Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

Ligi Daraja la Kwanza 2014/15, updates hapa

Niombe wadau thread hii iendelezwe hata msimu ujao kwani Ligi Daraja la kwanza imekuwa haipewi nafasi kwenye media zetu licha ya kuwepo vipaji vingi na burudani nzuri huko.

Aidha ni ushauri kwa TFF kuweka usimamizi wa kutosha kwenye michezo hiyo ya ligi daraja la kwanza kwani kuna vimbwanga na vituko wakati mwingine kwenye maamuzi uwanjani!

Kwa msimu huu unaoishia nimeona mengi kwenye michezo hiyo katika viwanja mbalimbali ambapo kile kinachoitwa Uzalendo kimeonyesha kuvuka mipaka hadi kufikia wakati mwingine mchezaji anadaka mpira akiwa langoni (siyo kipa) halafu mwamzi anaingiwa kigugumizi anatoa mpira nje ya 18 ili kuwaokoa wenyeji wasinyeshewe.

Pia kuna list ya viwanja vyenye vimambo kikiwemo cha Mabatini, Uwanja wa karume waamuzi wanauogopa kishenzi kwakuwa macho ya TFF yapo pale pale!!!.

Leteni burudani tukuze vipaji vya vijana
 
Pamoja mkuu ngoja tuiombee toto Africa akawakilishe Mwanza city.
 
Ligi Daraja la Kwanza 2014/2015 imekwisha rasmi huku timu za Afrikan Sports, Majimaji, Toto Afrika na Mwaduni zikipanda daraja rasmi kwa ajili ya msim ujao 2015/2016.

Ahsanteni sana wadau tuliokuwa pamoja huku jukwaani, Mlendamboga mwenye sredi yako.

Maziku Masunga Jr., Pukudu, Deo Corleone, Ulimakafu, Makoye Matale, Rockcity native, grafani11, BBA, mkolaj, Pumb, Com nyakipambo, mnyikungu, yahoo, miss lucy, mwanguku amanyisye, joriki, Wakutu, Nakapanya, Nyamwega, tamuuuuu, Kifai, Alex Mponela, Makoye Matale, Nemesis, Sodium, SHARO GANGSTAR, kilangi jr, Mtoto wa nzi, ikhatibu, sembo, Landala, Kikwebo, guti, Mtumpole, LoyalTzCitizen, Mr Adam Gella, Masuke, Kaiza2020, kidE Meshack, ACCOUNT FULL, shabhibhii nafwa, Trimmer, na muhuni!

Ahsanteni sana kwa sapoti yenu wakati wote wa ligi, tukutane msimu mwingine wa Ligi Daraja la Kwanza!

Asante nawe pia kamanda.:smile-big:
 
Wakuu, nani mwenye kujua kinachojiri Ligi Daraja la Pili, kuna timu gani za Raia ambazo zinakaribia kupanda? NA timu ngapi zinashuka Ligi Daraja la Kwanza!
 
Back
Top Bottom