Lijue soko la HISA

Lijue soko la HISA

Naomba kuuliza..nawezaje kununua hisa kwnye masoko ya nje ya nchi.?na kama naweza je kuna njia za online kununua na kufanya malipo kwnye masoko ya hisa ya nje ya nchi.?

You can use brokers in Europe, you need to specify which instruments you want to invest:

kuna FX, CFDs, Shares na Binary Options

follow the link below: Looking to invest money online?

Hili pia ni swali la kwangu. Wadau tafadhali saidia I hapa

see above

Hili swali mbona halijibiwi

see response above;

if you want more details quote and i will check your response.
 
Samahani mkuu kam una maelezo ya kutosha elezea tu apa tukakuelewa..mfano nataka kununua hisa NEW YORK STOCK OF EXCHANGE,nafanyaje kununua online na malipo yake yafanyike online..tupe maelezo ya kutosha tu unafanyaje
 
ok. this is how i started (nimetafsiri kidogo)

1. unawasiliana na broker yoyote unayemtaka kutoka kwenye list niliyotuma;
2. atakupa form ya kujaza, utatoa mpaka account ya benki unayotaka kulipia na kuchukua faida (ni vizuri ukiwa na benki account tofauti na ya matumizi mengine)
3. ata-verify account kwa kutumia mbinu tofauti kuhakikisha kwamba pesa ni halali na unasema wewe ni wewe, maana broker wengi wako mbali na wewe (hii itachukua muda kutokana na umbali etc)
4. atakuuliza kiasi gani unataka kuweka kwenye "trading stock account" na currency gani unataka (Euro, US Dollar au GB Pound) hizi ni main currencies
5. anaweza kukushauri opportunities/fursa zilizoko na atakweleza risk na unataka uwe exposed kiasi gani kwenye shares unazotaka kununua na ni kiasi gani hizo share;
6. basi unanunua na kuuza - au uza na kununua (unaweza kutengeneza pesa kwa movement tofauti) - remember stock price have 3 movements, up, down or sideways
7. unaweza kununua kutoka kwenye nchi zilizoendelea na kila broker ana access kwenye market segment fulani

niko tayari kujibu maswali zaidi - KARIBUNI
 
Nashukuru mkuu kwa maelezo yako mazuri na nimekuelewa..ila ww binafsi una shauri nin kuhusu kununua hisa nje ya nchi,zinalipa au bado ni bahati nasibu kam bongo tu
 
kwa nje, opportunities ziko nyingi sana, kwa DSE kuna makampuni 25 tu (18 nationwide and crossovers) ila kwa nje ya nchi kuna zaidi ya instruments zaidi ya 5,000 hili neno instrument ni jina linalotumika sana kwenye soko la dunia - lina maanisha shares/CFDs za makampuni mbalimbali kama pepsi, yahoo. google, apple etc, fedha za nchi mbalimbali kama japan, uk, us, australia etc, commodites kama gold, oil, sugar, cotton etc, stocks/indices kama spx, nas100 etc
 
Habari ya muda huu wana jf..,

Bila kuwachosha, nina swali nahitaji kufahamu juu ya faida za hisa.

Natamani kununua hisa kwa sasa kutoka katika kampuni yoyote ile na hii itakua ni mara yangu ya kwanza, hivyo basi ningependa kufahamu kuwa faida za hisa au gawio (dividend) huwa zina range katika kiwango gani kwa hisa moja peke yake.
Najua kuwa gawio huwa linategemeana na faida iliopata kampuni kwa muda wa biashara ila ninahakika kuna makadirio ya faida huwa yanaendana kwa kila hisa moja na kwa kila kampuni. Mfano hisa moja gawio linaweza likawa mara mbili ya bei ulionunulia na kadhalika.

Wataalam naomba nipatieni mwanga..,
 
Ni kipindi muhimu kujua kuhusu hisa. Hivi karibuni utakuwa umesikia makampuni mbalimbali hasa yale ya simu yakiwatangazia watu kununua hisa. Ni muhimu kwako kujua kuhusu biashara hii. Huenda ikawa ya faida kwako au eneo zuri kwako kwa kuwekeza.

Mapema niseme kuwa usiogope wala usiwe mwenye hofu. Biashara ya hisa ni ya watu wote tajiri au maskini. Laki moja, laki mbili nk. unaweza kununua hisa. Ili umiliki hisa kwenye kampuni ya simu si lazima umiliki mamilioni kama unavyodhani. Na hapa ndipo tunapokosea na kuwaacha matajiri watambe nasi tubaki kulalamika.

