Habari wakuu, ligi kuu bara inaendelea kwa mechi kadhaa viwanjani. Kutoka uwanja wa Sokoine ubao mpaka sasa unasomeka Mbeya anaongoza kwa goli moja bila majibu likifungwa na Hassan Mwasapili dakika 6, mechi ya Stand na Simba itaanza mishale ya saa kumi unusu. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri.
========
Mbeya City Vs Yanga SC
Mbeya City 2 Yanga SC 1
MPIRA UMEKWISHAAA
-Mahundi kwa Mbeya City, anaingia Issa Nelson
-Mwashiuya anaachia shuti kali kabisa hapa, lakini nje.
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, kipa Mbeya City anaidaka krosi safi ya Msuva kwa ufundi kabisa
Dk 87, shuti kali la Mwashiuya linapaaa juuuu ya lango la Mbeya City
Dk 86, Kessy anaingia vizuri na kuchonga krosi moto, City wanaokoa na kuwa konaaa, inachongwa na Mwashiuya, inaokolewa
Dk 81, bado inaonekana Mbeya City ndiyo wanaonekana kulalia kwenye lango la Yanga
DK 79, Nchimbi anawatoka mabeki wote wa Yanga, yeye na Dida anatoa nje
Dk 75, Niyonzima anaingia vizuri lakini Kenny Ally anamshitukia na kuokoa
SUB Dk 68, Yanga wanamtoa Tambwe na nafasi yake inachukuliwa na Obrey Chirwa
DK 64 sasa, mashambulizi ni kwa zamu na Mbeya City kidogo wanaongeza undava kidogo hasa upande wa walinzi na viungo wakabaji
Dk 59, Msuva anaachia shuti kali hapa lakini linamgonga beki na kuwa konaa, inachongwa haina manufaa
Dk 54, mpira umesimama, Mahundi wa Mbeya City anatibiwa
Dk 52, Niyonzima anawatoka mabeki wawili Mbeya City lakini wanaokoa na kuwa kona, hata hivyo haina matunda
SUB Dk 51, Yanga wanamtoa Kaseke aliyewahi kuichezea Mbeya City na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi kubwa na kupata kona, inachongwa hapa, shuti kali hapa lakini unatoka nje, goal kick...kipa wa Mbeya City yuko chini anatibiwa
MAPUMZIKO
GOOOOOOOO Ngoma anaunganisha krosi ya Msuva vizuri hapa na kuandika bao moja kwa Yanga
-KADI Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ally Ramadhani
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 44, hakuna matumaini kama Yanga wanaweza kusawazisha dhidi ya Mbeya City kwa kuwa hakuna shambulizi kali
Dk 42, GOOOOOOL, mwamuzi anasema lile ni bao lililofungwa na Kenny Ally dak ya 36, hivyo Mbeya City wanaongoza kwa mabao 2-0
Dk 41 sasa, bado mpira umesimama na wachezaji Mbeya City wamekwenda kuwapumzisha mashabiki wao
35, Mbeya City wanaukwamisha mpira wavuni baada ya Kenny Ally kuukwamisha wavuni, lakini mwamuzi anasema kuwa walicheza kabla ya filimbi. Mashabiki na wachezaji Mbeya City naona wanaonyesha hasira hapa, askari wanalazimika kuanza kuzuia vurugu hivi, mpira umesimama sasa
Dk 32, Raphael Alfa wa Mbeya City anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini Dida anaonyesha ujuzi na kupangua, kona. Yanga wanaokoa
Dk 28, Shamte anaachia 'bunduki' kali mpira wa adhabu, safari hii Dida anadaka kwa ustadi mkubwa
Dk 26, Msuva anaachia mkwaju safi hapa lakini kipa Mbeya City anapangua na kuwa konaaaa, inachongwa hakuna majibu mazuri
22' City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga
21' Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii
19' Kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma
19' SUB: upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani.
15' Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa
14' Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili
13' Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda
11' Sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha
06' GOOOOOOO, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi
01' Kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.
