Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

Ligi ya Klabu Bingwa Afrika: Simba SC 2 - 1 AS Club Vita | Simba yafuzu kucheza hatua ya mtoano 2019

HONGERENI WATANI ZANGU KWA KUIWEKA HISTORIA NA KUFIKA QUARTER FINAL AMBAPO MNA ZAIDI YA MIAKA 15 HAMJAFIKA HUKO. JAPO NILIKUWA MKONGO JANA ILA KUWAPONGEZA MUHIMU JAMANI. 🙈

CC. Watani zangu kina Ghazwat, Viol, Mtoto halali na hela , Sesten Zakazaka 100 Likes, Van pebles, OKW BOBAN SUNZU , King Ngwaba , Krizy Beat , BAK , Shunie , toxic9 , Arushaone , Sanchez magoli, Sapta Sapta , Komeo Lachuma, Therapist 2015 , oscarsolomon ,Proved na wengine wengi.

👏👏👏👏👏👏👏👏 MPIRA SI UADUI.
Umekua sasa Shadeeya .wengine hawajui kua mpira sio uadui, ila kwakweli nilishangazwa na wale mashabiki kutoka Kinshasa waliojitokeza kushangilia kwa nguvu sana pale Kazadi alipotupia goli lao pekee nikasema miongoni mwao wewe hukosekani pale😀😀😀😀

Asante kwa pongezi na wewe pole kwa kupapaswa na Lipuli

Uhauri wa bure; UACHE KUHAMAHAMA TIMU
 
Ni kweli ...uko sahihi...lakini hiki ni kipindi cha mpito...kwani wewe unadhani itapita miaka mitatu bila kibao kugeuka?? itafika muda Yanga itaifunga Simba....Mwaka 1981 Yanga iliifunga Simba baada ya kugaragazwa kwa karibu miaka mitano kikiwemo kipigo cha goli 6-0 cha mwaka 1977 kilichotokana na Yanga kufukuza wachezaji karibu wote 25 na kuamua kuanza upya...goli la Yanga la 1981 lilifungwa na Juma Mkambi kwa kona ya Amasha...kabla ya hapo Simba nayo ilikuwa na kipindi kigumu kuanzia mwaka 1968 hadi mwaka 1973 pale ilipojikomboa kwa goli la Willy Mwaijibe...Yanga kwa sasa inajijenga upya...haina kikosi kizuri sana...inashinda mechi zake kutokana na wachezaji kupigwa saikolojia na Zahera na nguvu za wanachama na hasa mikoani...Simba ina kikosi kizuri kwa sasa chenye wachezaji karibu wanane wa kigeni kwenye kikosi cha kwanza..Yanga ya Manji nayo ilikuwa hivyo hivyio lakini kwa waelewa ilikuwa ni wazi kuwa Manji akiondoka Yanga itakuwa kwenye kipindi kigumu ..na hicho ndicho kilichotokea..Ila kwa bahati nzuri Yanga haijasambaratika, bado iko vizuri na kuwashangaza wale wote wasioitakia mema klabu hii..kwa hiyo Yanga itakuja na nguvu mpya muda siyo mrefu ujao...
Wakati huo premier league inaitwa ligi daraja la kwanza. Kwenye mechi hiyo Yanga alimaliza uteja wa miaka mitano mfululizo. Kina Mohamed Kajole Machela, Mohamed Bakari Tall, Athumani Mambosasa, Nicodemus Njohole, Adam Sabu kwa upande wa Simba ndio walikua wanamalizamaliza soka lao huku kwa upande wa Yanga kina Amasha Ahmad, Yusuf Ismail Bana n.k ndio walikua wanaibuka na kikosi cha vijana cha Yanga kikawa kimekomaa kuchukua majukumu
 
Back
Top Bottom