1. HISA NI NINI?

Hisa ni mali kama zilivyo mali nyingine unazomiliki. Tofauti ya hisa na mali nyingine ulizonazo kama shamba, gari, nyumba nk.ni kuwa mali nyingine huweza kushikika au kuonekana kwa macho wakati hisa ni mali isiyoonekana kwa macho. Yumkini zote ni mali tu.

Hisa ni maslahi au haki fulani unayokuwa nayo katika taasisi au kampuni fulani. Ndiyo maana ni mali isiyoonekana kwasababu huwezi kuona maslahi au haki kwa macho.

2. KUMILIKI HISA KATIKA KAMPUNI.

Kampuni yoyote unayoiona huwa inao wanahisa. Wanahisa ndio wamiliki wa kampuni. Kwahiyo hata wewe ukinunua hisa kwenye kampuni yoyote na wewe unakuwa mmoja wa wamiliki.

Haijalishi ukubwa wa kampuni na kiwango chako cha hisa ulichonunua bali ni kuwa ukishanunua tu hapohapo na wewe unakuwa mmoja wa wamiliki. Hata hisa za laki moja nazo zinakufanya kuwa mmoja wa wamiliki.

Kiwango cha hisa zako ndicho kiwango cha umiliki wako. Kampuni ikiwa na hisa 100,000 na wewe ukamiliki hisa 50,000 basi wewe unaimiliki nusu ya kampuni. Ukimiliki hisa 25,000 basi wewe unamiliki robo ya kampuni. Halikadhalika ukimiliki hisa 500, 100, 50, 10, 5 au hata hisa 3 basi hichohicho kiwango chako cha hisa ulichonunua ndicho kiwango chako cha umiliki wa kampuni husika.

Kwahiyo ukinunua hisa 100 Vodacom basi wewe utaimiliki Vodacom kwa kiwango cha hisa hizo ulizonunua. Isipokuwa ni muhimu kujua kuwa anayemiliki hisa nyingi kuliko wote ndiye hujulikana kama mmiliki mkuu wa kampuni.

3. JE, UTAFAIDIKAJE NA HISA?

Kila mwanahisa hupata gawio la faida pale kampuni inapotangaza faida. Kampuni hutangaza faida kila baada ya mwaka au nusu mwaka au vinginevyo.

Utapata mgao kwa asilimia kutokana na kiwango chako cha hisa ulizonazo. Ukiwa na hisa nyingi utapata mgao mkubwa, ukiwa na hisa kidogo utapata mgao mdogo na vivyo hivyo.

4. HISA HUPATIKANA VIPI?

Kampuni husika hutangaza kuuza hisa zake pamoja na bei ya kila hisa. Bei ya hisa moja inaweza kuwa Tshs 1,000/=, 10,000/= nk. Lakini pia kampuni nyingi huweka kima cha chini cha hisa unazotakiwa kununua, mfano kampuni itasema tunauza hisa kuanzia hisa 100 au 50 na si chini ya hapo nk.

Kwahiyo wewe utafuata sharti hilo na mengine yatakayokuwa yamewekwa na utanunua hisa unazotaka.

5. JE, UKINUNUA HISA UNAPEWA NINI?

Ukinunua hisa unapewa cheti cha umiliki wa hisa. Cheti cha umiliki wa hisa ndicho ushahidi kuwa wewe unamiliki hisa katika kampuni fulani. Cheti hicho kama hisa zote ulizochukua umezilipia vizuri na hudaiwi unaweza kukitumia kukopea hela katika mabenki, kama dhamana mahakamani nk.

Cheti cha umiliki wa hisa ni sawa ni sawa na hati ya nyumba/kiwanja, au kadi ya gari na vyombo vingine. Hati hizi zinavyoweza kutumika ndivyo na cheti cha umilki wa hisa kinavyoweza kutumika.

6. JE UNAWEZA KUUZA HISA BAADA YA KUNUNUA.

Ndio, hisa ni bidhaa kama bidhaa nyingine. Unaweza kununua hisa leo na kesho ukiwa na shida ya hela ukauza. Katika makampuni ya umma ( PLC) kama haya ya simu unaruhusiwa kumuuzia yeyote utakayemuona amefika bei.

Ni kiasi gani uuze hakuna anayekupangia. Ni biashara kama biashara nyingine yoyote. Unaweza kuwa umenunua hisa kwa tshs 1,000,000/= lakini ukauza hata 5,000,000/=. Ni wewe tu na mteja wako. Na unaruhusiwa hata kumtumia dalali kukutafutia mteja.

Lakini pia unaweza kuamua kuuza baadhi ukamaliza shida yako na ukabakiza baadhi. Si lazima kuuza zote.

