Lift ya Jengo la Millenium Towers yaanguka ikiwa na watu, kuzidisha idadi ya Watu kwatajwa kuwa chanzo

Dahha sijui ilikuwaje Kwa hao watu maana mwalimu wangu wa physics kipindi anatufundisha hayo mamba alisema cable ya lift ikikatika na kuanza ku fall down vichwa vya watu vinagusa paa la lift na migu inakuwa inalea elea tu
Mbona kama fizikia inakataa.

Kanuni za mwendo na inertia zinaelekeza hawa watu walikuwa wanasafiri kwa kasi moja na lift. Watapoteza uzito hawatasimama imara lakini hadi kufika kwenye paa I doubt.

Kwa sababu vitu vizito na vyepesi havina kasi ya kudondoka tofauti vyote vinavutwa kwa usawa 10ms2.

Tena tukichukulia na vitu kama ukubwa na ukinzani wa hewa, kunakuwa na uwezekano mkubwa hao watu wakadondoka chini kuliko 'kudondoka juu' unakokusema.
 
Daaah mimi naona shetani apumzishwe kila kitu shetani😂😂, unachepuka shetani, ukijikwaa kidogo shetani, mtu kajitupa shetani, ukifukuzwa KAZI KWA KUIBA shetani aseee awe tu na yeye anaenda kushtaki KWA MUNGU 🤣🤣🤣
🤣🤣
 
Kupatwa na hofu kwenye lift ni jambo la asili kabisa. Huwa tunajifunza baadaye kuacha kuogopa umbali.

Hofu za asili kwa wanadamu ni mbili tu; umbali mrefu (height) na kelele kali (noise). Hofu nyingine zoooooote tunajifunzaga.

Hapo mwili ulisoma ghafla 'Upo JUU NA UNA HATARI YA KUDONDOKA' ndo maana defence zikakick in fasta.
 
Ingetokea huku Mwanza kwetu mamaaaaaaa[emoji1787][emoji23] tungekomaje?? Mngetuita kila jina la kishamba!
Nawatakia uponaji wa haraka majeruhi!!!
 
Inatisha. Ushawahi kuota unaanguka ghorofani au sehemu ya juu. Au ushawahi kupanda tu lifti halafu iwe inashuka vile taratibu.
Zile ndoto zinakuwaga na lengo la kukuamsha. Kwa sababu akili inajua kabisa kwamba tukimuonesha anadondoka ni lazima tu atapata hofu na atashtuka (fear of heights)

Ni sawa na mtu vitani azimie atake kufakufa wanatoaga kisindano cha adrenalini weeeeeeeh ataaamka tena kwa morale.
 
Nakaziaa

Ova
 
imenishangaza hiyo design, eti watu 3 zaidi waliozidi ndio waangushe lift?
Kwenye Sructure analysis kila kitu kimekuwa considered, ndiyo maana kuna zile factor of safety ambazo zinasaidia mambo kama hayo yasitokee.

Labda wakati wa implementation kama iliandikwa cable wire ya 48mm wao wakaweka 30mm kuokoa gharama ndiyo hupelekea hizo disaster.

Nakumbuka hata lile jengo lililoanguka miaka ile Kariakoo design ilisema nondo za 16mm wakati wa Ujenzi wakaweka 10mm 🙌
 
Unakuta jengo ni refu sasa utapanda floor ngapi. Mfano umeenda pale mafuta house unaenda floor ya 19.
Ni kweli Mkuu, lift haziepukiki kwenye majengo marefu ila kwenye majengo ya ghorofa 5 bora kupanda kwa ngazi tu

All in all, wenzetu wanaohusika na quality and standards kwenye ujenzi wajitahidi kuhakikisha vinafikiwa pamoja na proper designs
 
Pole sana kwa wahanga, vp jengo oilijengwa na wachina au?
 
Inamaana likizidiwa uzito huwa linakubali ku operate?

Hapo kuna mawili either kuna sababu imefichwa ama elevator ilionesha indication ya kuzidiwa mzigo lakini sababu sie wabongo ni vichwa ngumu ndo ikawa hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…