Lijue soko la HISA

Habari ndugu zangu wapendwa wa jukwaa hili tumaini langu la dhati wote ni wazima wa afya na ndomaana tukaweza kukutana hapa kujuzana na kufundishana mambo tofauti ya kijamii, siasa na hata uchumi

Lengo langu la kuandika uzi huu naomba kufahamu ni vipi naweza kupata faida endapo nikanunua hisa katika kampuni yoyote ile ambayo inajihusisha na uuzaji wa hisa. Na faida au gawio huwa linakuwa kila baada ya mda gani miezi kadhaa, mwaka au baada ya miaka kadhaa.

Na pia kwaambaye anaufahamu zaidi juu ya masuala ya uuzaji na ununuzi wa hisa ningependa anifumbue macho namna ya kutafuta gawio baada ya kampuni kulata faida.

Natumaini kupata mchango chanya katika maswali yangu.

Asanteni.
 
Fuatilia taarifa Za minada ya hisa inayo fanyika katika soko la DSE kupitia taarifa mbalimbali ikiwepo website yao pamoja Na vyombo mbalimbali vya habari. Acha uvivu wa kutafuta Habari, chukua hatua. Uvivu Na uzembe haiwezi kukutoa hata siku moja.
 
jamani kuna hizi index naomba anaejua zinatumika vipi anijuze maana nimejaribu kizifatilia mara ziwe negative mara postive ila sioni nini kinachozibadilisha plz naomba mtu anijulishe
 
Mkuu hivi Vodacom hapo awali walikua wanauza hisa au ndo wameaza sasa hivi?
 
Wakuu hivi Vodacom hapo awali walikua wanauza hisa au ndo wameaza sasa hivi?
 

Soma mwanzo wa uzi huu.Jamaa ameelezea kwa undani majibu ya maswali yako.
Acha kusoma uzi kuanzia katikati!
 
Kuna mtu aliuliza kama Dangote wanauza hisa lkn sijaona jibu, na mm nauliza swali hilo hilo. Je, Dangote wanauza hisa au watauza? Na ni lini? Jibu tafadhali.
 
Wakuu,

Nilikuwa nahitaji msaada wa kujua soko la hisa nchini Tanzania kama ifuatavyo;
1.Linaendeshwa vipi?
2.Kianzio cha kuwekeza hisa ni kiasi gani kwa mtu anayeanza.
3.Je kuna matawi mikoani ya kuwekeza HISA?
 
mkuu Mimi na laki tano tu ambayo nahitaji kununulia hisa na lengo langu bei hisa ikipanda niiuze basi sasa maswsli yangu niyafuatayo
1.Je laki tano wataikubali?

2.Je naweza nunua hisa hata huku mikoani
 
Wadau wa Jf kuna fursa katika kampuni inayoitwa Bitco International ...
kampuni hii inahusika na investment ya coin iitwayo Bitcoin ambapo utainvest hela yako na utapata return ya 3% kila siku kwa muda wa siku 50.Bitcoin ni coin maarufu sana kwenye mataifa ya ulaya na America kwa muda mrefu sasa na pia imeanza kutumika katika matumizi ya kawaida kama fedha nyingine huko kwa wenzetu.
hii fursa ni real na na watu wanaendesha maisha yao kupitia bitco international.Kwa hapa kwetu Tanzania fursa hii bado ngeni ,ila wachache walioichangamkia wananufaika ikiwamo na mimi.

Uthubutu ni kitu muhimu sana katika mafanikio ya mwanadamu,nawashauri msikubali hii fursa iwapite .

kwa yeyote ambaye atahitaji maelezo ya kina na kujiunga anitafute kwa namba hii 0712 799747 au whatsapp kwa namba hiyo hiyo ,mimi nipo Dar.
 
mkuu Mimi na laki tano tu ambayo nahitaji kununulia hisa na lengo langu bei hisa ikipanda niiuze basi sasa maswsli yangu niyafuatayo
1.Je laki tano wataikubali?

2.Je naweza nunua hisa hata huku mikoani
1. Wataikubali laki 5 yako.
2. Unaweza, wasiliana na brokers.
 
Naomba kujua nani anapanga kuwa kampun fulani ina hisa mfano 200
Wanaangalia nini kupanga hiyo idadi
 
Naomba kuuliza..nawezaje kununua hisa kwnye masoko ya nje ya nchi.?na kama naweza je kuna njia za online kununua na kufanya malipo kwnye masoko ya hisa ya nje ya nchi.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…