Hayo ni kwa uchache tu kuhusu hisa

Like page ya @tanzania_yetu iliyoko facebook kwa mengine mengi zaidi
 
Asante sana kwa elimu hiyo Mungu akubariki="Davion Delmonte Jr., post: 14102944, member: 179011"]
Habarini wana jukwaa, leo nimejiskia kuandika kuhusu soko la hisa kwa hapa Tanzania. Nimeona baadhi ya watu walikua wakiuliza sasa si vibaya hata wakapata kufahamu ni kitu gani hichi. Huu utakuwa ni mwendelezo wa zile mada zangu za uwekezaji kwenye dhamana za serikali (treasury bond + bills) na biashara ya fedha za kigeni. kwa hiyo unaweza kuijumlisha na hii.
Hisa ni nini ?

Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara. Kwa hiyo unapomsikia mtu akisema anamiliki hisa kwenye kampuni fulani, basi ujue ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia za hisa anazomiliki. Mfano kama kampuni ama biashara ina jumla ya hisa 100 na wewe ukanunua hisa 20 basi wewe ni mmiliki kwa asilimia 20.
Unaponunua hisa pia kuna mtu ambaye anakuwa anaziuza kwa wakati huo huo ndipo wewe ukapata nafasi ya kuzinunua kutoka kwake. Hivo unatakiwa utambue kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinazouzwa sokoni kama nyanya au vitunguu. Vivo hivyo kama mfano wa nyanya na vitunguu zokoni, kwenye hisa pia kuna wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa katika soko ambalo tunaliita soko la hisa.
Soko hili la hisa kama masoko mengine tu ya bidhaa mfano unapokwenda soko la karume utakutana na madalali ambao wao kazi yao inakuwa ni kukushawishi wewe ununue katika duka fulani bila ya wewe moja kwa moja kukutana na mmiliki haswa wa biashara, na biashara ikishafanyika wao kuna kiasi wanakichukua kama ada ya kufanya udalali wa kuuza na pesa nyingine ndiyo inakwenda kwa mmiliki wa biashara. Vivo hivyo katika masoko ya hisa utakutana na madalali kama hawa ambao tunawaita �brokers�. Pindi unapotaka kununua au kuuza hisa lazima upitie kwao kwanza kwa sababu katika hisa, wao ndio haswa wana uhalali wa kisheria kushiriki moja kwa moja katika soko la hisa.
Soko la hisa kwa Tanzania

Tanzania pia kama nchi nyingi za ulimwengu wa kileo nasi tuna soko letu la hisa ambalo ni Dar es salaam stock exchange DSE kwa wasio fahamu DSE ipo jengo la Golden Jubilee Tower floor 10. Soko letu la hisa ambalo naweza kusema ni changa ukilinganisha na masoko ya nchi nyingine lina takribani makampuni 21.
Kama nilivooleza awali kwa Tanzania ukitaka kununua au kuuza hisa zilizo orodheshwa na DSE utatakiwa kwanza upitie kwa brokers ambao huwa wanakuwa na taarifa kamili za bei zilizopo sokoni kwa wakati huo na mabroker wengi wanatoa huduma ya ushauru kuhusu kufanya maamuzi ya kununua au kuuza maana ni watu wenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya hisa. Kwa Tanzania tuna mabroker kama Orbit Securities Co. Ltd, Rasilimali Limited, Solomoni Securities Ltd, Core securities Ltd, Tanzania securities Ltd, Vertex International Securities japo pia kuna bank zina act kwa niaba ya mabroker fulani mfano CRDB Bank kwa hiyo ina maana hapo banki pia unaweza kuweka order ya kununua au kuuza hisa.
Kingine muhimu kabla ya kuuza au kununua hisa lazima uwe na account ya banki ambayo malipo mengi yatapitia huko pale unapouza au pindi ukipata gawio lako la hisa kutokana na faida ya kampuni.
Umuhimu wa kuwekeza kwenye hisa

