Ligi ya Mabingwa Afrika | Uwanja wa Taifa, Dar: Simba SC 1-1 UD Songo. Simba yatolewa kwa faida ya goli la ugenini iliyopata UD Songo

Ligi ya Mabingwa Afrika | Uwanja wa Taifa, Dar: Simba SC 1-1 UD Songo. Simba yatolewa kwa faida ya goli la ugenini iliyopata UD Songo

Dah! Mpira una matokeo ya ajabu sana! Yaani Simba walimaliza mchezo kabla ya mechi! Kilichowakuta ni siri yao. Poleni sana watani.

Hivi yule mwanga aliyesema itapita Simba, Azam na KMC yuko wapi yule!
Anapita kimya kimya leo. 😅😅
 
Namuiitaji Demiss aje kuni riwaza jamani, this is Simba baaaaaaana, i think this is not simba i knew
 
Kutolewa kwa Rollers na Orlando Pirates lipo la kujifunza.

Shabiki Nambamoja

Wakati Simba ikiwa imeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya, michezo yake mikubwa ya kirafiki ilikuwa dhidi ya Township Rollers na Orlando Pirates

Michezo yote walitoka sare ya bao 1-1

Ni kipindi hicho mashabiki wa Simba walikuwa wakiibeza Yanga iliyokuwa imeweka kambi mkoani Morogoro wakisema kuwa inacheza na vitimu vidogo, wao wanacheza na wakubwa wenzao

Kilichotokea sasa, Yanga iliyokuwa Morogoro, imeiondosha Rollers iliyoweka kambi Afrika Kusini mwezi mzima!

Orlando Pirates nayo imeondolewa na Green Buffalos ya Zambia kwa kuchapwa mabao 2-1

Hawa ndio wenzetu walisema ni timu kubwa walizopimana nazo huko Afrika Kusini

Kocha Mwinyi Zahera amedhihirisha kuwa mpira ni mbinu tu, mengine yote ni mbwembwe

Haijalishi umeweka kambi wapi, muhimu ni kuwa na mbinu stahili ili uweze kushinda mchezo

Pia michezo ya kirafiki wakati mwingine sio kipimo sana cha uimara wa timu

Kikubwa tuwaombee ndugu zetu wasivurugane na tumuombe Mzee Kilomoni atulie kwanza maana akileta maneno hasira zote zitahamia kwake.

kila mtu karudi nafasi yake Yanga wakimataifa , Simba wa mchangani.
 
Back
Top Bottom