Ligi ya Mabingwa Afrika | Uwanja wa Taifa, Dar: Simba SC 1-1 UD Songo. Simba yatolewa kwa faida ya goli la ugenini iliyopata UD Songo

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001

Kikosi cha Mnyama

Haya wanaJF ziimebaki dakika chache kuelekea mpambano mkali kati ya Simba Sc na UD Songo.

Mtangazaji wako mwandamizi kwa kushirikiana na wadau wote muhimu tunakueletea moja kwa moja kambumbu kutoka uwanja wa Taifa.

Hamasa ya mashabiki ni kubwa sana. Uwanja wa Taifa unaendelea kujaa.
*****

UPDATES
Simba yatupwa nje ya michuano ya Mabingwa Afrika kwa faida ya bao la ugenini waliyoipata UD Songo kutoka Msumbiji.

UD Songo ndiyo waliokuwa wa kwanza kutikisa nyavu za Simba kupitia kwa nahodha wake Luis kunako dakika 14 ya mchezo.

Goli la kusawazisha la Simba SC, Limefungwa na Erasto Nyoni kwa njia ya mkwaju wa penati kunako dakika ya 86 ya mchezo.

Mchezo wa kwanza Simba SC walitoka Srae ya 0-0 dhidi ya UD Sonko, Hivyo kwa matokeo hayo UD Sonko wanasonga mbele kwa faida ya goli la ugenini.

Simba SC inakuwa ni timu ya pili kutoka Tanzania kutolewa kwenye michuano kimataifa ya CAF, Baada ya klabu ya KMC FC ya Kinondoni kutolewa Ijumaa hii kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…