Shemasi Jimmy
Member
- Apr 23, 2021
- 93
- 104
LIJUE BARAZA LA SANHEDRIN LILILOTENGENEZA MASHITAKA YA KUMUUA YESU
Wote waliokuwepo katika Baraza wakasimama, wakampeleka Yesu kwa Pilato. 2 Wakafungua mashtaka yao kwa kusema: “Tumemwona huyu mtu akipotosha taifa letu. Yeye anawaambia watu wasi lipe kodi kwa Kaisari na kujiita kuwa yeye ni Kristo, mfalme.”(luka 23:1-2)
Na Shemasi Jimmy 0659 611 252
Ni baraza la wazee 70 wenye uwelewa mpana wa vitabu vya Mishnah na Torati. Liliundwa na kada 4 tofauti
Mafarisayo mfano Nikodemo
- Masadukayo –Josefu kayafa
- Makuhani-kayafa & Anasi
- Wafanyabiashara wenye ushawishi mfano Yusufu Wa Armathaya
- Baraza hilo lilikua limegawanyika katika aina kuu mbili
- Lesser Sanhedrin hili lilikua baraza la wazee 23 hawa walifanya maamuzi katika ngazi ya mkoa.
- The great Sanhedrin hili lilikua baraza la wazee 70 hawa walifanya maamuzi juu ya taifa zima la Israeli, walikua na ushawishi mkubwa kwa jamii nzima ya Israeli. kwa sababu hiyo, serekali ya Rumi ilifanya kila iwezalo kuhakikisha inakua na vibaraka ndani ya baraza hilo muhimu.
- Chanzo cha baraza hili ni wale wazee 70 waliochaguliwa na Musa jangwani ili wawe msaada kwake.
- Hes 11:16 SUV Kisha BWANA akamwambia Musa, Nikusanyie watu sabini, miongoni mwa wazee wa israeli, ambao wewe wawajua kuwa ndio wazee wa watu hawa, na maakida juu yao; ukawalete hata hema ya kukutania, wasimame huko pamoja nawe