Mwekezaji katika hisa anaweza kufaidika kwenye mambo yafuatayo yanayotokana na umiliki wake wa hisa.
i) Gawio la hisa (dividend) kwa sababu tumeshaeleza hapo juu kwamba ukimiliki hisa unahesabika wewe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hivo basi pale kampuni inapopata faida kuna gawio ambalo utapata kulingana na idadi ya hisa unazomiliki. Mfano kwa mwaka kama huu banki ya CRDB ilitangaza gawio la sh. 15 kwa kila hisa moja. Lakini hapa kwenye gawio sio lazima kupata kila mwaka kutegemeana na sera za kampuni. Kama kampuni haipati faida ama ipo kwenye kujitanua ina maana faida itayopatikana itawekwa kwenye kupanua kampuni.
ii) Kupanda kwa bei ya hisa kunatoa fursa ya kuongeza utajiri wako kama ukiamua kuuza. Hapa naongelea personal portfolio ya mtu binafsi kukua kama itatokea bei ya hisa itapanda. Mfano mzuri kwa wale walionunua hisa za NMB mwaka 2009 kwa shilingi 600 na leo hii hisa ya NMB ni 2900 kwa hiyo unaona kuna ongezeko kama la 2300 kwa kila hisa uliyonunua 2009. Ikiwa na maana kama ungeweka 12,000,000 ungenunua hisa 20,000 ambazo kwa leo hii kama ungeziuza ungekuwa na kitu kama 58,000,000. Sasa can you imagine after seven years ile milioni 12 inakupa pesa ya kununua apartment ya NHC sio faida hiyo?
iii) Zaweza kutumika kama dhamana ya kuombea mkopo katika taasisi zinazotoa mikopo. Hapa tunaongelea kitu kinachoitwa stock-secured loans. Kwa taasisi za fadha wanaweza kutupa muongozo namna ya kutumia hisa zako ili ziwe dhamana ya mkopo. Lakini kitu kikubwa kabisa ni kwamba sio kila hisa yaweza kutumika kama dhamana. Kinachoangaliwa hapa ni liquidity ya hisa nikiwa na maana zile hisa ambazo zinauwezekano wa kuuzika kwa haraka na zenye bei iliyo stable ndizo hasa taasisi za fedha wanazipa kipaumbele kwa sababu zinakuwa na hatari kidogo. Kwa Tanzania hapa naweza kusema hisa kama za TBL, TWIGA CEMENT, CRDB, TCC, NMB na SWISSPORT naweza kusema zipo more liquid na unaweza kutumia kama dhamana bila usumbufu wowote.
iv) Zinahamishika, ikimaanisha zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako. Kwa nchi za magharibi ambazo masoko yake ya hisa yamekuwapo kwa zaidi ya karne moja. Kuna hisa ambazo mpaka sasa zinamilikiwa na watu lakini zilinunuliwa miaka mingi iliyopita na mababu zao. Utaongelea makampuni kama J.P Morgan, General Electric, Ford, GM nk ambazo umiliki wa hisa umetembea vizazi na vizazi.
Who is who in stock investing?

Nimeandika kwa kiingereza kuweka msisitizo. Nikiwa na maana kwamba nataka kuonesha nguvu ya kuwekeza katika soko la hisa inaweza kukufanya uwe mtu wa namna gani katika ulimwengu wa sasa.
Uwekezaji katika hisa umetengeneza matajiri wakubwa katika ulimwengu wa sasa. Watu kama kina Warren Buffet, Carl Icanh, George Soros na wengineo wengi. Hao niliowataja hawakugundua chochote kwenye maisha yao kama mabilionea akina Bill Gates, Larry Elison, Steve Jobs, Henry Ford na wengineo wengi. Ila utajiri wao haswa ulitokana na kuwekeza kwenye hisa.
Mtu kama Warren Buffet na Carl Icanh leo hii wanamiliki makampuni mengi ambayo hawakuyaanzisha wenyewe bali wameyamiliki kwa kununua hisa mpaka wakawa major shareholders.
Hata kwa nchi kama Tanzania huwezi kuamini kuna watu wametengeneza utajiri wa ajabu kwa hisa hizi hizi unazoziona pale DSE. Binafsi nilibahatika kukutana na mtu akaniambia yeye alinza kuwekeza kwenye hisa mwaka 1999 na mpaka wakati ananisimulia ananiambia alikua na portfolio ya karibu milioni 500. Sasa hapo unaweza kufikiri mwenyewe how fast kuwekeza kwenye hisa kunaweza kukufanya kwa kiasi fulani na wewe ukaonekana na wewe ni mtu fulani.
Lakini don�t be carried away easily kama kawaida kutengeneza utajiri kunahitaji akili. Sio tu kwa sababu unapesa basi unaenda na wewe kununua hisa. Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla ya kwenda kununua hisa. Huu ni uwekezaji kama uwekezaji mngine ambao unakuwa na hatari (risks). Saa nyingine unaweza kwenda kununua hisa lakini kumbe kampuni inaenda kufa siku za mbeleni. Au pia kampuni haioneshi mwelekeo wowote wa kufanya vizuri siku za mbeleni. Kwa hiyo inamaana hapo kwa lugha ya kihuni utakua umeingia choo cha kike hahahahahahah. Maana kama kampuni hai perform, haitengenezi faida ina maana 1) bei ya hisa itashuka halafu 2) hisa zitakua haziuziki tena kwa hiyo hamna namna yoyote ya kurudisha pesa ulizowekeza. Mfano tu hapa Tanzania kuna kampuni kama Precision Air ambalo halijawahi kutoa dividend kwa shareholders na hisa zake pale DSE haziuziki maana hazihitajiki kwa sababu kampuni hai perform.
Ushauri kutoka kwa Buffet.

