Ni wazi kuwa inajulikana kuwa mechezo umehitimishwa kwa sare ya Yanga 1 - 1 Simba.
Isingekuwa kukosa umakini kwa Emmanuel Martin na Geoffrey Mwashiuya basi matokeo ya leo yangekuwa ni Yanga 3 - 1 Simba.
Tukiweka pembeni kosa kosa hizo ambazo zilikuwa dhahiri, bado kimchezo wana jangwani wamekuwa ni timu yenye ufanisi zaidi ya Simba uwanjani. Ufanisi huo unaonyeshwa na idadi ya Mashuti yaliyo lenga lango ndani ya dakika 90 za mchezo. Mashuti yaliyolenga lango ni 9 kwa Yanga na 4 kwa simba.
Pia Mabingwa hao watetezi walionekana kushika ufanisi katika idara ya ulinzi. Idara hiyo iliweza kujilinda vyema hata kusababisha upinzani kulazimika kupiga mipira mingi mno nje ya lango la goli. Simba ilikuwa na mashuti 12 nje ya lango la goli ya Yanga.
Licha ya Mabingwa hao kuwakosa wachezaji wake Muhimu kabisa wa kikosi cha kwanza yaani TAMBWE, KAMUSOKO na NGOMA. Bado waliweza kuwaweka kwapani mabingwa wa mwaka 2012 ambao walisheheni wachezaji wenye gharama inayokadiriwa kufuki Bilioni 1 na Milioni 300 kwenye kikosi chao cha kwanza.
Idara pekee ambayo Mabingwa hao walishindwa kuitawala ni umiliki wa mpira.
Mchambuzi maarufu nchini Tanzania aliweza kupata nafasi ya kusema lolote Baada ya mechi hiyo. Na hii ndicho alichokisema:-
"Sikiliza...1-1 Taifa....lakini, Yanga haikuwa na Three key players..Kamusoko, Ngoma na, Tambwe. Na walikosa mabao ya wazi zaidi. Something is missing Msimbazi. Wachezaji hawana authority kubwa uwanjani kama ambavyo rafiki yangu Haji Manara na mashabiki wanataka. Kama unaweza kusema Simba ina Wacheza wengi wapya na inahitaji muda basi hata Yanga leo ilikuwa na wachezaji wapya nusu ya timu. Raphael, Buswita, Gadiel, Ajib, Rostande, Tshishimbi..game pekee ambayo Simb walionyesha authority kubwa uwanjani "
Kikosi hiko cha Mabingwa hao watetezi (chenye thamani ya Milioni 146) sasa wako na alama sawa na Kikosi cha Mabingwa wa mwaka 2012 (chenye thamani ya Bilioni 1 na milioni 300 )
Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligikuu Tanzania wako kwenye mbio a kuhakikisha wanapata kutetea kombe la ligi kuu kwa mara ya anne mfululizo.