Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20 Simba SC dhidi ya UD do Songo, Yanga SC dhidi ya Township Rollers

Ligi ya Mabingwa Afrika 2019/20 Simba SC dhidi ya UD do Songo, Yanga SC dhidi ya Township Rollers

Hahahaaaa. Hamnaga vitu ka hivyo kwamba mkiishia hatua fulani basi msimu ujao mtafikia zaidi ya pale. Duuuh.

Wacha nisubiri Shadeeya wa watu nione kama hii kauli yako itatimia Ses.
Tuombe uzima tu ili tukutane hapa wewe mwenyewe ukiwa shahidi, ila nitakapokukumbusha wakati huo usije na wewe ukasema 'Sesten kausha"😂😛🤣
 
Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), leo Jumapili Julai 21, 2019 limetoa ratiba ya awali ya michezo ya ligi ya mabingwa wa Afrika CAFCL msimu ujao 2019/2020 ambapo wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano hiyo Simba na Yanga wamepangwa kuanza na timu kutoka ukanda wa COSAFA (kusini mwa Afrika).

Mabingwa wa Tanzania Simba SC, wamepangwa kuanza na UD do Songo ya Msumbiji na wataanza ugenini huku Yanga SC, walioshika nafasi ya pili msimu uliopita kwenye ligi kuu Tanzania wakipangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana.

Kwa mijibu wa ratiba mechi za kwanza za raundi ya kwanza zitapigwa kati ya Agosti 9, 10, na 11 huku mechi za marudiano zikipigwa kati ya Agosti 23, 24, na 25.

Endapo Simba SC na Yanga SC wanafanikiwa kupenya kwenye hatua hiyo, wataingia kwenye raundi ya pili ambapo Simba SC, inakutana na mshindi kati ya Nyasa Big Bullets ya Malawi dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe huku Yanga SC ikikutana na Green Mamba ya Eswatini dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Mechi za raundi ya pili zitapigwa kati ya Septemba 13, 14 na 15 na marudiano itakuwa kati ya Septemba 27, 28, na 29.

View attachment 1158995
Njia unakosea wakati wa kwenda tu.

Yanga Daima mbele,nyuma mwiko
 
KIKOSI KILICHOCHEZA DHIDI YA TOWNSHP ROLLERS MARCH 2018 CHINI YA LWANDAMINA.

Kabwili, Kessy, Dante, Yondani, Ngonyani, Makapu, Tshitshimbi,Buswita, Chirwa, Ajib, Marthin

Kwasasa wamepotea njia kwakweli
 
Simba angekutana na Zesco hatua ya mtoano tungesikia Hemed Kivuyo akisema simba wamekufa kiume na ndio kocha angefukuziwa hapo.
 
Simba angekutana na Zesco hatua ya mtoano tungesikia Hemed Kivuyo akisema simba wamekufa kiume na ndio kocha angefukuziwa hapo.
Hizo kwaya zenu nawaonea huruma... (Makirikiri wameanza safari kuja kufanya yao
 
Back
Top Bottom