Ligi kuu Bara: Azam FC Vs Simba SC

ibesa mau

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2015
Posts
2,109
Reaction score
1,697

Leo ndio vikosi bora vitakuwa uwanjani na baada ya dakika 90 jibu litapatikana kipi ni kikosi bora msimu huu.

Tuanze kwa kujadili vikosi hivyo wakati tukisubiria kipyenga cha muamuzi kuanza mtanange.
=======

KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA

Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.

Dakika 45 + 2:Mchezo hauna kasi na unaweza kuwa mapumziko muda wowote kuanzia sasa.

Dakika ya 45; Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.

Dakika ya 43: Inapigwa faulo, Mavugo anaiunganisha kwa kichwa lakini Manula anadaka na wakati huohuo mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipenga kuonyesha ameotea.

Dakika ya 42: Mnyate anafanyiwa faulo. Inaelekea kwenye lango la Azam.

Dakika ya 37: Azam wanacheza vizuri, wanapigiana pasi na kisha kupiga shuti lakini kipa wa Simba analidaka.

Dakika ya 33: Upande wa kushoto wa Simba kazi ni ngumu kati ya Kapombe na Mohammed Hussein 'Zimbwe JR' ambapo wote ni mabeki wa pembeni lakini wanakuwa wanapanda kusaidia mashambulizi, hivyo kunogesha ushindani wao.

Dakika ya 30: John Bocco wa Azam anapiga shuti kali langoni mwa Simba, kipa anatema kisha anadaka tena.

Dakika ya 28: Mnyate anaingia kwenye lango la Azam lakini mpira unatoka na kuwa goal kick.

Dakika ya 23: Ajib anabaki na kipa Aishi Manula lakini anakosa baada ya Manula kufanya kazi nzuri ya kuokoa hatari hiyo.

Dakika ya 20: Kiungo wa Azam, Migi anaonekana akipambana zaidi eneo la katikati.

Dakika ya 15: Simba wanakuwa wakali wanafanya mashambulizi kadhaa lakini Azam wanakuwa makini wanaokoa.

Dakika ya 7: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja, Azam wamejaribu kufanya shambulizi lakini halikuwa na nguvu. Idadi ya mashabiki ni kubwa waliojotokeza uwanjani hapa.

Dakika ya 5: Mchezo bado haujawa na kasi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.

Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Credits: Updates Kwa hisani ya Saleh Jembe
 
Itakua mechi nzuri sana kwani wote wana vikosi vzr ila ningependa kuona mmojawapo anashinda kwani binafsi sitaki yanga awe bingwa tena
 
Leo ndio vikosi bora vitakuwa uwanjani na baada ya dakika 90 jibu litapatikana kipi ni kikosi bora msimu huu.

Tuanze kwa kujadili vikosi hivyo wakati tukisubiria kipyenga cha muamuzi kuanza mtanange.

Sijui kwa Kikosi hiki Azam anatokaje leo " Shamba la Bibi ":
  1. Vicent Agban
  2. Janvier Bokungu
  3. Mohamed Tshabalala Zimbwe Jr
  4. Novatus Lufunga
  5. Method Mwanjali
  6. Jonas Gerald Mkude ( El Capitano )
  7. Mwinyi Kazimoto
  8. Said Ndemla
  9. Laudit Mavugo
  10. Ibrahim Ajib Mido Fundi Abracadabra
  11. Mohamed Kichuya
Mungu ibariki Simba Sports Club.
 
FT: Azam 1 Simba 3

Jeshi la Simba litakaloanza leo dhidi ya Azam fc mchezo wa ligi kuu ya vodacom

1.Vicent Angban
2.Bokungu janvier
3.Mohamed Tshabalala.
4.Novaty lufunga
5.Method Mwanjali
6.Jonas Mkude
7.Shiza kichuya
8.Mzamiru Yassin
9.Laudit Mavugo
10.Ibrahim Ajibu
11.Jamal Mnyate

Bench.
1.Manyika
2.Hamadi juma
3.Semwanza
4.Ndemla
5.Mohamed Ibrahim.
6.Blagnon
7.Hija ogando
 
Kimetuliaaaaa mnyama anaungurumaaaaa
 
Vipi umerudi lini kimya kimya kujihusisha na maswala ya Simba chini ya utawala ule ule wa Aveva kinyume na kiapo chako hapa?
 
Itakua mechi nzuri sana kwani wote wana vikosi vzr ila ningependa kuona mmojawapo anashinda kwani binafsi sitaki yanga awe bingwa tena
Yanga hawezi kuwa bingwa msimu huu
 
Tunaomba updates jamani kama mpira umeanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…