lala mbere
Senior Member
- Aug 25, 2016
- 128
- 113
kutana na timu zote sio hii inayoitwa yanga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hahah.... tena si kidogo... yaani hadi kale amekananiliiii 3... looh.Yanga wana "zambi" jamani loh[emoji14]
Kali neuro kwaoYANGA 3-0 AFRICAN LYON 'LIVE' FULL TIME KUTOKA UWANJA WA TAIFA
hongereni watani zetu kwa ushindi MNONO
TAARIFA ZOTE KWA HISANI YA SALEH JEMBE BLOG
![]()
FULL TIME!
Mwamuzi anapuliza kipenga kumaliza mchezo, baada ya bao hilo, mwamuzi anaweka kati kisha mpira unamalizika.
Dakika ya 90 + 4:Chupukizi aliyeingia, Yusuph anapata mpira na kuwatoka mabeki wa Lyon, anampatia Mahadhi pasi ambaye anapiga shuti kali na kujaa wavuni.
GOOOOOOOOOOOOOOOO!!!
Deusi Kaseke anatoka anaingia chipukizi Yusuph Mhilu.
Dakika ya 90 + 2: Lyon wanaonekana kukata tamaa, Yanga wanakuwa wanacheza wao muda mwingi.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika nne za nyongeza.
Dakika ya 89: Kaseke anakosa nafasi baada yakucheza vizuri na Tambwe.
Dakika ya 88: Donald Ngoma anatona na nafasi yake inachukuliwa na Matheo Anthony.
Dakika ya 85: Lyon wanafanya shambulizi lakini inakuwa faulo kutokana na mshambuliaji wao kumsukuma Bossou.
Dakika ya 79: Yanga bado wanaongoza mabao 2-0. Dakika ya 79: Yanga bado wanaongoza mabao 2-0.
Dakika ya 77: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Msuva anaingia Juma Mahadhi
Dakika ya 77: Lyon wanakosa nafasi ya wazi,Ramadhani Kipalamoto anabaki yeye na Dida, anapiga shuti lakini anakosa.
Dakika ya 75: Lyon wanapata faulo nje ya eneo la 18 la Yanga, wanapiga lakini inakuwa offside.
Dakika ya 65: Yanga wanaonekana kuelewana na kucheza ile staili yao ya 'kampa kampa tena'
Dakika ya 63: Yanga wamecharuka, wanaanza kufanya mashambulizi makali, Msuva anapata nafasi nyingine anakosa.
Goooooooooooooooooooooooaaal
Dakika ya 60: Simon Msuva anafunga bao zuri, anapokea pasi ndefu kutoka kwa Kamusoko, Msuva anamptoka kipa wa Lyon na kutupia wavuni, Yanga mbili, Lyon hawajapata kitu.
Dakika ya 51: Mchezo umesimama kwa muda, kuna mchezaji wa Lyon ameumia, anapata matibabu uwanjani.
KIPINDI CHA PILI
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha zinaongezwa dakika tatu.
Dakika ya 44: Yanga wanatulia na kupigiana pasi vizuri, Ngoma na Tambwe wanaonekana kuelewana.
Dakika ya 43: Lyon wanafanya mashambulizi makali katika lango la Yanga, mchezaji HoodMayanja anamtoka Bossou na kupiga shuti kali linatoka nje ya lango na kuwa goal kick.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dakika ya 40: Matokeo bado Yanga wanaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na DEUS KASEKE NA SIO SIMON MSUVA
Dakika ya 38: Hali ya hewa ni ya ubaridi kiasi kwa kuwa kulikuwa na manyunyu katika baadhi ya mitaa ya Dar. Lyon nao wanamka lakini Yanga wanapiga pasi ndefu kuwa kuanzia nyuma.
Dakika ya 36: Lyon wanafanya shambulizi, kipa wa Yanga, Dida anaupangua mpira huo na kisha mabeki wa Yanga wanautoa.
Dakika ya 33: Yanga wanapiga faulo lakini inaokolewa.
Dakika ya 32: Yanga wanapata faulo nje ya eneo la lango la African Lyon.
Dakika ya 29: Yanga wanaendelea kuumiliki mpira muda mwingi wa mchezo.
Dakika ya 20: Yanga wanaendelea kucheza vizuri, Lyon wamepunguza staili yao ya kucheza kwa kutegea wapinzani wao waotee 'off site trick'.
Dakika ya 18: Deusi Kaseke anaipatia Yanga bao la kwanza baada ya mabeki wa Lyon kujua ameotea, kisha akamchambua kipa vizuri.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO!!!!
Dakika ya 10: Mchezo bado haujashika kasi sana kwa kuwa timu zote zinaonekana kucheza kwa kusomana
Dakika ya 15: Yanga wanaonekana kujipanga na kufanya mashambulizi kadhaaa
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
7' Yanga wanashindwa kupata bao, Tambwe anabaki yeye na kipa lakini shuti lake linatoka nje ya lango.
5' Bado matokeo ni 0-0, mchezo haujawa na kasi.
1' Mchezo umeshaanza.
========
Kikosi cha Yanga kilichoanza
1. Deo Munishi ‘Dida’
2. Hassan Kessy
3. Haji Mwinyi
4. Andrew Vincent ‘Dante’
5. Vincent Bossou
6. Thaban Kamausoko
7. Simon Msuva
8. Haruna Niyonzima
9. Donald Ngoma
10. Amiss Tambwe
11. Deus Kaseke
Sub
Kakolanya, Oscar, Pato Ngonyani, Mahadhi, makapu, Mateo, Yusuph
Yanga Vs African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa, leo Jumapili, mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Shukran kwa uungwana wako wa kutimiza ahadi ila bado hujachelewa kufanya maamuzi mtani.Hongereni sana mtani.!
Hahahaha!, hii misemo hii!, mtatuponza wengine tupigwe huku Na wafia timu zao!Mwenye bomba hakai foleni, tumerudi kwenye himaya yetu.
jifunze kuweka akiba ya maneno, na sie tuliposhinda 3 tulikua na maneni kama hayaYanga leo wameonyesha tofauti Kubwa saaana na timu zingine za ligi kuu, kama ya mchangani na zinginezo.. Wanapanga mashambulizi kuanzia chini, hawapigi pigi tu ili ilimradi mpira uende mbele... Kama jamaa wale Ile juzi
*-kweli mkuu,.. nasadiki maelezo yako 100%[emoji3]Yanga leo wameonyesha tofauti Kubwa saaana na timu zingine za ligi kuu, kama ya mchangani na zinginezo.. Wanapanga mashambulizi kuanzia chini, hawapigi pigi tu ili ilimradi mpira uende mbele... Kama jamaa wale Ile juzi
Walisawazisha?Wanawamudu yanga hawa Lyon muda wowote wanasawazisha.!
Hahahaaah mkuu soma post ya kwanza utajua kama walisawazisha au la.!Walisawazisha?
Pole mtanijifunze kuweka akiba ya maneno, na sie tuliposhinda 3 tulikua na maneni kama haya
Huwaga hatufanani na hatutakuja kufanana hata siku moja... Mm nnapowaza niwe kama Mazembe, wewe utawaza uwe kama Yanga,. Sasa lini tutafanana? JkT Ruvu kwako wewe tu kaka...ukumbuke kurudi baada ya mechi na JKT Ruvu
Kwa kuwa JKT Ruvu mlitoa nao sare unadhani watapata pointi kwetu?ukumbuke kurudi baada ya mechi na JKT Ruvu