Wewe ni mbishi na unataka kujifanya ni mjuaji wakati hujui. Nilikwambia tokea juu kuwa Yanga walialikwa ila wakayakataa haya mashindano ukasema ni uongo. Badae ukaomba source mdau kakupa bado unakuja na hoja mpya ya mashindano.
Hakuna shaka, Simba na Yanga ni taswira la soka la Tanzania na kila shindano linaloandaliwa huwa linalenga zaidi uwepo wa timu ambayo ni Simba na Yanga kwasababu ya kibiashara na kisiasa.
Hivyo waliotanguliwa kupewa mualiko ili washiriki haya mashindano ni Simba na Yanga kwasababu ndio timu kubwa na kongwe. Kwenye huo mwaliko Yanga alikataa ila Simba ndiye akakubali. Baada ya kukataa Yanga ndipo wakawapa mwaliko Azam na Azam wamekubali. Baada ya kukubali Azam na Simba wakaziteua timu za Zanzibar mbili ili kufanya timu ziwe nne.