ibesa mau
JF-Expert Member
- Sep 17, 2015
- 2,109
- 1,697
Leo ndio vikosi bora vitakuwa uwanjani na baada ya dakika 90 jibu litapatikana kipi ni kikosi bora msimu huu.
Tuanze kwa kujadili vikosi hivyo wakati tukisubiria kipyenga cha muamuzi kuanza mtanange.
=======
KIPINDI CHA KWANZA KIMEKAMILIKA
Mwamuzi anapuliza filimbi kukamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika 45 + 2:Mchezo hauna kasi na unaweza kuwa mapumziko muda wowote kuanzia sasa.
Dakika ya 45; Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 43: Inapigwa faulo, Mavugo anaiunganisha kwa kichwa lakini Manula anadaka na wakati huohuo mwamuzi alikuwa ameshapuliza kipenga kuonyesha ameotea.
Dakika ya 42: Mnyate anafanyiwa faulo. Inaelekea kwenye lango la Azam.
Dakika ya 37: Azam wanacheza vizuri, wanapigiana pasi na kisha kupiga shuti lakini kipa wa Simba analidaka.
Dakika ya 33: Upande wa kushoto wa Simba kazi ni ngumu kati ya Kapombe na Mohammed Hussein 'Zimbwe JR' ambapo wote ni mabeki wa pembeni lakini wanakuwa wanapanda kusaidia mashambulizi, hivyo kunogesha ushindani wao.
Dakika ya 30: John Bocco wa Azam anapiga shuti kali langoni mwa Simba, kipa anatema kisha anadaka tena.
Dakika ya 28: Mnyate anaingia kwenye lango la Azam lakini mpira unatoka na kuwa goal kick.
Dakika ya 23: Ajib anabaki na kipa Aishi Manula lakini anakosa baada ya Manula kufanya kazi nzuri ya kuokoa hatari hiyo.
Dakika ya 20: Kiungo wa Azam, Migi anaonekana akipambana zaidi eneo la katikati.
Dakika ya 15: Simba wanakuwa wakali wanafanya mashambulizi kadhaa lakini Azam wanakuwa makini wanaokoa.
Dakika ya 7: Mchezo unachezwa zaidi katikati ya uwanja, Azam wamejaribu kufanya shambulizi lakini halikuwa na nguvu. Idadi ya mashabiki ni kubwa waliojotokeza uwanjani hapa.
Dakika ya 5: Mchezo bado haujawa na kasi, timu zote zinashambuliana kwa zamu.
Dakika ya 1: Mchezo umeanza hapa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Credits: Updates Kwa hisani ya Saleh Jembe