Ili uweze kufanikiwa katika uwekezaji wako wa hisa na huko mbeleni uweze kuchekelea utajiri ulioukusanya kama yule rafiki yangu wa milioni 500, ni budi kujua unawekeza kwenye hisa za makampuni yapi.
Kujua mbinu murua za kuwekeza kwenye hisa ntaleta mezani na kujadili kiufupi njia ambazo aliziainisha bilionea Warren Buffet ambaye kama nilivooleza hapo juu ni moja ya mwekezaji wa hisa kuwahi kutokea mpaka sasa kwenye dunia hii.
Ntajaribu kuweka baadhi tu ya njia au mambo makubwa ya kuangalia kabla ya kufikia maamuzi ya kuwekeza kwenye hisa. Katika njia hizo Buffet aliziorodhesha katika makundi manne ambayo ni 1) viashiria vya biashara yenyewe (business tenets) 2) menejimenti ya kampuni husika (management tenets) 3) viashiria vya kifedha (financial tenets) 4) viashiria vya soko kwa kampuni husika (market tenets).
Buffet anashauri kwamba ukishajiridhisha na utafiti wako kwenye kampuni fulani dhidi ya viashiria kwenye makundi hayo manne basi ndio wasaa mzuri wa kufanya uwekezaji kwenye hisa zake na baadae uje na wewe uchekelee.
Katika viashirio hivo kuna maswali mwekezaji unatakiwa ujiulize kama
- Je biashara au kampuni nnayotaka kuwekeza inaeleweka ?
- Je biashara au kampuni ina historia gani ya uendeshaji wake (operating history)?
- Je biashara au kampuni ina future yoyote nzuri kwa kipindi cha mda mrefu ujao (favourable long term prospects)?
- Je menejimenti ya kampuni au biashara ina ufanisi wa kufanya maamuzi?
- Je menejimenti ya kampuni ina uhusiano mzuri na kuaminika na shareholders?
- Je kampuni inapata faida?
- Je gawio la hisa la kampuni linaleta maana?
- Je thamani halisi ya biashara ni ipi ?
Ikiwa utajiridhisha na maswali hayo hapo juu kwa kiwango cha at least cha asilimia 70 za kuridhika basi nenda kanunue hisa. La umeridhika kwa asilimia 30 halafu wewe unaenda kununua, hapo hutakua tofauti na mtu anayecheza kamari kudhani kwamba mambo mbeleni yatakuwa mazuri akati viashiria havioneshi hivo.
Nimeliona sana hili tatizo kwa Tanzania hapa, mtu akishasikia IPO basi yeye ana rush tu kwenda kununua bila hata kupima angalau viashiria vichache hapo juu. Kwa nchi za wenzetu biashara hii inachukuliwa kwa umakini mkubwa sana na hata wengine kabla ya kununua wana seek advice kwa wataalamu wa masoko ya hisa.
Na ndio maana leo hii tunawashuhudia watu kama kina Warren Buffet, kama ingekuwa hawana umakini wowote wa kuwazua kabla ya kufanya maamuzi ya kuwekeza wasingekuwa hapo walipo.
Kwa hiyo ndo hivo, sio wote wana akili kama za Buffet ila pia haikuzuii kutumia akili yako kufanya uchanganuzi wa kuwekeza kwenye hisa na baadae ije kukulipa. Maana ieleweke kwamba unachokiwekeza ni pesa zako kwa hiyo sio vema kufanya maamuzi ya kupoteza pesa bila kuwa na uhakika angalau kwa asilimia fulani.
Mwisho kabisa kwa sababu hii ni elimu pana na hapa nimetoa tu kamwanga ningependa kusikia kutoka kwenu pia wana jukwaa maana naamini kuna watu wanajua mambo mengi mnoo kwenye hii field. Cc Bavaria
Asanteni sana, nawatakia uwekezaji mwema
Vince Forum
[/QUOTE]
 
Habarini wana jukwaa, leo nimejiskia kuandika kuhusu soko la hisa kwa hapa Tanzania. Nimeona baadhi ya watu walikua wakiuliza sasa si vibaya hata wakapata kufahamu ni kitu gani hichi. Huu utakuwa ni mwendelezo wa zile mada zangu za uwekezaji kwenye dhamana za serikali (treasury bond + bills) na biashara ya fedha za kigeni. kwa hiyo unaweza kuijumlisha na hii.

