Ligi Kuu Bara: Simba 2-2 KMC FC - Uwanja wa Mkapa, Sept 07 2022

Ligi Kuu Bara: Simba 2-2 KMC FC - Uwanja wa Mkapa, Sept 07 2022

Siamini mpk Yanga wenye kujinasibu wana kikosi Imara wana mrefer Azam,kweli mlipelekewa moto aiseee nyie leo ndo wakuwaheshimu na kuwatolea mfano kikosi cha Azam hahaaaa kweli kombe lileeeee mwenye mbio atalipata.
 
Simba hawakabi kabisa na wanacheza mpira kama wako mazoezini.

Baada ya kufungwa goli la pili na KMC ndio kidogo walicheza mpira.

Mabeki wa Simba kazi yao ni kurudishi mipira nyuma tu basi. Mpaka wanawapasia maadui na wanafuna.
Quttara anapiga mpira wa adhabu anarudisha nyuma.

Ubingwa mwaka huu Simba hata nafasi ya pili hawachukui kwa mpira huu.
Mechi ya Yanga na Azam ndio mechi bora kabisa.
Na leo tungecheza na Yanga au Azam tungepigwa nyingi sana.

Usajiri tu wa msimu huu tumeferi.
Usajiri wa akina Okwa na Mzungu na Okra ni majanga matupu.

Tunawahitaji sana Onyango na Kennedi kidogo wako siriaz. na Kapombe.
Shabalala heshima kwake anajituma sana.
Msimu huu kidogo Mozes Phili anajituma.
 
Acha inyeshe tuone panapovuja-

Tatizo la Simba sio kocha, Kama wengi tunavyoaminishwa! Kwa mtazamo wangu tatizo la Simba ni Uongozi, hasa kipindi hiki Cha Try again na Babra.

Wanasajili wachezaji wa viwango vya kawaida Sana, nadhani wanaangalia Sana gharama kuliko ubora, Mambo yakiwa magumu zigo anaangushiwa kocha, mpaka Sasa ni kocha wa tatu huyu kuachana na timu katika uongozi wao! Mfano Try again aliahidi mwaka huu watavunja bank ili kumpata Adabayo mwisho wa Siku haikuwezekana, hivyo hivyo kwa Manzuki.

Hivi viongozi wamewezaje kufunga usajili huku kukiwa hakuna mshambuliaji no 9, na mkabaji wa chini! Unaendaje kwenye mashindano huku timu haijakamilika!

Wachezaji , Banda, Agpani, Onyango, Okwa na Mzungu wote hawa ni mapro, lakini hawana nafasi ya uhakika kikosi Cha Kwanza, hili ni tatizo, pro anakaa benchi! na wanaoanza baadhi yao viwango vyao vinatia mashaka! Matokeo yake wale tuliodhani wamechoka wanapata nafasi

Mm nashauri uongozi wangetengeneza idara ya kurungenzi ya ufundi, waajiri mtu au watu, wataalamu wa mpira ili wawe wanawashauri hasa kipindi Cha usajili! La sivyo tutakuwa tunapoteza Sana mabegi Airport.
Msimu uliopita hatukufanya vizuri! Kwa sababu hatukusajili vizuri- Kuna viashiria msimu huu pia hatujasajili vizuri,. Viongozi wajitafakali.
Naanza kuamini Barbra ndio mchawi Simba huyu ndio chanzo wachezaji wa mafungu
 
Back
Top Bottom