Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

Ni kweli ...uko sahihi...lakini hiki ni kipindi cha mpito...kwani wewe unadhani itapita miaka mitatu bila kibao kugeuka?? itafika muda Yanga itaifunga Simba....Mwaka 1981 Yanga iliifunga Simba baada ya kugaragazwa kwa karibu miaka mitano kikiwemo kipigo cha goli 6-0 cha mwaka 1977 kilichotokana na Yanga kufukuza wachezaji karibu wote 25 na kuamua kuanza upya...goli la Yanga la 1981 lilifungwa na Juma Mkambi kwa kona ya Amasha...kabla ya hapo Simba nayo ilikuwa na kipindi kigumu kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1973 pale ilipojikomboa kwa goli la Willy Mwaijibe...Yanga kwa sasa inajijenga upya...haina kikosi kizuri sana...inashinda mechi zake kutokana na wachezaji kupigwa saikolojia na Zahera na nguvu za wanachama na hasa mikoani...Simba ina kikosi kizuri kwa sasa chenye wachezaji karibu wanane wa kigeni kwenye kikosi cha kwanza..Yanga ya Manji nayo ilikuwa hivyo hivyio lakini kwa waelewa ilikuwa ni wazi kuwa Manji akiondoka Yanga itakuwa kwenye kipindi kigumu ..na hicho ndicho kilichotokea..Ila kwa bahati nzuri Yanga haijasambaratika, bado iko vizuri na kuwashangaza wale wote wasioitakia mema klabu hii..kwa hiyo Yanga itakuja na nguvu mpya muda siyo mrefu ujao...
Mkuu embu tusaidie Udhamini wa Sportpesa kwa Yanga ukoje?
 
ETI KUNA WATU WANADAI PAPAAAAAAAAA ndio aliwapa ile akili as vita ya kuingia na COASTER alafu BASI wakapanda STAFF na Mashabiki wa Clube....watalaamu wanakumbukia mechi ya simba na Yanga,...Yanga waliingia na coaster alafu basi likaja na makomando .......kweli akili za kuambiwa unachanganya na za kwako GOOD BYE VITA CLUBEEE + PAPAAAAA
 
Mungu ndiye anayejuwa wekundu walifukiaga nini pale kwa mchina,hakuna mgeni anayetokaga salama gemu za kwa mchina,hongereni sana.
 
Mi naombeni kujua. Kwa nini nchi zingine champions league zina timu zaidi ya moja.
Nimemsikiliza Mwigulu Nchemba jana kuhusu Simba, akasema wale wenzake wanaoshabikia timu nyingine hawajitambui sababu Simba kama ikifika nusu fainali nchi inapewa nafasi zaidi ya moja champions league, ni kweli?

Kwa kadri team flani inavyofanya vizuri kwenye michuano hii,nafikiri kufika kuanzia semi final,fainali yenyewe na kubeba kombe,ndivyo nafasi za hiyo nchi (ambayo team flani inatoka) zinavyoongezeka!!!
 
Back
Top Bottom