Hisa ni nini ?

Kwa lugha rahisi kabisa hisa inawakilisha sehemu ya umiliki katika biashara. Kwa hiyo unapomsikia mtu akisema anamiliki hisa kwenye kampuni fulani, basi ujue ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia za hisa anazomiliki. Mfano kama kampuni ama biashara ina jumla ya hisa 100 na wewe ukanunua hisa 20 basi wewe ni mmiliki kwa asilimia 20.

Unaponunua hisa pia kuna mtu ambaye anakuwa anaziuza kwa wakati huo huo ndipo wewe ukapata nafasi ya kuzinunua kutoka kwake. Hivo unatakiwa utambue kwamba hisa ni kama bidhaa nyingine zinazouzwa sokoni kama nyanya au vitunguu. Vivo hivyo kama mfano wa nyanya na vitunguu zokoni, kwenye hisa pia kuna wanunuzi na wauzaji ambao wanakutanishwa katika soko ambalo tunaliita soko la hisa.

Soko hili la hisa kama masoko mengine tu ya bidhaa mfano unapokwenda soko la karume utakutana na madalali ambao wao kazi yao inakuwa ni kukushawishi wewe ununue katika duka fulani bila ya wewe moja kwa moja kukutana na mmiliki haswa wa biashara, na biashara ikishafanyika wao kuna kiasi wanakichukua kama ada ya kufanya udalali wa kuuza na pesa nyingine ndiyo inakwenda kwa mmiliki wa biashara. Vivo hivyo katika masoko ya hisa utakutana na madalali kama hawa ambao tunawaita brokers. Pindi unapotaka kununua au kuuza hisa lazima upitie kwao kwanza kwa sababu katika hisa, wao ndio haswa wana uhalali wa kisheria kushiriki moja kwa moja katika soko la hisa.

Soko la hisa kwa Tanzania

Tanzania pia kama nchi nyingi za ulimwengu wa kileo nasi tuna soko letu la hisa ambalo ni Dar es salaam stock exchange DSE kwa wasio fahamu DSE ipo jengo la Golden Jubilee Tower floor 10. Soko letu la hisa ambalo naweza kusema ni changa ukilinganisha na masoko ya nchi nyingine lina takribani makampuni 21.

Kama nilivooleza awali kwa Tanzania ukitaka kununua au kuuza hisa zilizo orodheshwa na DSE utatakiwa kwanza upitie kwa brokers ambao huwa wanakuwa na taarifa kamili za bei zilizopo sokoni kwa wakati huo na mabroker wengi wanatoa huduma ya ushauru kuhusu kufanya maamuzi ya kununua au kuuza maana ni watu wenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya hisa. Kwa Tanzania tuna mabroker kama Orbit Securities Co. Ltd, Rasilimali Limited, Solomoni Securities Ltd, Core securities Ltd, Tanzania securities Ltd, Vertex International Securities japo pia kuna bank zina act kwa niaba ya mabroker fulani mfano CRDB Bank kwa hiyo ina maana hapo banki pia unaweza kuweka order ya kununua au kuuza hisa.

Kingine muhimu kabla ya kuuza au kununua hisa lazima uwe na account ya banki ambayo malipo mengi yatapitia huko pale unapouza au pindi ukipata gawio lako la hisa kutokana na faida ya kampuni.

Umuhimu wa kuwekeza kwenye hisa

Mwekezaji katika hisa anaweza kufaidika kwenye mambo yafuatayo yanayotokana na umiliki wake wa hisa.

i) Gawio la hisa (dividend) kwa sababu tumeshaeleza hapo juu kwamba ukimiliki hisa unahesabika wewe ni mmoja wa wamiliki wa kampuni hivo basi pale kampuni inapopata faida kuna gawio ambalo utapata kulingana na idadi ya hisa unazomiliki. Mfano kwa mwaka kama huu banki ya CRDB ilitangaza gawio la sh. 15 kwa kila hisa moja. Lakini hapa kwenye gawio sio lazima kupata kila mwaka kutegemeana na sera za kampuni. Kama kampuni haipati faida ama ipo kwenye kujitanua ina maana faida itayopatikana itawekwa kwenye kupanua kampuni.

