Mlendamboga
JF-Expert Member
- Sep 14, 2011
- 667
- 338
- Thread starter
-
- #261
Niombe wadau thread hii iendelezwe hata msimu ujao kwani Ligi Daraja la kwanza imekuwa haipewi nafasi kwenye media zetu licha ya kuwepo vipaji vingi na burudani nzuri huko.
Aidha ni ushauri kwa TFF kuweka usimamizi wa kutosha kwenye michezo hiyo ya ligi daraja la kwanza kwani kuna vimbwanga na vituko wakati mwingine kwenye maamuzi uwanjani!
Kwa msimu huu unaoishia nimeona mengi kwenye michezo hiyo katika viwanja mbalimbali ambapo kile kinachoitwa Uzalendo kimeonyesha kuvuka mipaka hadi kufikia wakati mwingine mchezaji anadaka mpira akiwa langoni (siyo kipa) halafu mwamzi anaingiwa kigugumizi anatoa mpira nje ya 18 ili kuwaokoa wenyeji wasinyeshewe.
Pia kuna list ya viwanja vyenye vimambo kikiwemo cha Mabatini, Uwanja wa karume waamuzi wanauogopa kishenzi kwakuwa macho ya TFF yapo pale pale!!!.
Leteni burudani tukuze vipaji vya vijana