Ligi ya Mabingwa Afrika: Simba SC kung'atana na Mbabane Swallows ya Swaziland

Ligi ya Mabingwa Afrika: Simba SC kung'atana na Mbabane Swallows ya Swaziland

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), limetangaza ratiba ya michuano ya mabingwa wa Afrika na Kombe la Shirikisho barani Afrika katika ngazi za vilabu.

Katika ligi ya mabingwa barani Afrika mabingwa wa Tanzania Simba Sports Club, watakuwa nyumbani Novemba 27/28, 2018 kupambana na Klabu ya Mbabane Swallows, kutoka nchini Swaziland katika hatua ya awali na baadaye kurudiana kati ya Desemba 4/5, 2018 nchini Swaziland.

Na Kombe la Shirikisho barani Afrika, timu ya Mtibwa Sugar, nao wataanzia nyumbani kubabiliana na Northern Dynamo, ya Shelisheli Novemba 27/28, 2018 na kurudiana Kati ya Desemba 4/5, 2018 nchini Shelisheli.View attachment 927780
IMG_20181109_173103_462.jpeg
 
hivi zile kelele za sisi ni wa kimataifa zimeishia wapi

eti hapo jangwani nawauliza
Naona saa hizi kibao kimegeuka zamu yao kuiona dream linner ikikata upepo hewani[emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124] [emoji124]
41710.jpg
 
Hivi Mara ya mwisho Mikia fc kushiriki mashindano haya ilikuwa lini vile? Au no kipindi kile 2003 waipopigwa nje ndani De Liboro ya Angola? Hebu wajuzi was kumbukumbu nijuze tafadhari maana naona wanachonga sana.
 
hivi zile kelele za sisi ni wa kimataifa zimeishia wapi

eti hapo jangwani nawauliza
Mkuu MO11 huo ni msumari kwao hakuna atakayetoa jibu..!

Kuna wakati walisema kwani wao na sisi lini kwenye TPL..Siku ilipowadia kwa jinsi walivyochezeshwa kanyamazongo kwa soka la hakika hadi wakatamani mpira uishe..Unadhani wana hamu tena!
 
Hivi Mara ya mwisho Mikia fc kushiriki mashindano haya ilikuwa lini vile? Au no kipindi kile 2003 waipopigwa nje ndani De Liboro ya Angola? Hebu wajuzi was kumbukumbu nijuze tafadhari maana naona wanachonga sana.
Mwaka uleee Nyerere anazaliwa,

Muweze kushiriki tena club bingwa kwa miaka ya karibun labda Malinzi arudi madarakani
 
Mikia fc alicheza na timu gani vile, hebu tukumbushe mkuu
Mwaka uleee Nyerere anazaliwa,

Muweze kushiriki tena club bingwa kwa miaka ya karibun labda Malinzi arudi madarakani
 
Back
Top Bottom