Lijue Kabila la Waluguru na utamaduni wao

Lijue Kabila la Waluguru na utamaduni wao

Bwana Banzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
397
Reaction score
196
Asili: asili ya waluguru husemekana kuwa imetokana na watu kutoka maeneo ya chini(low land) kuhamia katika mlima kwasababu mbalimbali kwa mfano mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na njaa na pia kukwepa utumwa wakati wa enzi za utumwa , mfano kuna mapokeo miongoni mwetu kuwa waluguru walikuwa wakiishi pamoja na koo za kizigua, lakini baadae ikatokea kutokuelewana na kuanzia kupigana na watu kukimblia mlimani kwa ajili ya usalama. Pia kuna wanaosema kuwa watu walikuwa wakienda kwa mtu mmoja aliekuwa mlemavu wa mguu (kiguru) kwahiyo wale waliokwenda waliitwa watu wa kiguru (au waluguru).n.k

Wanakopatikana:Waluguru ni mojawapo ya kabila kubwa linalopatikana ukanda wa pwani ya Tanzania, makabila mengine ni wazaramo, wandengereko, wakwere,wakutu,wazigua na wadoe na mengineyo mengi. Kabila hili linalopatikana katika mikoa ya Pwani na Morogoro. Katika mkoa wa Morogoro hupatikana kwa wingi katika wilaya zifuatazo; wilaya ya Morogoro mjini, wilaya ya morogoro vijijini, wilaya ya mvomero na pia wilaya ya kilosa. Katika mkoa wa Pwani hupatikana katika wilaya ya bagamoyo, kibaha na pia hata maeneo ya wilaya ya kisarawe.

Dini: Kwa upande wa dini, waluguru wamegawanyika katika dini kulingana na maeneo, kwa mfano wale walio milimani wengi wao ni wakristo na katika hao wakristo wengi wao ni wakatoliki. Waluguru wanao ishi katika tambarare na maeneo ya Pwani wengi wao ni waislamu,na pia kuna wanaofuata dini za jadi.Uluguruni uislamu na ukristo karibia una idadi sawa za waumini, lakini tukiwa uluguruni au hata sehemu nyingine, huwa hatutenganishwi na tofauti ya imani bali wote huwa kitu kimoja na ushirikiana kwa kila jambo.

Koo za kiluguru: Waluguru wana koo nyingi kama ilivyo kwa makabila mengine, lakini koo za waluguru huwa zinafuata upande wa mama. Baadhi ya koo za kiluguru ni kama zifuatazo: 1. Wamwenda; mwanaume anitwa mkude na mwanamke ni mwenda 2. Wambiki; mwanaume huitwa banzi au zinga au jaka au jakakwa na mwanamke huitwa kina mbiki 3. Wamlali; mwanaume hutwa bwakira na mwanamke ni mlali 4. Wachuma; mwanamke anaitwa chuma na mwanaume anaitwa Luanda 5. Waponda hawa husemwa pia ni wachuma 6. Wakongela, mwanaume mluge na mwanamke ni kongela. 6. Wavinoge (wamaze); mwanaume ni kobelo au belege, mwanamke huitwa kibua au kinoge. 7. Wabena; mwanamke ni kibena na mwanaume ni mbena. 8.Wayingu; mwanamke huitwa makonde na mwanaume huitwa nguya 9. Wamasenga .10. Wamgela mwanaume ni mloka na mwanamke ni mgela 11. Wakiluwa mwanaume mpeka na mwanamke ni kiluwa; 13.wazeru, 14. Wanyagatwa mwanaume msumi na mwanamke anaitwa mtonga 15. Wachilo mwanaume magari na mwanamke ni mchilo 16. waafigwa mwanaume kwembe na mwanamke ni wahindi 17.Wakami, mwanaume anaitwa mkami na mwanamke ni kongera18.wabunga mwanaume nyawale au koba na mwanamke ni bunga 19. walengwe, mwanaume msimbe na mwanamke ni kilegu 20.kinamnyani,mwanaume anaitwa dimoso....koo zipo nyingi tushirikiane kadiri tuwezavyo ili kuweza kuzitaja koo nyingine zilizobaki.