ii) Kupanda kwa bei ya hisa kunatoa fursa ya kuongeza utajiri wako kama ukiamua kuuza. Hapa naongelea personal portfolio ya mtu binafsi kukua kama itatokea bei ya hisa itapanda. Mfano mzuri kwa wale walionunua hisa za NMB mwaka 2009 kwa shilingi 600 na leo hii hisa ya NMB ni 2900 kwa hiyo unaona kuna ongezeko kama la 2300 kwa kila hisa uliyonunua 2009. Ikiwa na maana kama ungeweka 12,000,000 ungenunua hisa 20,000 ambazo kwa leo hii kama ungeziuza ungekuwa na kitu kama 58,000,000. Sasa can you imagine after seven years ile milioni 12 inakupa pesa ya kununua apartment ya NHC sio faida hiyo?

iii) Zaweza kutumika kama dhamana ya kuombea mkopo katika taasisi zinazotoa mikopo. Hapa tunaongelea kitu kinachoitwa stock-secured loans. Kwa taasisi za fadha wanaweza kutupa muongozo namna ya kutumia hisa zako ili ziwe dhamana ya mkopo. Lakini kitu kikubwa kabisa ni kwamba sio kila hisa yaweza kutumika kama dhamana. Kinachoangaliwa hapa ni liquidity ya hisa nikiwa na maana zile hisa ambazo zinauwezekano wa kuuzika kwa haraka na zenye bei iliyo stable ndizo hasa taasisi za fedha wanazipa kipaumbele kwa sababu zinakuwa na hatari kidogo. Kwa Tanzania hapa naweza kusema hisa kama za TBL, TWIGA CEMENT, CRDB, TCC, NMB na SWISSPORT naweza kusema zipo more liquid na unaweza kutumia kama dhamana bila usumbufu wowote.

iv) Zinahamishika, ikimaanisha zinaweza kuwa kama urithi kwa watoto wako. Kwa nchi za magharibi ambazo masoko yake ya hisa yamekuwapo kwa zaidi ya karne moja. Kuna hisa ambazo mpaka sasa zinamilikiwa na watu lakini zilinunuliwa miaka mingi iliyopita na mababu zao. Utaongelea makampuni kama J.P Morgan, General Electric, Ford, GM nk ambazo umiliki wa hisa umetembea vizazi na vizazi.

Who is who in stock investing?

Nimeandika kwa kiingereza kuweka msisitizo. Nikiwa na maana kwamba nataka kuonesha nguvu ya kuwekeza katika soko la hisa inaweza kukufanya uwe mtu wa namna gani katika ulimwengu wa sasa.
Uwekezaji katika hisa umetengeneza matajiri wakubwa katika ulimwengu wa sasa. Watu kama kina Warren Buffet, Carl Icanh, George Soros na wengineo wengi. Hao niliowataja hawakugundua chochote kwenye maisha yao kama mabilionea akina Bill Gates, Larry Elison, Steve Jobs, Henry Ford na wengineo wengi. Ila utajiri wao haswa ulitokana na kuwekeza kwenye hisa.

Mtu kama Warren Buffet na Carl Icanh leo hii wanamiliki makampuni mengi ambayo hawakuyaanzisha wenyewe bali wameyamiliki kwa kununua hisa mpaka wakawa major shareholders.

Hata kwa nchi kama Tanzania huwezi kuamini kuna watu wametengeneza utajiri wa ajabu kwa hisa hizi hizi unazoziona pale DSE. Binafsi nilibahatika kukutana na mtu akaniambia yeye alinza kuwekeza kwenye hisa mwaka 1999 na mpaka wakati ananisimulia ananiambia alikua na portfolio ya karibu milioni 500. Sasa hapo unaweza kufikiri mwenyewe how fast kuwekeza kwenye hisa kunaweza kukufanya kwa kiasi fulani na wewe ukaonekana na wewe ni mtu fulani.

Lakini dont be carried away easily kama kawaida kutengeneza utajiri kunahitaji akili. Sio tu kwa sababu unapesa basi unaenda na wewe kununua hisa. Kuna vitu vingi sana vya kuangalia kabla ya kwenda kununua hisa. Huu ni uwekezaji kama uwekezaji mngine ambao unakuwa na hatari (risks). Saa nyingine unaweza kwenda kununua hisa lakini kumbe kampuni inaenda kufa siku za mbeleni. Au pia kampuni haioneshi mwelekeo wowote wa kufanya vizuri siku za mbeleni. Kwa hiyo inamaana hapo kwa lugha ya kihuni utakua umeingia choo cha kike hahahahahahah. Maana kama kampuni hai perform, haitengenezi faida ina maana 1) bei ya hisa itashuka halafu 2) hisa zitakua haziuziki tena kwa hiyo hamna namna yoyote ya kurudisha pesa ulizowekeza. Mfano tu hapa Tanzania kuna kampuni kama Precision Air ambalo halijawahi kutoa dividend kwa shareholders na hisa zake pale DSE haziuziki maana hazihitajiki kwa sababu kampuni hai perform.