=========
Stand UTD Vs Simba SC
Stand UTD 0 Simba SC 1
MPIRA UKWISHAAAAA
-Mnyate anaachia shuti la chinichini hapa lakini ni goal kick
-Mpira unateleza na unaonekana kuwasumbua wachezaji wengi
-Simba wanaonekana kuosha kila mpira unaokwenda langoni mwao
DAKIKA 6 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanapata kona na inakwenda kuchongwa Bukungu, kipa Frank Muonge anajitahidi kudaka vizuri kabisa
SUB Dk 88, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo
Dk 88, mvua imeanza kunyesha uwanjani hapa na mashabiki wengi wanakimbia kutoka majukwaani
Dk 87, Angban yuko chini baada ya kuumia wakati akijaribu kuudaka mpira wakati wa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake
Dk 82, kipa Muhonge anatoka na kumuwahi Mavugo aliyekuwa anakaribia kufunga. Lakini anampiga na mguu tumboni wakati akiokoa
Dk 81, Mavugo anapokeza nafasi mujarab ya kufunga kwa kuwa kipa wa Stand alikuwa ametoka langoni, likiwa wazi MAvugo amepiga nje
SUB 80, Moussa Ndusha ambaye ITC yake imekuja, anaingia kuchukua nafasi ya Kazimoto
SUB Dk 75 Kichuya anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate
DK 70, Wanachofanya Simba, wote wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi kwa kuwatumia watu watatu waende mbele kushambulia ambao ni Kichuya, Mavugo na Mwinyi Kazimoto tu
Dk 67, Kiemba anafanya yake hapa, anamtoka Bukungu na Juuko na kutoa pasi safi
Dk 64, Mo Ibrahim anaingia vizuri, ananyoshaa, unapita juu kidogo
DK 60, Selembe anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Simba, goal kick
Dk 58, Stand wanapata kona inachongwa na Angban anaidaka kwa ulaini kabisa
Dk 56, Job analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa pasi nzuri ya Kichuya iliyokuwa inakwenda kwa Mo Ibrahim. Inakuwa inachongwa lakini haina faida
Dk 53, Stand wanafanya shambulizi kwa mpira wa adhabu, lakini juuuu
Dk 50, Stand wanaonekana kwenda taratibu na zaidi wanamtumia Amri Kiemba ambaye yuko vizuri
Dk 47, mpira umeanza kwa kasi na Stand United wanaonekana wamepania kusawazisha bao
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anapaa kama mkizi na kuunganisha kichwa mpira wa adhabu lakini unatoka sentimeta chache kwenye lango la Stand
Dk 43, hakuna shambulizi kali zaidi ya kila timu kupiga pasi nyingi, Stand wakionekaan kufika zaidi kwenye lango la Simba
Dk 42 sasa, Stand wanaonekana kuongeza mashambulizi mengi zaidi ya Simba ambao wanafanya mashambulizi ya kushitukiza tu
Dk 35, Stand wanapata kona baada ya kusukuma mashambulizi mfululizo kwenye lango la Simba
]Dk 33, GOOOOOOOOO Kichuya aaukwamisha mpira wavuni
Dk 31, PENAAAAAAAT...MAVUGO Anaangushwa na Adeyum
Dk 30, Stand wanafanya shambulizi kali hapa, piga nikupige lakini Simba wanaokoa
KADI Dk 29, Mwanjale analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sabato
Dk 27, mpira unaendelea lakini ni taratibu kutoka kila upande kama vile hakuna timu yenye haraka
Dk 26 sasa, mpira umesimama, kuna mchezaji wa Stand United anatibiwa pale uwanjani
Dk 23, Mo Ibrahim anapoteza nafasi nzuri hapa ya kufunga akiwa amebaki na lango, mpira unamzidi nguvu
Dk 22, mpira unaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali kwenye mlango.
DK 19, Bukungu anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kelvin Sabato
Dk 13, Stand wanaonekana ni wengi zaidi nyumba huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza
Dk 10, mpira unaonekana kuwa wa juu zaidi na hata milango haina kashkash sana, kila timu iko makini kwenye ulinzi
Dk 5 sasa, bado mpira unaonyesha kuchangamka lakini timu zote mbili si bora katika umaliziaji
Dk 1, mechi inaanza na Simba wanakuwa wa kwanza kushambulia. Lakini Mavugo anacheza faulo na mwamuzi anasema mpira uelekezwe Simba
Kwa hisani ya Saleh Jembe