Ngoma za asili: ngoma za asili katika kabila la waluguru ni mdundiko, mkwajungoma, mbeta,zembwela,mchiriku au mnanda, zembwe ( hii upigwa manyanga tu, huku kina mama wakitembelea kila nyumba wakati wa ngoma), Kihamba, gombesugu, vanga. Hizi ngoma hupechezwa mara nyingi wakati wa mavuno

Jando na unyago: kwa kawaida watoto wakiume lazima waingizwe sunnah (kutahiriwa) na hili tendo ufanyika wanapokuwa wadogo, na kwa mabinti wanapovunja ungo hualikwa (huwa mwali-umoja, uwingi-wali) na kufundishwa kuwa mama bora kwa maisha ya baadae… na akisha maliza kuwa mwali hupelekwa mkoleni na kisha kunemwa kwa kutumia ngoma yoyote, yaweza kuwa mdundiko au kwa kutumia ngoma yoyote itakayopendekezwa.

Salamu kwa waluguru: waluguru huwa na salamu kulingana na wakati katika siku, kwa mfano asubuhi husalimiana kwa hivi; A. Aulamke? Au tza mitondo? B. anoga, imanye gwegwe? (B najibu).....mchana husalimiana hivi; A. Ausindile? au kwa mgima? B. Na mgima,imanye gwegwe? Au anoga imanye gwegwe? na jioni pia husema hivi; tza nemiye? usiku husema tza nechilo?

Watani wa waluguru: watani wa waluguru kwa upande wa watu wa kutoka maeneo ya bara ni pamoja na Wanyamwezi, Wasukuma, na pia wengineo ni wapogoro na wambunga,washambaa, wazigua

Vyakula;
waluguru hupendelea kula vyakula vifuatavyo: Ubwabwa(wali), Mkembe (bondo), ng'andulo( ugali uliokobolewa na mahindi kulowekwa kisha kutengeneza unga) ,ugali,Magimbi,Mafenesi, Mihogho, Machungwa, Ng'owo(ndizi), Mighughwa, Mashelisheli,Natzi, Masasa, Mastafeli, Mapela, Mabowa, Mananasi, Mvighonzo, Mvikwaji, Mapapaya, Ngadu, Mangala, Nguruka, Mwidu, Betze, Bwasi, Mnamvu, kalabwagila (mboga maboga), mlenda mgunda, mlenda lanzi lanzi.

Hayo ni machache kuhusu kabila la waluguru. Naamini mtakuwa mmejifunza kitu ndugu zangu wapendwa kutokana na maelezo niliyowapa, kwa anaefahamu zaidi anaweza pia kutuongezea kitu nasi tujifunze……..kumbuka unaweza kuta baadhi ya mambo kama si yote yanafanana na kabila la WAZARAMO au WAKUTU au hata WAKWERE, usishangae kwa sababu wote ni watu wa kabila lenye chanzo cha sehemu moja isipokuwa harakati za maisha tu ndio zika zaa majina tofauti. ahsanteni kwa kusoma na kuthamini nilichokiandika.
 
Mweeeh! Sio kila kitu, vingine sumu, kalaga bao masai dada
 
Asante kwa bandiko mkuu nimejifunza 🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Asante kwa bandiko mkuu nimejifunza 🙏🙏🙏🙏🙏🙏
Shukrani kaka kwa kunipa moyo kwa nilichoandika, furaha ya mwalimu ni pale anapopata majibu kuwa ameeleweka. Ahsante nawe pia ndugu
 
nyama ya ngombe mtuachie bana
kila kitu nyinyi
Ahaa haaaa! Ni kweli, kwanza hao ng'ombe wenyewe tunawaogopa sembuse kumchinja, sisi twala mboga za majani, unalujua DEREGA? Ukila hilo utasahau nyama kabisa ndugu yangu..jaribu uone
 
Back
Top Bottom