Ligi ya Mabingwa Afrika nchini eSwatin: Mbabane Swallows 0 - 4 Simba SC

Ligi ya Mabingwa Afrika nchini eSwatin: Mbabane Swallows 0 - 4 Simba SC

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Simba inashuka uwanjani katika mechi ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 4-1 walioupata kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Novemba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Tujuzane yanayojiri. Je mpira utachezwa saa ngapi?

====

UPDATES:

Pambano la marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Mbabane Swallows na Simba SC unaopigwa kuanzia saa 10:30 Mavuso nchini eSwatin uwanja wa Mavuso.

Dakika ya 28:
Simba wanatangulia kupata bao kupitia kwa Clatous Chama.

Mbabane Swallows 0-1 Simba SC.

Dakika ya 33:
Clatous Chama anaifungia Simba bao la pili.

Mbabane Swallows 0-2 Simba SC.

Dakika ya 53:
Emmanuel Okwi anaifungia Simba bao la tatu dakika ya 52.. Mbabane Swallows 0-3 Simba SC (Agg: 1-6).

Dakika ya 85:
Mbabane Swallows 0-4 Simba SC. Bao la nne la Simba limetoka kwa MK14 Meddie Kagere. (Agg: 1-8).

Dakika 90:
Mpira umemalizika, Simba wanasonga mbele kwa jumla ya mabao 8-1 baada ya leo kushinda 4-0 kwenye mchezo wa maruadiano.

FT: Mbabane Swallows 0-4 Simba SC (Agg: 1-8).
IMG_20181204_182930.png
 
10:30Jioni kwa saa za TZ, ila kule kwao Uswazi itakuwa saa 9:30
 
Tafadhali Aishi Manula kale kajicho kako kakuchungulia kaache !Hapo kuna watoto Balaa!
 
Halafu Waswatini wana amini ushirikina kupindukia! Watoto wa Kariakoo wamejazana Manzini na Mbabane wanapiga hela za uganga wa Kienyeji!
 
Back
Top Bottom