Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Ule uvumi umetufundisha mambo mengi; lakini kubwa ni kuwa mashine ya kuchakatia uzushi ilichakata sana jana.. lakini leo imeshindwa kuendelea. Baada ya Rais wa Watu kutokea leo akiwa na afya njema na kufanya kitu ambacho watu walitakiwa kukidhania kingefanyika (baada ya kufanya uteuzi) basi ule uvumi ulitakiwa ubadilike na kunogeshwa namna hii...
Kwa mfano,
Huyu wa leo siyo Magufuli ni double wake. Si unajua kila Rais ana "double" wake yaani mtu anayefanana naye kwa kila namna. Na huyu double tunaweza kusema alienda akafanyiwa "plastic surgery" huko Cuba na amekuwa akitumika mara kwa mara...
Kwamba, baada ya kuugua alikimbizwa Afrika ya Kusini, ambako alipanda ndege ya mwendo kasi hadi Ujerumani alikofanyiwa matibabu, halafu akapandishwa ndege nyingine ya haraka na kurudi Ikulu Dar ambako alipokelewa kwa njia ya siri kupitia mlango ulioko baharini - akitokea meli ya nyambizi (submarine)..
Kwamba, tukio la leo kwa kweli halikuwa "live" ila lilirekodiwa kabla hajaugua na kuwa limeunganishwa vipande vipande kidigitally. Rais mwenyewe ameendelea mapumzikoni huko pembezoni mwa Milima ya Alps, Uswisi.
Yaani, ukishaamua kutunga uongo usiishie njiani, endelea nao hadi uonekane ni ujinga na watu wachukulie kama ni burudani fulani. Nje ya hapo jambo kubwa la kujifunza ni kuwa Rais Magufuli ule ulinzi labda hautoshi... kuna watu siyo tu wanaweza kuwa wanapanga mabaya, lakini wanayaombea, wanayasubiria, na kila waendapo kulala wanayaotea...
Ila ule uzushi ungenoga kama leo ungeendelea kidogo kuleta mantiki maana nilivyoona anashabikia sambusa na wasaidizi wake kama kuna kuumwa basi labda alipiga chafya tu kubwa watu wakashtuka na "kiwanda cha uvumi" kikaingia kazini.. Yaani, mtu hata kiungulia asipate.. na hakuna aliyefikiria hata ile connection ya suala la DPP uzito wake?
Sasa rais jamani hata chafya asipige. "Tuambiwe haraka alipiga chafya kubwa kiasi gani" , "Ni raisi wetu sote tunataka kujua kwa haraka... "
We unaonaje huu uvumi ungenoga noga vipi leo baada ya Jeuri ya Rais kuonekana leo..?