Ligi kuu bara: Simba yaipitia Stand bila kusimama, Yanga yasalimu amri

wp_ss_20161103_0002.png

Plujim akiwaandaa wakina salome
 
Habari wakuu, ligi kuu bara inaendelea kwa mechi kadhaa viwanjani. Kutoka uwanja wa Sokoine ubao mpaka sasa unasomeka Mbeya anaongoza kwa goli moja bila majibu likifungwa na Hassan Mwasapili dakika 6, mechi ya Stand na Simba itaanza mishale ya saa kumi unusu. Tuwe sote pamoja kujuzana yatakayojiri.
========

Mbeya City Vs Yanga SC

Mbeya City 2 Yanga SC 1

MPIRA UMEKWISHAAA

-Mahundi kwa Mbeya City, anaingia Issa Nelson

-Mwashiuya anaachia shuti kali kabisa hapa, lakini nje.

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

Dk 89, kipa Mbeya City anaidaka krosi safi ya Msuva kwa ufundi kabisa

Dk 87, shuti kali la Mwashiuya linapaaa juuuu ya lango la Mbeya City

Dk 86, Kessy anaingia vizuri na kuchonga krosi moto, City wanaokoa na kuwa konaaa, inachongwa na Mwashiuya, inaokolewa

Dk 81, bado inaonekana Mbeya City ndiyo wanaonekana kulalia kwenye lango la Yanga

DK 79, Nchimbi anawatoka mabeki wote wa Yanga, yeye na Dida anatoa nje

Dk 75, Niyonzima anaingia vizuri lakini Kenny Ally anamshitukia na kuokoa

SUB Dk 68, Yanga wanamtoa Tambwe na nafasi yake inachukuliwa na Obrey Chirwa

DK 64 sasa, mashambulizi ni kwa zamu na Mbeya City kidogo wanaongeza undava kidogo hasa upande wa walinzi na viungo wakabaji

Dk 59, Msuva anaachia shuti kali hapa lakini linamgonga beki na kuwa konaa, inachongwa haina manufaa

Dk 54, mpira umesimama, Mahundi wa Mbeya City anatibiwa

Dk 52, Niyonzima anawatoka mabeki wawili Mbeya City lakini wanaokoa na kuwa kona, hata hivyo haina matunda

SUB Dk 51, Yanga wanamtoa Kaseke aliyewahi kuichezea Mbeya City na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya

Dk 46, Yanga wanaanza kwa kasi kubwa na kupata kona, inachongwa hapa, shuti kali hapa lakini unatoka nje, goal kick...kipa wa Mbeya City yuko chini anatibiwa

MAPUMZIKO
GOOOOOOOO Ngoma anaunganisha krosi ya Msuva vizuri hapa na kuandika bao moja kwa Yanga

-KADI Mbuyu Twite analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Ally Ramadhani
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 44, hakuna matumaini kama Yanga wanaweza kusawazisha dhidi ya Mbeya City kwa kuwa hakuna shambulizi kali

Dk 42, GOOOOOOL, mwamuzi anasema lile ni bao lililofungwa na Kenny Ally dak ya 36, hivyo Mbeya City wanaongoza kwa mabao 2-0

Dk 41 sasa, bado mpira umesimama na wachezaji Mbeya City wamekwenda kuwapumzisha mashabiki wao

35, Mbeya City wanaukwamisha mpira wavuni baada ya Kenny Ally kuukwamisha wavuni, lakini mwamuzi anasema kuwa walicheza kabla ya filimbi. Mashabiki na wachezaji Mbeya City naona wanaonyesha hasira hapa, askari wanalazimika kuanza kuzuia vurugu hivi, mpira umesimama sasa

Dk 32, Raphael Alfa wa Mbeya City anaachia mkwaju mkali kwelikweli lakini Dida anaonyesha ujuzi na kupangua, kona. Yanga wanaokoa

Dk 28, Shamte anaachia 'bunduki' kali mpira wa adhabu, safari hii Dida anadaka kwa ustadi mkubwa

Dk 26, Msuva anaachia mkwaju safi hapa lakini kipa Mbeya City anapangua na kuwa konaaaa, inachongwa hakuna majibu mazuri

22' City wanagongeana vizuri tena, Mahundi hatari huyu, anaachia shuti kaliii, hatari kabisa unatoka sentimeta chache kabisa kwenye lando la Yanga

21' Yanga wanagongenaa vizuri hapa, mpira unamfikia Msuva anaachia fataki....wapiii

19' Kipa wa Mbeya City anaokoa mpira hatari wa Donald Dombo Ngoma

19' SUB: upande wa Mbeya City, Hemed Mlutabozwa anatoka baada ya kuumia, anaingia Hemed Ramadhani.

