Ligi Kuu Tanzania Bara, YOUNG AFRICANS Vs KMC machi 10, 2019 kutoka B.W Mkapa Stadium

Ligi Kuu Tanzania Bara, YOUNG AFRICANS Vs KMC machi 10, 2019 kutoka B.W Mkapa Stadium

Yanga mnatakiwa tu mfurahi kwa sababu ya kupata point 3 kwa msaada wa Ally Ally.
Mi nilijua KMC wanapata goli la pili kumbe Ally ameamua awafungie Yanga.
Kweli nimeamini ndo mana Yanga wanatawala vyombo vya habari ili kufunika hujuma zao wanazofanya ili wapate matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama ambavyo AJ Soura wanapaswa kumfurahia Shabalala kwa ile penalti ya goli la pili?
 
Hilo goli la pili la Yanga linatia mashaka. Huyo beki amejifunga vipi kwa mtindo huo? Huyo beki amulikwe!!!!

Tiba
ukishambuliwa sana hakuna namna zaidi ya kujifunga

shaibu ninja wa yanga aliwahi jitwisha ndoo ya namna hiyo tukicheza na ruvu
 
Saa moja walikuwa wa pili,,saa tatu wakawa wa tatu..,saa tano wakawa mikia...
 
Hao wanaamini tigo pesa,ndio maana washajigai pointi za mechi ambazo hawajacheza
Sasa unajuaje kama Mtatoboa kwenye hizo viporo Mtani au unapiga mahesabu ambayo hata kwa wakati huu hayapo.

Kabla hatujacheza na wale MBAO mlisemaga hivi hivi ila mwisho wa siku tukamkalisha huko huko kwao Mwanza na mwisho wa siku mkabaki na bumbuwazi. Hivyo kwa Azam tutawaachia bumbuwazi ka lile.
 
Ukiwa nje ya Tanzania, usisahau code number wakati wa kupiga simu.

+2 5 5

Algeria, Congo na Egpyt. Asante wana Msimbazi kutukumbusha code number yetu.
 
Kwani Ally Ally ananini na Yanga?
ShaffihDauda / Dick Dauda / 7 hours ago

Kwa mara nyingine tena beki wa KMC Ally Ally amehusika katika kuamua mchezo unaoihusisha timu yake dhidi ya Yanga.

Ally Ally amejikuta mchezaji mwenye bahati mbaya kila anapocheza dhidi ya Yanga, leo March 10, 2019 amejifunga kwenye mchezo wa ligi kuu Tanzania bara na kuifanya Yanga kushinda mchezo huo kwa magoli 2-1.

Mchezo wa raundi ya kwanza msimu huu uliochezwa October 25, 2018 Ally Ally alimchezea rafu Heritier Makambo nje kidogo ya box la penati ikiwa ni dakika ya 89 ya mchezo na kupelekea Feisal Salum kuifungia Yanga bao pekee katika mchezo huo kwa mkwaju wa adhabu ndogo.

Kumbukumbu zinaonesha July 10, 2018 Ally Ally wakati akiwa Stand United ya Shinyanga aliwahi kujifunga kwenye mchezo ulioihusisha timu yake dhidi ya Yanga. Ally Ally alijifunga wakati akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na Yusuf Mhilu.

Mambo kama haya ni kawaida kwenye mchezo wa soka, inawezekana Ally Ally huwa anakamia kufanya vizuri kwenye mechi dhidi ya Yanga lakini madhara ya kukamia mechi wakati mwingine husababisha afanye makosa mengi.

Kuna wakati fulani Nemanja Vidic alikuwa na wakati mgumu kwenye mechi za Manchester United dhidi ya Liverpool, kama mechi 4 mfululizo ilitokea anaburuzwa na Torres na kushindwa kumzuia kufunga magoli.

Visit website
 
JF inatumia internet mtandao ukisumbua sasa hata hizi updates utazipataje
Huh, ndio inafahamika JF inatumia internet, sasa kama nipo eneo ambalo internet ni tatizo je? ndio maana unaona nimepost thread nikaacha ili baadae nipate updates kamili na nimeshazipata
 
Back
Top Bottom