Ligi kuu Tanzania bara

Hepatis B

Senior Member
Joined
Feb 11, 2013
Posts
193
Reaction score
155
Kwa kweli ligi kwa sasa ni tamu sana hongereni club zote zanazo shiriki ligi hii matokea ya michezo ya leo ni kwamba mpira sasa umeanza kueleweka kila kona ya Tanzania.

Timu kubwa mjipange sana na mbadilike, mazoea sasa wekeni pembeni point tatu kuchukua sio rahisi kama ilivyokuwa zamani.
 
Utakuwa mgeni wa Ligi ya Tanzania, bila shaka.

Huo ni upepo tu wa mwanzo wa ligi. Ikifika mechi 5,6 timu nyingi huishiwa pumzi. Majeruhi hutokea.

Baada ya hapo sasa, utajua hujui.

Anyway, ngoja tusubiri tuone.
 
Zile millioni mia 500 za azam zimeleta chachu sana kwenye ligi letu pendwa....kataa kubali saivi tupo kwenye moja ya maligi bora africa top 5 hatukosi.
 
Utakuwa mgeni wa Ligi ya Tanzania, bila shaka.

Huo ni upepo tu wa mwanzo wa ligi. Ikifika mechi 5,6 timu nyingi huishiwa pumzi. Majeruhi hutokea.

Baada ya hapo sasa, utajua hujui.

Anyway, ngoja tusubiri tuone.
Yote yanaweza kutokea ila ligi imeanza vizuri sana upinzani kila kona. Timu kubwa zinashangalia kushinda timu ndogo ushindi ni kwa shida sana, kwa hapo kweli nimekuwa mgeni kwenye ligi.
 
TFF waweke makini na rushwa ili kupanga matokeo, hasa kwa hizi team kubwa Simba na Yanga....Serikali kupitia takukuru iweke jicho kwa TFF, waamuzi na baadhi ya wachezaji wa team hizi ndogo ili suala la rushwa lisiwepo kabisa na matokeo halisi yapatikane...
 
Umetisha mkuu umemaliza kila kitu. Mpira uchezwe.
 
Ni kweli ligi imekuwa nzuri ila uwa najiuliza wapanga ratiba kwann Simba na yanga huwa hawachezi mechi za saa 8 mchana, nikipata jibu ntaridhika kuwa hakuna upendeleo
 
Ni kweli ligi imekuwa nzuri ila uwa najiuliza wapanga ratiba kwann Simba na yanga huwa hawachezi mechi za saa 8 mchana, nikipata jibu ntaridhika kuwa hakuna upendeleo
Ligi iliyoisha hata azam sikumbuki lini alicheza saa nane.
 
Ni kweli ligi imekuwa nzuri ila uwa najiuliza wapanga ratiba kwann Simba na yanga huwa hawachezi mechi za saa 8 mchana, nikipata jibu ntaridhika kuwa hakuna upendeleo
Ntibazokiza miaka 43,kagere45 uwachezeshe juani saa nane ili wafe,kuwa serias bro
 
Kuna zile milioni 500 za mgawo kwa kila timu na kuna mgawo kulingana na nafasi utakayoshika mwisho wa msimu. Watauwana hawa majeruhi watakuwa wengi sanaaa .
 
Baada ya raundi kumi, wanaosafiri na Coaster na wanaosafiri na ndege wataanza kuachana mbali.
Mpira ni uwekezaji.
 
Ni kweli ligi imekuwa nzuri ila uwa najiuliza wapanga ratiba kwann Simba na yanga huwa hawachezi mechi za saa 8 mchana, nikipata jibu ntaridhika kuwa hakuna upendeleo
Ni kwa sababu Yanga na Simba ndiyo Vilabu vyenye mashabiki wengi. Hivyo kuchangia kuongeza mapato ya uwanjani.
Muda huo wa saa 8 mchana, mashabiki hao wanakua bado kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.

Kwa hiyo kama kuna upendeleo, basi ni ule upendeleo wa kufa kufaana.
 
Mapato uwanjani ni ishu nyingine kabisa, kuna upendeleo wa wazi kabisa katika vilabu vyetu vya Simba na Yanga tusipobadilika tutaishia kulalamika tu kuwa ligi yetu mbovu maana kiukweli Simba na Yanga wanapaswa kuwekwa kwenye ratiba ya kucheza saa 8.
 
Upendeleo uliopo ni wa kimaslahi tu. Hakuna sababu nyingine. Na ukiona hivyo vilabu vidogo vimeamua kutulia tu huku vikiwa na uwezo wa kutoa malalamiko yao kwenye Bodi ya Ligi, basi unatakiwa ukubali tu matokeo.

Hata mimi pia siungi mkono timu kucheza saa nane mchana! Lakini ndiyo hivyo tena, wanazihitaji hela za Mdhamini (Azam Media) kwa ajili ya kujiendesha.

Na huyo Mdhamini pia angependa kuona watu wengi wakifuatilia matangazo kupitia king'amuzi chake! Na kwa bahati mbaya, hiyo saa 8 watu wengi bado wanakua wako kazini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…