15' Mbeya City nao wanapata kona baada ya krosi ya Maundi kuokolewa na kutoka. Mwasapili ndiye anachonga hapaa, Yanga wanaokoa

14' Msuva anamtoka Mwasapili, krosi safi kabisa lakini City wanaokoa na kuwa kona ya pili

13' Msuva anaingia vizuri na kupiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa lakini haina matunda

11' Sasa, bado Yanga wanaonekana hawajatulia wala kufanya shambulizi kali linaloweza kuwapa City presha

06' GOOOOOOO, Hassan Mwasapili anapiga mpira unaojaa moja kwa moja wavuni baada ya kumshinda kipa Dida Munishi

01' Kila timu imeanza taratibu ikijaribu kutengeneza nafasi lakini hakuna inayocheza kwa papara.
=========

Stand UTD Vs Simba SC

Stand UTD 0 Simba SC 1

MPIRA UKWISHAAAAA

-Mnyate anaachia shuti la chinichini hapa lakini ni goal kick

-Mpira unateleza na unaonekana kuwasumbua wachezaji wengi

-Simba wanaonekana kuosha kila mpira unaokwenda langoni mwao

DAKIKA 6 ZA NYONGEZA

Dk 89, Simba wanapata kona na inakwenda kuchongwa Bukungu, kipa Frank Muonge anajitahidi kudaka vizuri kabisa

SUB Dk 88, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo

Dk 88, mvua imeanza kunyesha uwanjani hapa na mashabiki wengi wanakimbia kutoka majukwaani

Dk 87, Angban yuko chini baada ya kuumia wakati akijaribu kuudaka mpira wakati wa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake

Dk 82, kipa Muhonge anatoka na kumuwahi Mavugo aliyekuwa anakaribia kufunga. Lakini anampiga na mguu tumboni wakati akiokoa

Dk 81, Mavugo anapokeza nafasi mujarab ya kufunga kwa kuwa kipa wa Stand alikuwa ametoka langoni, likiwa wazi MAvugo amepiga nje

SUB 80, Moussa Ndusha ambaye ITC yake imekuja, anaingia kuchukua nafasi ya Kazimoto
SUB Dk 75 Kichuya anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Jamal Simba Mnyate

DK 70, Wanachofanya Simba, wote wamerudi nyuma na wanafanya mashambulizi kwa kuwatumia watu watatu waende mbele kushambulia ambao ni Kichuya, Mavugo na Mwinyi Kazimoto tu

Dk 67, Kiemba anafanya yake hapa, anamtoka Bukungu na Juuko na kutoa pasi safi

Dk 64, Mo Ibrahim anaingia vizuri, ananyoshaa, unapita juu kidogo

DK 60, Selembe anapiga kichwa safi mbele ya mabeki wa Simba, goal kick

Dk 58, Stand wanapata kona inachongwa na Angban anaidaka kwa ulaini kabisa

Dk 56, Job analazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa pasi nzuri ya Kichuya iliyokuwa inakwenda kwa Mo Ibrahim. Inakuwa inachongwa lakini haina faida

Dk 53, Stand wanafanya shambulizi kwa mpira wa adhabu, lakini juuuu

Dk 50, Stand wanaonekana kwenda taratibu na zaidi wanamtumia Amri Kiemba ambaye yuko vizuri

Dk 47, mpira umeanza kwa kasi na Stand United wanaonekana wamepania kusawazisha bao

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anapaa kama mkizi na kuunganisha kichwa mpira wa adhabu lakini unatoka sentimeta chache kwenye lango la Stand

Dk 43, hakuna shambulizi kali zaidi ya kila timu kupiga pasi nyingi, Stand wakionekaan kufika zaidi kwenye lango la Simba

Dk 42 sasa, Stand wanaonekana kuongeza mashambulizi mengi zaidi ya Simba ambao wanafanya mashambulizi ya kushitukiza tu

Dk 35, Stand wanapata kona baada ya kusukuma mashambulizi mfululizo kwenye lango la Simba

]Dk 33, GOOOOOOOOO Kichuya aaukwamisha mpira wavuni

Dk 31, PENAAAAAAAT...MAVUGO Anaangushwa na Adeyum
Dk 30, Stand wanafanya shambulizi kali hapa, piga nikupige lakini Simba wanaokoa
KADI Dk 29, Mwanjale analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sabato

Dk 27, mpira unaendelea lakini ni taratibu kutoka kila upande kama vile hakuna timu yenye haraka

Dk 26 sasa, mpira umesimama, kuna mchezaji wa Stand United anatibiwa pale uwanjani
Dk 23, Mo Ibrahim anapoteza nafasi nzuri hapa ya kufunga akiwa amebaki na lango, mpira unamzidi nguvu

Dk 22, mpira unaonekana kuchezwa zaidi katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali kwenye mlango.

