikumjibu, nikawa naelekea mlangoni:
Mama Husna: "Sikia wewe mtoto, swala la kuachana na Mimi bado sana. Huwezi kuingia kwenye maisha yangu na kutoka kama unavyotaka, unadhani hii ni K ya majaribio eeh?
Sikutaka hata kujibizana nae, nikafungua mlango, nikatoka. Akaja hadi mlangoni, akaanza kunisindikiza na maneno:
Mama Husna: "Nenda kidume, ila nakuapia nitakachokufanya lazima utarudi tu. Na kwa taarifa yako mavuzi yako ninayo"
Moyo ukalia Pa!. Kasemaje? Japo nilisikia vizuri alichosema ila akili yangu ilijitahidi kutaka kupinga nilichosikia. Huyu Mama mavuzi yangu yeye ya nini sasa?. Na kwanini ameyatunza?. Mara zote alikuwa akishamaliza kunishave, anafuta na kitambaa na kuweka kila kitu kwenye ndoo. Sikuwa namfatilia ila niliamini alikuwa anaenda kumwaga chooni, ila akili ikaanza kuniambia pengine alikuwa anayatunza. Ili iweje sasa? Upande mmoja wa akili ikaniambia kuwa mikwara tu, lakini upande mwingine ukaniambia unamjua vizuri huyo mtu.
Mama Husna baada ya kuniambia kauli ile, alirudi ndani na kufunga mlango. Nikabaki najiuliza, niondoke au nirudi ndani?. Nikaamua kugeuka niangalie ulipo mlango wake. Ile nageuka, naona pazia za kwenye madirisha ya wale majirani zinafunga, shwaa, shwaa. Hii iliniashiria kulikuwa na watu wanachungulia/wanafatilia lile sakata.
Nikabaki nimesimama tu bila kujua nifanye nini...
** ** *****
Soma muendelezo hapa: Life style yangu ilinipotezea mwanamke mzuri