Ushauri kutoka kwa Buffet.

Ili uweze kufanikiwa katika uwekezaji wako wa hisa na huko mbeleni uweze kuchekelea utajiri ulioukusanya kama yule rafiki yangu wa milioni 500, ni budi kujua unawekeza kwenye hisa za makampuni yapi.
Kujua mbinu murua za kuwekeza kwenye hisa ntaleta mezani na kujadili kiufupi njia ambazo aliziainisha bilionea Warren Buffet ambaye kama nilivooleza hapo juu ni moja ya mwekezaji wa hisa kuwahi kutokea mpaka sasa kwenye dunia hii.

Ntajaribu kuweka baadhi tu ya njia au mambo makubwa ya kuangalia kabla ya kufikia maamuzi ya kuwekeza kwenye hisa. Katika njia hizo Buffet aliziorodhesha katika makundi manne ambayo ni 1) viashiria vya biashara yenyewe (business tenets) 2) menejimenti ya kampuni husika (management tenets) 3) viashiria vya kifedha (financial tenets) 4) viashiria vya soko kwa kampuni husika (market tenets).

Buffet anashauri kwamba ukishajiridhisha na utafiti wako kwenye kampuni fulani dhidi ya viashiria kwenye makundi hayo manne basi ndio wasaa mzuri wa kufanya uwekezaji kwenye hisa zake na baadae uje na wewe uchekelee.

Katika viashirio hivo kuna maswali mwekezaji unatakiwa ujiulize kama

- Je biashara au kampuni nnayotaka kuwekeza inaeleweka ?
- Je biashara au kampuni ina historia gani ya uendeshaji wake (operating history)?
- Je biashara au kampuni ina future yoyote nzuri kwa kipindi cha mda mrefu ujao (favourable long term prospects)?
- Je menejimenti ya kampuni au biashara ina ufanisi wa kufanya maamuzi?
- Je menejimenti ya kampuni ina uhusiano mzuri na kuaminika na shareholders?
- Je kampuni inapata faida?
- Je gawio la hisa la kampuni linaleta maana?
- Je thamani halisi ya biashara ni ipi ?

Ikiwa utajiridhisha na maswali hayo hapo juu kwa kiwango cha at least cha asilimia 70 za kuridhika basi nenda kanunue hisa. La umeridhika kwa asilimia 30 halafu wewe unaenda kununua, hapo hutakua tofauti na mtu anayecheza kamari kudhani kwamba mambo mbeleni yatakuwa mazuri akati viashiria havioneshi hivo.

Nimeliona sana hili tatizo kwa Tanzania hapa, mtu akishasikia IPO basi yeye ana rush tu kwenda kununua bila hata kupima angalau viashiria vichache hapo juu. Kwa nchi za wenzetu biashara hii inachukuliwa kwa umakini mkubwa sana na hata wengine kabla ya kununua wana seek advice kwa wataalamu wa masoko ya hisa.

Na ndio maana leo hii tunawashuhudia watu kama kina Warren Buffet, kama ingekuwa hawana umakini wowote wa kuwazua kabla ya kufanya maamuzi ya kuwekeza wasingekuwa hapo walipo.

Kwa hiyo ndo hivo, sio wote wana akili kama za Buffet ila pia haikuzuii kutumia akili yako kufanya uchanganuzi wa kuwekeza kwenye hisa na baadae ije kukulipa. Maana ieleweke kwamba unachokiwekeza ni pesa zako kwa hiyo sio vema kufanya maamuzi ya kupoteza pesa bila kuwa na uhakika angalau kwa asilimia fulani.

Mwisho kabisa kwa sababu hii ni elimu pana na hapa nimetoa tu kamwanga ningependa kusikia kutoka kwenu pia wana jukwaa maana naamini kuna watu wanajua mambo mengi mnoo kwenye hii field. Cc Bavaria

Asanteni sana, nawatakia uwekezaji mwema

Vince Forum
Jana usiku nilikuwa nasoma post Kama hii inayo husu hisa.

Kiukweli kwa Sasa nimekuwa mpenzi mkubwa wa kutaka kujifunza kuhusu Jambo hili.

Very soon nitanunua hisa kwenye bank ya Crdb naona wanafanya vizuri sana
 
Back
Top Bottom