DK 19, Bukungu anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Kelvin Sabato

Dk 13, Stand wanaonekana ni wengi zaidi nyumba huku wakifanya mashambulizi ya kushitukiza

Dk 10, mpira unaonekana kuwa wa juu zaidi na hata milango haina kashkash sana, kila timu iko makini kwenye ulinzi

Dk 5 sasa, bado mpira unaonyesha kuchangamka lakini timu zote mbili si bora katika umaliziaji

Dk 1, mechi inaanza na Simba wanakuwa wa kwanza kushambulia. Lakini Mavugo anacheza faulo na mwamuzi anasema mpira uelekezwe Simba

Kwa hisani ya Saleh Jembe
Sasa mbona niko stendi huku sijamwona huyo simba[emoji86] [emoji86]
 
Mimi ni Yanga ila mwaka huu timu yetu ni kimeo hakuna kombe tutapata labda tujipange next year.
Wakuu zangu Guasa Amboni tAi-kibombo Belo Makoye Matale Nifah 1954 mwambageu Sibonike libeva @Mawembasa1976 brigedia mafia IL Capitano Gide MK logframe Turnkey NIYOMBARE Mtoto wa nzi na nasmapesa mwenzenu tayari kashakiri mapeema..
1. Je.. bado mna wasiwasi na ubora wa huyu mnyama mkali pengine kuliko wote mwituni??
2. Je.. bado hamuamini kua anaenda kutangazwa bingwa wa VPL mapema kabisa mwezi March japo ligi inaisha mwezi April??
 
Simba luala huyo au simba mboje atawatisha wengine lakini sio hawa ulio list hapo juu hawa wanaujua mpira na mashabiki wa ukweli hiyo baiskeli yenu ya tope masika ikifika mtakuwa porini hakuna hata sehemu ya kujibanza (kujificha )mtaloana na ndio mwisho hapo utajipa u busy utakaojipa udhru si udhru ila utapotea sana humu mambo yakianzakwenda halijojo.
 
Hahaha.. Mimi hua najiuliza sana, yaani tutaanzaje kupoteana? Kama;
1. Mikoani Tunashinda
2. Tukikutana na Heavyweight wenzetu Tunashinda
3. Tukikutana na Lightweight au Matawi yenu Tunashinda in style.

Na hata kama ikitokea [japo hili haliwezakani kabisa].. Je lile litimu libovu lililotuaibisha katika uga wa kimataifa, lililojaa mibabu litakua katika hali gani??
 
Mimi ni Yanga ila mwaka huu timu yetu ni kimeo hakuna kombe tutapata labda tujipange next year.
Msimu uliopita mlipoteza mechi ngapi na mlikusanya point ngapi jumla mkapata ubingwa?? Yawezekana kabisa tatizo ni simba kupandisha standards na sio yanga kuwa kimeo.
 
Msimu uliopita mlipoteza mechi ngapi na mlikusanya point ngapi jumla mkapata ubingwa?? Yawezekana kabisa tatizo ni simba kupandisha standards!

Tulipoteza mechi moja tu,ila pia consistence ya ushindi Simba itapandisha points za ubingwa mwaka huu
 
Hahaha.. Mimi hua najiuliza sana, yaani tutaanzaje kupoteana? Kama;
1. Mikoani Tunashinda
2. Tukikutana na Heavyweight wenzetu Tunashinda
3. Tukikutana na Lightweight au Matawi yenu Tunashinda in style.

Na hata kama ikitokea [japo hili haliwezakani kabisa].. Je lile litimu libovu lililotuaibisha katika uga wa kimataifa, lililojaa mibabu litakua katika hali gani??
Uzuri wa wino tofauti na kuchora mchangani japo unasema hilo la kupigwa halipo ila wino upo uzuri mwingine una kipaji cha kujificha pindi mambo yakienda mrama hicho wala sikubishii unaweza sana kujichimbia kuhusu yanga iache hivyo hivyo kizuri chajiuza hizi kelele za mlango tu.
 
Simba luala huyo au simba mboje atawatisha wengine lakini sio hawa ulio list hapo juu hawa wanaujua mpira na mashabiki wa ukweli hiyo baiskeli yenu ya tope masika ikifika mtakuwa porini hakuna hata sehemu ya kujibanza (kujificha )mtaloana na ndio mwisho hapo utajipa u busy utakaojipa udhru si udhru ila utapotea sana humu mambo yakianzakwenda halijojo.

Kumbe ¼ Mupo Wengi Kweli!!!
 
Back
Top Bottom