TAHADHARI. Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, inapenda kuwa tahadharisha wananchi wote juu ya kuchafukwa kwa hali ya hewa kwa mashabiki wa yanga kulikosababishwa na wekundu wa msimbazi leo ktk uwanja wa taifa. Kwa hali hiyo basi, mamlaka inawatahadharisha wanasimba wate pamoja na wapenda amani wengine, kutowapigia simu mashabiki wa yanga kuepuka kunyeshewa na mvua ya matusi. Mamlaka inaongeza kwamba, hata kama ulikuwa na miadi na shabiki wa yanga, usiwasiliane naye hadi baada ya siku mbili au pale mtakavyotaarifiwa vinginevyo na mamlaka. Zingatia haya ili kuepuka usumbufu na madhara yanayoweza kujitokeza.