Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Wasaidie hawa ma bush lawyer... hii habari ni yakupikwa ukweli walikua watu saba tuu na wote wamevunjika miguu kama si dislocation ya mifupa yao maana mm ni miongoni mwa wakio saidia majeruhi
Uwii kuvunjika miguu tena[emoji848][emoji15]
 
Taarifa zinazotoka sio sahihi hata kidogo,waliokumbwa na kadhia hiyo ni watu saba tu,baada ya kuanguka mafundi walikuwa na waliifungua lift na waliotolewa ni 7 tu,na imeanza kuporomoka toka ghorofa ya 14.
Sipati picha viungo vyao[emoji848]
 
Ingetokea huku Mwanza kwetu mamaaaaaaa[emoji1787][emoji23] tungekomaje?? Mngetuita kila jina la kishamba!
Nawatakia uponaji wa haraka majeruhi!!!
Hahaaa nlitaka kusema hivyo ,kitu kikitokea dar dhana ya ushamba haiwezi kuongelewa
 
Pole sana kwa majeruhii, ni muhimu kufuata instruction manual kama imesema watu 10 basi ni hao,
Pia wenye jengo wasisahau kuwaita osha kwa ajili ya ukaguzi, lakini pia maintenance ya mara kwa mara ni muhimu
Nani unahisi atakuwa na jukumu la kuhesabu wenzake!? Hili nadhani Sio rahisi, Machine yenyewe ni rahisi kutambua uzito kuzidi na kutoa alarm ya kupungua watu, ila hapo ni uzembe, au lack of qualified technical personnel, au pia ni inferior quality ya lift machine,
 
Ndiyo maana kuna baadhi yetu, huamua kufanya mazoezi kwa kutumia ngazi badala ya lift.

Kuna haja ufanyike uchunguzi kuhusu uimara wa hiyo lift badala ya kutoa conclusion kuwa shida ni Kuzidi hao watu 3.

Huenda cable hazikuwa na uwezo au vinginevyo.
Lift nyingi uzito ukizidi haitembei. Kuna jambo linafichwa hapa si bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…